
Kwa niaba ya KII na kwa niaba yangu mimi mwenyewe nimepokea taarifa za
kifo cha Prof. Gabriel Mwaluko kwa majonzi makubwa. Prof Mwaluko
mwanataaluma nguli katika fani ya udaktari na ambaye aliku
wa
mkuu wa chuo kikuu cha mt. Yohana (St. John's) amefariki dunia akiwa
nchini India alikokuwa akipatiwa matibabu ya Saratani ya koo katika
Hospital ya Appolo. Prof Mwaluko ambaye wakati wote alijawa na tabasamu
na asiye na makuu ndani ya miaka miwili ya uwepo wake SJUT alikuwa na
jitihada kubwa ya ya kukiendeleza chuo. Katiba hotuba ya alipotutembelea
Kituo cha Mt. marko Dar Es Salaam aliahidi kukifanya kuwa cho kikuu
kishiriki jambo ambalo ingekuwa hatua kubwa ya maendeleo ya chuo, Kwa
kuanzia akakubali mahafali ya St. marks kwa mara ya kwanza kufanyika Dar
es Salaam.
Binafsi nitamkumbuka sana lakini chuo cha Mt. Yohana
kinapaswa kumbkumbuka kwa vitendo kwa kuondoa urasimu katika utendaji
na pili kufanikisha kukifanya kituo cha Dar es Salaam kuwa Chuo Kikuu
Kishiriki ili kukipa nguvu zaidi jambo ambalo Prof Mwaluko alitamani
litokee kabla mwaka huu haujaisha.
Bwana alitoa na Bwana Ametwaa... Jina la Bwana lihimidiwe.