m
"If you want to conquer fear, don't sit at home and think about it. Go out and get busy. "
-- Dale Carnegie, motivational expert
Friday, 12 April 2013
MAAJABU, MAKANISA NDANI YA MAPANGO
Mapango yana mchango mkubwa katika historia ya Uyahudi na Ukristo kwa
ujumla. Daudi alijificha kwenye pango wakati akimtoroka mfalme Sauli,
nyaraka muhimu za 'bahari ya shamu'pia zilipatikana kwenye pango, na
wakristo pia wamekuwa wakikutana kwenye mapango kwa ajili ya kuabudu.
Huko Bulgaria, katika mji wa Mihalich - kuna pango ambalo kanisa
lilikuwa likikutana. Wanahistoria na wataalamu wa mambo ya kale
wanaamini kuwa kanisa hilo la pango limetumika mnamo karne ya 10.
Flickr/Klearchos Kapoutsis - Creative Commons |
Kwa mujibu wa tovuti ya a view on cities,
Kanisa la pango la Mtakatifu Stefano mjini Budapest, Romania,
lilifungwa na wakomunisti mwaka 1951, na kisha kufunguliwa tena mwaka
1989. Kanisa hilo lilikamilishwa ujenzi wake mwaka 1931.
© Flickr/Robot B - Creative Commons |
Pengine kanisa la pango ambalo linafahamika sana duniani ni lile la
Misri, ambapo wa'Zabbaleen', watu wanaokusanya taka jijini Cairo
wanaabudu.
Kwa mujibu wa mtandao wa wikipedia,
kuna makanisa ya pango saba yaliyojificha kwenye mapango ya mlima
Mokattam. Kanisa la Mtakatifu Simon the Tanner ndilo kanisa kubwa
mashariki ya kati, likiwa na uwezo wa kuchukua watu waliokaa 20,000.
© Flickr/Roaring Jellyfish - Creative Commons |
Kanisa hilo limechuka jina la Mtakatifu Simon the Tanner ili kumuenzi, mkristo wa dini ya Coptic kutoka karne ya kumi.
Urithi ambao umeachwa na makanisa ya handaki ni mkubwa na wa kipekee.
Mtume Paulo anaandika kwenye waraka wa Waebrania sura ya 11 kuhusu waamini waaminifu ambao wameonesha imani ya kipekee.
"(Watu ambao ulimwengu haukustahili kuwa nao), walikuwa
wakizunguka-zunguka katika nyika na katika milima na katika mapango na
katika mashimo ya nchi" Waebrania 11:38
Mpaka hivi sasa, kuna wakristo ambao huabudu kwenye makanisa yaliyo kwenye mapango.
Subscribe to:
Posts (Atom)