Kumekuwa
na mvutano usio na tija katika bunge letu juu ya kura ipi ipigwe kupitisha
ibara za rasimu ya katiba. Nimefuatilia mvutano huo tangu ulipoanza ambapo kura
ya wazi inaungwa mkono kwa kiasi kikubwa na wabunge wa vyama vya upinzani na kura ya siri inapigiwa chapuo
na chama tawala.
Ukweli
ni kuwa wapinzani wanataka kura siri
wakidhani kila mtu atakuwa huru kupigia analotaka. Ni hisia kuwa kuna
demokrasia kubwa katika kura ya siri. Wapinzani wanaamini kuwa kura ya siri
itawafanya wale wajumbe wasio na msimamo watashindwa kufuata mkumbo na kwa
namna hiyo watapata katiba iliyotoka katika mioyo ya watu.
Ni
hisia nzuri japo si uhalisia.
Ukweli
wa pili ni kuwa CCM na wanaounga kura ya wazi wana sababu ya kwanza ni maslahi
ya chama wanaamini kuwa kura ya wazi itasaidia kuwasomba kirahisi wajumbe wasio
na msimamo na kwa namna hiyo itakuwa rahisi kupitisha maazimio yenye mlengo wa
kwao. Pili ni ile hoja wanayoisimamia kwamba kwa kuwa KUUNDA KATIBA MPYA NI
JAMBO ZITO LITAKALOCHUKUA MIAKA 50 ZAIDI BASI NI MUHIMU KILA MTANZANIA AKAJUA
MJUMBE WAKE AMEAMUA NINI JUU YA KATIBA… ikiwa amewasilisha alilomtuma au la.
Ukweli
wa tatu ni Siasa za nchi yetu, siasa kwa sasa imegubikwa na UONGO, UNAFIKI NA
UBINAFSI kwa lugha moja mwenyewe huita UZANDIKI. Ni siasa ambazo mtu hutamka
asilolitenda mwonekano wake ni tofauti na alivyo, ni vigeugeu, analolisema leo
kesho analipinga ili tu maslahi yake yalindwe. Kwa mfano yupo mwanasiasa mmoja
aliwahi nukuliwa akisema anahama CCM na kuja kurudi CCM ni sawa na kulala na
mama yake… ajabu kweli kujitusi yeye na mamaye kwa ajili ya maslahi yake
binafsi ya kisiasa ili wanaCUF wampokee vizuri lakini hatimaye alihama tena CUF
na kurudi CCM… sina hakika anamtazamaje mamaye.
Binafsi
ningependa kura ya siri ili wenye kuwaridhisha wanaotaka demokrasia lakini kwa
unafiki wa wanasiasa wengi NAUNGA MKONO KURA YA WAZI naunga mkono kwa sababu
1.
Nataka
kubaini wajumbe wangu watasema nini bungeni kwa sababu pamoja na utashi wao lkn
tumewatuma kutuwakilisha, ni mashaka kuwa wapo watakaopitisha mambo yao binafsi
ambayo hatukuwatuma. Kwa sababu watakuwa huru, hur kufanya lolote hata lililo
kinyume.
2.
Kura ya siri
si kwamba itawasaidia wabunge wasio na msimamo bali inaweza kuwasaidia KUTOPIGA
KABISA wakati kwenye uwazi wataona aibu kutopiga kabisa.
3.
Nchi yetu
haitakuwa mwasisi wa kura ya wazi UN wenyewe ambao ndio baba wakusimamia
demokrasia mambo yao mengi hata ya baraza la usalama hupigwa hupitishwa kwa
kura ya wazi. Mfano ni maazimio tata juu ya mashariki ya kati ambapo wakati
mwingine Marekani amejikuta akiwa na kura yap eke yake kupinga maazimio fulani
juu ya mshirika wake Israeli.
4.
Suala la
katiba ni alama muhimu ya ushujaa, kuunda katika wakati wa amani ningependa
mashujaa wajulikane, misimamo yao iwe wazi na dunia nzima ijue. Isiwe misimamo
yam domo majukwaani watuambia wanaunga mkono muundo wa serikali tatu huku
mioyoni wao wamejaza serikali moja.
5.
Kwa tafsiri
yangu ushujaa ni kushinda magumu ambapo moja wapo ni kuwa tayari kwenda kinyume
na maazimio ya chama chako kwa uwazi ili kuthibitisha utashi wke na kwamba
hashurutishwi katika maamuzi.
6.
Kwamba
naunga mkono kura ya wazi kama adhabu kwa wanafiki waliozoea kuzungumza
wasilotenda na kutenda wasilozungumza umma wote ujuye atalopitisha katika
katiba itakayodumu miaka 50 ijayo au zaidi.
7. Kama kura zitakavyotumika katika maamuzi basi hata kuamua suala la kura ipi itumike lingekuwa la utashi wa mtu na si chama chake. Hofu yangu ni kuwa suala hili linaendeshwa kishabiki tu na si kwa dhamira za dhati za ndani ya wajumbe. Kila mtu ajifunze na ajenge hoja kwanini anataka kura ya aina fulani. Mimi nimechambua na kubaini tamu ya kura ya wazi na chungu ya kura ya siri.
7. Kama kura zitakavyotumika katika maamuzi basi hata kuamua suala la kura ipi itumike lingekuwa la utashi wa mtu na si chama chake. Hofu yangu ni kuwa suala hili linaendeshwa kishabiki tu na si kwa dhamira za dhati za ndani ya wajumbe. Kila mtu ajifunze na ajenge hoja kwanini anataka kura ya aina fulani. Mimi nimechambua na kubaini tamu ya kura ya wazi na chungu ya kura ya siri.
Ukweli ni ukweli tu uwe mtamu au mchungu…na
ukwli utakaokana leo kesho utaulilia ukiwa umekwishakuumbua
Wenu
katika Ukweli
Mwl
Peter Kapagi
Barua
pepe: kakakapagi@gmail.com
Simu:
0685306666