Hapa ni mojawapo ya mabango ya shughuli zinazofanyika kwenye ofisi ya KII ambao pia ndo wachapishaji na wamiliki wa blog hii.
Huu ni mwonekano unapingia tu ofisini
Vitendea kazi vya KII vinavyoonekana, hapa ni baada ya ngamizi mama "main computer" ya Hitachi All in 1 kuwa katika maboresha Safari Computers.
Java hayuko nyuma katika kusoma habari mbalimbali za mitandao zifaazo kwa ajili kuchambuliwa, kuhaririwa na hatimaye kuchapishwa.
Huduma za kifedha pia zinapatikana kwani hapo ukutani ni namba ya wakala wa Mpesa, unaweza kulipia kwa Mpesa katika huduma zetu
Melody, ambaye yupo katika mafunzo ya dharura kwa ajil uandishi wa habari KII
Bw. Kapagi afisa mtendaji mkuu-KII na Mhariri mwandamizi wa Blogu ya kapagiii.blogspot.com na pia sasa ni mhariri na msanifu wa blogu ya Mazingira Natural Products (mazingiranp.blogspot.com)
Java halali ofisini, hapa anatafakari mwenendo wa kazi
KII huwezi kukosa habari, hapa ni baadhi tu ya nyaraka zinazopatikana Computer Dictionary, Katiba ya nchi, Biblia na vitabu kadha wa kadha na chini ni magazeti ya kila siku kwa ajili ya kujisomea na kupata habari mbalimbali
"Chukua kazi yako na karibu tena" ni maneno ya mkurugenzi akitoa huduma.
Juvenile naye hayuko mbali kukamilisha timu ya utendaji ya KII, yupo kazini katika uchapaji.
Mkurugenzi wakati wote ni shughuli tu, usiku ndo kwanza ni kama asubuhi.
Ujirani mwenza, maarufu kama kwa mama peter, kioski na genge kila kitu unapata hapo. Na ndo biashara iliyomsomesha Peter Kapagi na wenzake.
Leo nimekuletea baadhi tu ya hekaheka za ofisini kwa KII, njoo ujionee mwenyewe utendaji mahiri kabisa wa KII. Kamwe hutojuta na hutorudi kama ulivyo.
Kwetu habari ni Maisha