m

"If you want to conquer fear, don't sit at home and think about it. Go out and get busy. "

-- Dale Carnegie, motivational expert

Sunday, 27 October 2013

Ofisi ya KII yafunguliwa rasmi

Tumeanza!!!
Ninayo furaha kubwa kwamba Ofisi yetu kuu ya Kapagi Information Institute -KII imefunguliwa rasmi hapo jana Jumamosi ya tar 25oct, 2013. Kila kitu kimeenda sawa kama nilivyokuwa nikitaarifu awali. Kwa niaba ya KII na mimi mwenyewe ninazo shukrani za pekee kwa Bwana Yesu Kristo na kwa wote walioshiriki kuniunga mkono na kuniamini hata kunichochea sana niweze kufungu ofisi japo wengi walipenda iwe Dar es Salaam.
Natamani kuwaorodhesha wote waliniunga mkono kwa hali, mawazo na mali hakika si wachache ni wengi lkn kwa neema nitaorodhesha japo wachache kwa niaba ya wengi.
Acha niwaorodheshe ijulikane kwamba wapo walio nyuma yangu na taasisi, wapo wanaoitakia mema, kuimbea, kushauri hata kuwa radhi kufadhili
Nianze kwa familia, dada John Janet Merinyo, Mauki, Furaha Samwel na Mr Chipanda, Sunny, Xaveria, Neema Michael, Abel Mwakyandwike, Uncle Mwasomola, Oswin Joctan, Rehema Chillery, Sia na Neem Stationery, Shangarai, Papalika, Mary Simon, Uncle Dickson (Computer Doctor), Teddy na Yamsebo Stationary, Bineth Printing bila Kumsahau Mama G wa ukweli (rehema Sanga) na Gladiness Stationery, Sae internet Cafe kwa Software, Mzee Chale na Marge (St. Marks Library), Janus Bernard,
Aaah, ni wengi na hili linanipa nguvu kwamba nimeanza na kuna watu wapo nyuma kwa ajili ya Taasisi hii Muhimu. Nisamehe ikiwa sikukuorodhesha na hiyo siyo maana kwamba sijaheshimu mchango wako. Una maana kwangu na kwa KII, na ikiwa una maana kwangu una kubwa kwa jamii nitakayoihudumia.
Niwe na tamko moja tu sasa kwamba nimeanza na sitorudi nyumba, nitaficha wapi sura yangu kwa kundi hili kubwa linaloniunga mkono usiku na mchana.
Niwe na Ahadi moja kwamba nilipofundisha ujasiriamali mara zote nimezungumzia kuwa "kwa wafanyakazi wenye mshahara wa msingi ujasiriamali ni njia ya kujipatia kipato cha ziada" LAKINI MIMI NITAENDA MBALI NATAKA KUFANYA UJASIRIAMALI KUWA JIPATO CHA MSINGI na mshahara kiduchu wa serikali na mashirika dhalimu kuwa kipato cha ziada. hili halitafanyika kwa njia nyingione isipokuwa kutumia kila furasa kuwahudumia watu na kuondoa matatizo ya msingi kwa jamii na taaluma.
Kwa kuwa ndo kama naanza nisiwe na mengi, Wakati ujao nitakuja na makala yenye Dira, Malengo na Wito wa Kapagi Information Institute-KII.
Tumeanza tukiwa dhaifu, tujipange kufanya Makubwa. Tanzania yenye huzuni inatusubiri ifanye sherehe ya kuzaliwa kwetu kama wakombozi.