m

"If you want to conquer fear, don't sit at home and think about it. Go out and get busy. "

-- Dale Carnegie, motivational expert

Saturday, 6 April 2013

BIBI ANAYEDAI KUISIKIA SAUTI YA MUNGU


Amani usiamini! Bibi kizee Veronica Amos Kayombo (76), mwenyeji wa Ludewa, Njombe anayeishi Buza, Dar, amedai kuisikia sauti ya Mungu ikimuagiza akaonane na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete ampe ujumbe muhimu, shuka nayo.

MAHOJIANO MAALUM

Akizungumza katika mahojiano maalum mwanzoni mwa wiki hii akiwa nyumbani kwake Buza, Bibi Veronica alisema amekuwa akitokewa na Mungu mara kwa mara na kumpa maelekezo mengi ambayo anatakiwa kuyatoa pale atakapofika kwa Mheshimiwa Rais Kikwete.


ATOKEWA NA TASWIRA YA MUNGU
“Nimekuwa nikitokewa na taswira na sauti ya Mungu, kwa idadi inaweza kufika mara saba na kuambiwa 
kuwa nisiondoke Dar, bila kuonana na Kikwete ili nimpe zawadi zake ambazo nimezitunza kwa muda mrefu na siri iliyoko moyoni ambayo nimepewa na Mungu,” alisema bibi kizee huyo.

KWA NINI JK?
Aliendelea kusimulia kwa masikitiko kuwa zawadi atazompatia JK ni kwa ajili ya kumpongeza kwa kuweza kuwasaidia albino, watu wasiojiweza, wazee na kutuliza vita nchini Kenya na Uganda ambazo zilikuwa zimejifichwa kwani nchi nyingine kama Rwanda na Burundi zilikuwa wazi.

ANATOKEA NJOMBE
Bibi Veronica alifika Dar akitokea Njombe kwa ajili ya mazishi ya mama yake mdogo na baada ya kumaliza msiba alijiandaa kuondoka lakini Mungu alimtokea 6:00 mchana na kumweleza kuwa asiondoke hadi atakapoonana na JK.

ATUMIA MKWANJA MREFU
Baada ya hapo amekuwa akifanya jitihada za aina mbalimbali kwa ajili ya kuonana na rais lakini hadi sasa hajafanikiwa kwani ameshapoteza fedha nyingi kwa kuwahonga watu ili wamfikishe Ikulu pale Magogoni, Dar na kutoa kopi za barua kwa ajili ya kuomba maombi ya kukutana naye.
“Nimepoteza fedha nyingi sana kila ninayekutana naye ananiambia atanipeleka lakini nimpatie fedha, natoa mpaka sasa nimeishiwa, nimeshaenda mpaka ofisi zote zinazohusika na kuwakutanisha watu na rais lakini sikufanikiwa, watu wamekuwa wakiniona chizi lakini nina akili zangu timamu na maono haya ni ya Mungu kwani mbali na kuambiwa pia la kufanya nikifika huko lipo kwenye kitabu hiki (anaonesha Biblia).
Bibi kizee huyo alipoona ameshahangaika huku akizuia kila mara kuingia Ikulu, aliamua kuita vyombo mbalimbali vya habari na kufikisha ujumbe wake ambapo mbali na hapa gazetini pia radio zitarusha matangazo yake moja kwa moja yatamfikia Rais Kikwete.

AMPA ZAWADI LOWASSA, MKAPA
Kwa mujibu wa bibi Vero, aliwahi kukutana na aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa ambaye alimpatia gunia la mahindi na zawadi za Rais wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa na mkewe Mama Ana Mkapa alipokuwa kwao Njombe.
Kumbukumbu zinaonesha kuwa mama huyo wakati anatoa zawadi hizo alioneshwa kwenye vyombo vya habari ambapo alitoa kitenge cha mama, gunia la mahindi na zawadi ya rais huyo mstaafu.

CHANZO GPL

KII proposed Institute, Join us...Karibu

The proposed Institute which have a great desire to serve people, Our world is emerging dependance on Information technology and Poor states including Tanzania are facing difficulties in supplying IT services, the important role is to look on how we can make IT affordable to the whole community.
Join with KII to serve the community in IT, Information and Counseling needs. We need to have a center which everybody will run to get service.
For us Habari ni Maisha "Information is Life"
Good Information brings progress and cure life while bad and wrong information destroy life progress.

Hatari! Tanzania kinara ulevi wa 'mataputapu'

Pombe ya kienyeji ikiandaliwa tayari kupelekwa kwa walaji 

Ni jambo la hatari kabisa kwa nchi maskini kuwa kinara wa ulevi, binafsi sifikiri kama watu walevi wanaweza kuendelea. Ukitembea maeneo mbalimbali nchini Tanzania utakuta majukumu ya malezi wameachiwa wanawake wanaume kazi yao kulewa tena mataputapu jambo ambalo linasababisha kurudisha nyuma maendeleo ya familia na Taifa kwa ujumla. Hebu fikiri mtu atawezaje kufikiri juu ya kesho ikiwa masaa 24 kalewa chakari, je pesa ya kunywea anatoa wapi bila kufanya kazi. Ama kweli hii ni Hatari na ni lazima watu wageuke na zaidi asasi mbalimbali zikiwemo vyama vya siasa vipige kampeni za kuondoa ujinga huu wa ulevi, na hapo ndipo tunaweza kuzungumza maendeleo. 

Baada ya utangulizi huu habari kamili kwa mujibu wa Mwananchi.co.tz inataarifu utafiti unaoonyesha ulevi barani Afrika. chanzo chetu kinaendelea kueleza'


Utafiti wa Kituo cha Habari cha Marekani CNN, umebaini kwamba Tanzania ni nchi ya sita barani Afrika kwa watu wake kunywa pombe chafu (mataputapu).
Utafiti huo wa Machi 23 mwaka huu, ulibaini kwamba Uganda inaongoza kwa kunywa pombe chafu maarufu kama Luwombo kwa asilimia 14.52 ikifuatiwa na Rwanda kwa asilimia 6.44.
Kwa mujibu wa utafiti huo, Tanzania inashika nafasi ya tano kwa kuwa na asilimia 4.52, ikiwa nyuma ya Burundi yenye asilimia 5.07.
Ivory Coast imekuwa nyuma ya Tanzania kwa kuwa asilimia 3.55 huku Tanzania ikiipiku Burkina Faso iliyoambulia asilimia 3.77, kwa wa watu wake kunywa pombe chafu.
Ripoti ya utafiti huo ilisema asilimia kubwa katika nchi za Afrika, wanapenda kutumia pombe kali kwa lengo la kuondoa msongo wa mawazo.
Mtaalamu wa masuala ya afya katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Kitengo cha Figo, Dk Francis Fulia aliwataka wananchi waache kunywa pombe hizo kwa sababu zinatengenezwa katika mazingira ambayo si salama.
Alisema hali hiyo inahatarisha usalama wa afya zao.
“Watanzania waachane na matumizi ya pombe hizo kwa kuwa zinatengenezwa katika njia sizisokuwa salama, pia zinasababisha magonjwa mbalimbali kama figo, ini, moyo ,kupata upofu ama kupoteza maisha,” alisisitiza.
Dk Fulia pia alipinga juu matumizi ya pombe katika kuondoa msongo wa mawazo.
“Pombe haina uhusiano wowote katika kupunguza mawazo, inatumika katika kumsahaulisha mtu tatizo lake kwa kipindi kifupi” alisema.
Aliongeza kuwa njia salama ya kuepuka msongo wa mawazo ni kusuluhisha kwa kutafuta chanzo cha msongo huo au kupata ushauri nasaha kutoka katika vituo mbalimbali vya afya.
Katika miaka ya hivi karibuni, kumekuwa na matukio ya wananchi kujitumbukiza katika unywaji pombe uliokithiri ikiwamo kunywa pombe aina ya virobo gongo na pombe nyingine.
Kwa msaada wa mwananchi.co.tz

Upara,sababu ya maradhi ya moyo?



Wanaume wanaoanza kuwa na upara huenda wakakabiliwa zaidi na tisho la maradhi ya moyo kuliko wenzao waliojaa nywele vichwani.
Hii ni kwa mujibu wa watafiti nchini Japan.
Utafiti huu uliowahusisha watu 37,000, ulichapisha taarifa kwenye jarida la mtandao, 'BMJ Open' ukisema kuwa wanaume wanaokuwa na upara kwa asilimia 32 wanaweza kuwa na maradhi ya moyo.
Hata hivyo, watatifi walisisitiza kuwa athari hizi ni chache ikilinganishwa na zile za uvutaji sigara na unene kupita kiasi.
Shirika linalojikita katika maswala ya maradhi ya moyo nchini Uingereza, limesema kuwa wanaume wanapswa kujichunga wasinenepe kupita kiasi kuliko kuchunga nywele zao.
Kuanza kukuwa na kipara ni kawaida ya maisha kwa wanaume . Wengi kuanza kukuwa na upara wanapokuwa miaka 50 na asilimia 80 ya wanaume hao, hupoteza nywele wanapokuwa na umri wa miaka 70.
Watafiti katika chuo kikuu cha Tokyo, walidurusu utafiti wa miaka mingi iliyopita, kuchunguza uhusiano uliopo kati ya kuwa na upara na maradhi ya moyo.
Walionyesha kuwa nywele ambazo zilianza kutoweka, zina uhusiano na maradhi ya moyo. Hii ilikuwa baada ya kuzingatia maswala kama umri, na historia ya familia.
Daktari, Tomohide Yamada, wa chuo kikuu cha Tokyo alisema kuwa walipata uhusiano mkubwa kati ya upara na tisho la kupata maradhi ya moyo.
"tuliona hili kama jambo muhimu, lakini halina athari kubwa kama mambo mengine yanayosababisha maradhi ya moyo kama vile uvutaji sigara, unene kupita kiasi na mafuta mengi mwilini pamoja na shinikizo la damu.''
Alisema kuwa wanaume wenye umri mdogo wanaopata upara wanapaswa kuanza kuzingatia afya njema ili kujikinga kutokana na maradhi ya moyo
Aidha alisema hakuna ushahidi wa kutosha kupendekeza kuwa wanaume wenye upara wafanyiwe uchunguzi wa maradhi ya moyo.
Maradhi ya moyo ndio moja ya sababu kuu za vifo nchini Uingereza.
Mmoja kati yawanawake wanane kufariki kutokana na maradhi ya moyo.
Husababishwa na mishipa ya damu ambayo husukuma damu kwa moyo pale inapoziba.
Mmoja wa madaktari wakuu Uingereza amesema kuwa ingawa utafiti huu unaibua hisia, wanaume wenye upara hawapaswi kuwa na hofu.
BBC