m

"If you want to conquer fear, don't sit at home and think about it. Go out and get busy. "

-- Dale Carnegie, motivational expert

Friday, 28 February 2014

YODAE: MBEBA MAONO NI LAZIMA AWE MTII NA MWENYE KUFUATA MAELEKEZO

Shalom Mpendwa.
Mwanzo: 37
Ninaendelea kujifunza kutoka kwa Mbeba maono Yusufu. Watu wengi tunamtazama Yusufu kam ambeba maono tu, lakini kumbe hatupaswi kuishia hapo tunatakiwa kuangalia namna alivyoyabeba maono na nguvu iliyomwezesha kubeba maono yake.

Maono ni jambo la kwanza, kubeba ni jambo la pili na nguvu ni jambo la tatu. Unaweza ukawa na maono lakini maono yako yakafa kwa sababu umeshindwa kubeba, wakati mwingine unaweza ukayabeba maono lakini ukashindwa kuendelea nayo kwa. Mpenzi kuinua mzigo ni jambo rahisi lakini kuendelea nao ama kupiga hatua nao ni jambo lingine gumu sana kwani inategemea nguvu ya misuli uliyonayo.

Binafsi naamini hakuna kijana aliyekosa maono ikiwa ana imani thabiti kwani Yoeli 2:28 inatamka wazi kuwa vijana wataona maono. Vijana wengi wanalo jambo la kufanya lakini hawajatambua na waliotambua wameshindwa kubeba. Lazima kuwa mwanagalifu unapokuwa na maono.

Kubeba maono ni kama kubeba YAI, yai si kiumbe chenyewe bali kasha lililobeba kiumbe kumbe kulivunja ni kuvunja kiumbe na kulitunza vizuri ni kutunza kiumbe kijacho. Kwa mfano kufikiri kuanzisha shule ni sawa na yai kwani mawazo yamebeba shule lakini si shule yenyewe.

Unapobeba maono kunakuwa na changamoto nyingi ambazo zinaweza kuharibu au kuua kabisa maono yako.

Kwa leo hebu tujifunze kwa Yusufu nguvu iliyomsaidia kubeba maono. YUSUFU ALIKUWA MTII NA MWENYE KUFUATA MAELEKEZO katika safari yake ya maono. Ndugu unapobeba maono umeanza safari ni kama kuku anapoatamamia yai, kutotoa kwa vifaranga kutategemea namna ambavyo atadhamiria kuatamia mayai yake.

AMUA KUATAMIA MAONO YAKO

Yusufu alikuwa mtii kweli kwani tunamtazama akiwa na umri wa miaka 17 tu tayari ameanz kuota ndozo zinazotoa maelekezo ya maono yake...nini atafanya kwa wakati gani na kwa nani.

Utii unaonekana kwa Yusufu kwanza kila alipoota kamsimulia baba yake na familia yake mst. 2, 5 na 9. Pili Yusufu alipotumwa kwenda kuwaona nduguze bado anaendelea na desturi ya utii kwani inaoneka anaenda mahali asipojua vizuri ndio maana anapofika anauliza wapo wapi ndugu zake na hapo tena utaona namna Yusufu anavyopenda kufuata maelekezo kwani anauliza. Hizi ni tabia za kawaida kwa mtu lakini zina maana sana kwa ajili ya kutunza maono. Mst 15

Utii wa Yusufu ndio uliopelekea kuweza kubeba maono yake, Kwani Ysufu unafiak wakati nduguze wanamkamata wanamvua kanzu bao hatuambiwi kama alileta matata bali alitii, wanamtumbukiza kisimani bado hakuleta matata akatii, wanamuuza bado akatulia akatii, Wamidiani wanamchukua hadi Misri bado anatii na tena wamidiani wanamuuza kwa Potifa bado anatii (kama angeleta matata ingeandikwa).

Kumbe kama umebeba maono ni lazima uwe mtii, unaweza kukumbana na mugumu wakati wa maono lakini yakupasa uchukulia kama changamoto tu, Yusufu aliandaliwa kuwa mtawala lakini tunaona natawaliwa na ndugu zake na hata utumwani jambo ambalo ni kinyume na alivyoona. Yeye anaona kutawala lakini yanayotokea ni kutaliwa na hata kutaka kuuawa. mst 23, 24, 27, 28, 36.

Maisha ya ushindi ni pamoja na kuwa na maono, wengine waimngia dhambini kwa sababu hawana maono, hawajui nafasi yao na wanapoelekea.

Ikiwa umebeba maono kubali kuwa mtii kwa Mungu mwenyewe, viongozi wa Imani na wakati mwingine hata watawala kwani hujua ni nani atakayeweza maono yako, maono yatatekelezeka kutia nani. Yusufu ilikuwa kupitia nduguze na hatimaye Farao