==========
Natamani mjadala uanze wa tozo la simu, kufungiwa kwa mwananchi na Mtanzania isiwe hoja ya kuzuia mjadala wa tozo la simu maana Naona magazeti yote yamegeukia mzozo wa kufungiwa Mwananchi na Mtanzania.
Nchi hii inachosha kwani wawekezaji wakubwa wa madini tunawaachia kodi wanatupa mrabaha wa 3% wakati madini ni ya kwetu wakati huo huo wanataka kumchangisha mwananchi 1000 kila mwezi kwa ajili ya simu ambayo mawasiliano yake ya mchango mkubwa kwa maendeleo ya Taifa. Nchi hii inaacha pesa nyingi za madili zinaliwa na mabeberu wajiitao wawekezaji huku ikitaka kuwakandamizi wananchi katika ardi yao wenyewe..inashangaza sana, inatia uchungu. Ona nchi za uarabuni zina vita kila siku lakini bado zina jeuri ya uchumi imara kwa sababu moja tu kuwa na utajiri wa Mafuta. ni kweli bado hatuchimbi mafuta lakini ni nani asiyejua madini ghali duniani kuwa ni Dhahabu, Almasi na Tanzanite? Je si ndo yametapaka Shinyanga, Geita, Mara, Arusha ukiachana na mikoa inayozalisha kidogo kama Chunya-Mbeya n.k? je madini hayo hayatoshi kujenga barabara, huduma za afya, maji na shule?
Tunapaswa kujifunza namna ya kuwanyonya wawekezaji na si kuwanyonya watanzania katika ardhi yao...hiyo haitakuwa demkrasia tena, itakuwa udikteta na unyonyaji mbaya zaidi kuliko ukoloni.
==========================
Kwa kweli tozo hilo halikubaliki kama vile Kodi za Kikoloni za Kichwa, Matiti tax na Kipande system.
Ikipitishwa kabisa tozo la simu basi ni Bora Tumrudishe Richard Turnbull, gavana Mwingereza aje atutawale hata akituchaapa tutamwelewa kwa kuwa ni Mzungu.