 |
Mdada akila majani ambayo huduma hiyo wanasema ni chakula kutoka mbinguni mwe! |
Kuna mengi ambayo yamekuwa yakizungumzwa kuhusu huduma za watumishi
mbalimbali, moja wapo ni hii huduma iitwayo Rabboni Centre ministries
iliyopo Pretoria nchini Afrika ya kusini, huduma hii iliyochini ya
mwanzilishi wake mwalimu ,mchungaji na nabii Daniel Lesego ilianza mwaka
2002. Ni huduma ambayo kwa watu wasioabudu hapo huitilia mashaka
kutokana na mwenendo wake.
Kwasasa wapo kwenye mfungo ambao watu hufika kanisani na hatimaye
wanaishia kula majani yaliyopo nje ya kanisa hilo akisema kwamba Roho
Mtakatifu huongoza mtu kula chochote huku ikidaiwa kuwa manyasi hayo ni
chakula kutoka mbinguni.
Inaelezwa kwamba mara baada ya maombi waumini wengi huanza kutapika
jambo ambalo kanisani hapo huashiria kwamba mtu amejazwa Roho Mtakatifu.
Lakini kama haitoshi nabii Lesego hufanya maombi huku amewakanyaga watu.
Huduma hii imekuwa gumzo nchini humo na nchi jirani kwa jinsi mambo yao
yanavyokwenda.
Mnasemaje watumishi kuhusu jambo hili? mwe kula manyasi kweli? mma!
 |
Hapa nabii huyo akikanyaga watu kama njia ya mafundisho yake. |
 |
Haa!! angalia jamani, sasa ng'ombe watakula nini jamani??? |
 |
Mungu tufunulie macho ya rohoni kuyajua mambo haya kama ni wewe au sisi kha! |
 |
Hajamaliza bado. |
 |
Baada ya manyasi ni mwendo wa kutapika sasa
|
 |
Picha ya juu na hii huyu ndio nabii Lesego Daniel mwenye maono na huduma hii. |
 |
Watu wanajaa kwenye huduma. |
 |
Mwe! kama uti wa mgongo shida hii dawa |
 |
Maombi yanaendelea. |
 |
Waumini wakikaribisha mwaka mpya. |
 |
Nabii anafundisha huku skuna yake imekanyaga mtu, sijui |
Tembelea
TOVUTI YAO Picha zote kwa hisani ya ukurasa wao wa Facebook.
Chanzo : gospelkitaa.blogspot.com