Mkutano wa injili maarufu kama Outreach wa CASFETA-ST. JOHN'S ambao umeanza tangu jumatano unaendelea kwa shangwe kuu Viwanja vya Bigwa, Lukuyu miembe miwili na hadi sasa watu 54 wakwishampokea Yesu Kristo wa Nazareth awe Bwana na Mwokozi wa Maisha yao.
Hebu tuangalie picha na matukio tangu kuwasili Mjini morogoro.
Mwimbaji maarufu wa nyimbo za Injili Shayo Felix akiimba kwa hisia kali kwenye viwanja vya Bigwa, Morogoro
Mchungaji mwenyeji wa Kanisa la Elim Pentekoste Mwanzo Mgumu akifuatilia mkutano.

Mhubiri Andrew Wikesi akihubiri full dose siku ya kwanza Jumatano ya tar 07.08.2013
Siku ya pili ya mkutano viti havikukalika, mambo yamekaza na hapa Mwimbaji Felix Shayo anamsifu mungu kwa shwangwe kuu.
Mkutano ni mzuri kweli kweli ambapo pia umeambatana na semina ya ujasiriamali ambayo imekuwa ikiendeshwa na Mwl Peter Kapagi. Watu wote wanakaribishwa sana katika mkutano wapate haki, amani na furaha yao maana ufalme wa Mungu unashuka kwa kila autakaye.
Warumi 14:17