m

"If you want to conquer fear, don't sit at home and think about it. Go out and get busy. "

-- Dale Carnegie, motivational expert

Saturday, 23 November 2013

MPASUKO CHADEMA, ZITTO AVULIWA UONGOZI,ARFI AJIUZULU UONGOZI




Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema kimemvua nyadhifa zote Naibu Katibu mkuu wake Zitto Kabwe ambae ni mbunge wa Kigoma Kaskazini.

Mwanasheria mkuu wa CHADEMA Tundu Lissu kwenye makao makuu ya chama hicho, amesema Zitto na wenzake watatu wamebainika kukihujumu chama  kwa kuanzisha kitu kinaitwa Mkakati 2013 kinacholenga kukisambaratisha chama hicho ili kuwaondoa madarakani Mwenyekiti na Katibu mkuu wake.

Nyadhifa alizovuliwa ni Unaibu katibu mkuu pamoja na Naibu kiongozi wa upinzani bungeni ambapo yeye, Dr. Kitila Mkumbo na Samson Mwigamba na mwingine mmoja Makao makuu wamepewa siku kumi na nne wajieleze kimaandishi kabla ya kuchukuliwa hatua zaidi za kinidhamu ikiwemo kuvuliwa Uanachama.

Wakati hayo yakiendelea naye Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho Bara na Mbunge wa Mpanda Said Amour Arfi ameamua kuandika waraka wa kujizulu wadhifa wake kama ifuatavyo;

Salaam,
Napenda kuwasilisha kwako taarifa ya kujiuzulu nafasi ya Makamu Mwenyekiti Bara kuanzia Leo Ijumaa 22 Novemba 2013 kwa kuchoshwa na Unafiki unaoendelea ndani ya Chama. Napenda ifahamike pia kwangu maslahi ya Wapiga kura, Wakaazi na wananchi wa Mpanda Mjini na Wilaya ya Mpanda ni muhimu katika kuwatumikia, hivyo basi sipo tayari kuchaguliwa marafiki.

Kwa kipindi kirefu zimekuwepo shutma dhidi yangu na kutiliwa mashaka mahusiano yangu na Mhe Pinda Waziri Mkuu pamoja na kulijadili katika vikao kadha Mpanda na Dar es Salaam bado yapo mashaka kwa nini alipita bila kupingwa hayo yalikua maamuzi ya Wanampanda kwenu imekua ni tatizo lakin hamsemi kwa nini Majimbo mengine 16 nchini yalipita bila kupingwa mlikua wapi na nani alaaumiwe huu ni Unafiki  wa kupindukia.
Aidha mmechukizwa sana kwa nini nilihoji kauli ya Muasisi wa Chama Mhe Mtei kutuchagulia viongozi naomba ifahamike wazi kwamba huu ni mtazamo wangu na utabakia hivyo siku zote kwa chama cha demokrasia kutoruhusu uongozi wa kiimla kwa kukidhi matakwa ya Waasisi ambao huvigeuza vyama kuwa Mali binafsi
Kwa kusema ukweli na kusimamia ukweli daima itabakia kuwa lengo langu katika maisha yangu siku zote hata kama itanigharimu maisha yangu
Nawasilisha.

Mgogoro wa Mapenzi waendelea kuleta Maafa: Nini Tatizo?

Mpedwa msomaji wa gazeti tandu la KII kumekuwepo mgogoro wa mahusiano ya kimapenzi umeendelea kuleta maafa hasa jijini Dar es Salaam. Tukiwa hatujasahau mauaji ya yaliyotokea kwenye familia ya mtangazaji Ufoo Saro tayari risasi zisikika Ilala Bungoni mojawapo ya viunga vya jiji la Dar es Salaam, risasi zilipigwa na Mpenzi wa Christina Newa na kusababisha vifo vya watu wawili. Sitaki kujadili zaidi juu ya hii miwili kwani ni alama tu ya migogoro mingi iliyopo nchini.
JE NI WIVU, UNAFIKI, UONGO KATIKA MAPENZI AU LIPO LINGINE?
HII NI MIGOGORO KABLA YA NDOA VIPI NDANI YA NDOA KUPO SALAMA?
Njoo tujadili hapa tupate suluhisho.
Hapa chini ni mojawapo ya picha za mauaji hayo zilizotawala kwenye vyombo vya habari

mtangazaji wa kituo cha ITV Ufoo saro akipelekwa katika wodr 12 katika jengo la kibasila leo jioni baada ya kufanyiwa upasuaji masaa kutokana na majeraha ya kupigwa risasikadhaa na mzazi mwenzake anaejulikana ANTHER MUSHI Anaefanyakazi Dafuu nchini sudani