Siasa za Tanzania zinaharibu maendeleo ya nchi, kelele nyingi huwapoteza watu kufikiri namna ya kendelea.
Watanzania wamewekeza muda wao katika siasa uchwara za nchi hii, wanalo tumaini kuwa siku moja wanasiasa watawakomboa... wengine wamesubri muda mrefu na sasa wamekata tamaa kwa kuwa chama fulani hakijawafikisha mahali wanapotaka.
Ndugu zangu utafiti wangu usio rasmi unaonyesha kuwa nchi nyingi zimefanikiwa baada ya watu wake kujitambua, kutambua hali zao na ktafuta suluhisho, na suluhisho kubwa ni kila mmoja kuimarisha uchumi wake kwanza na hasa kwa njia ya ujasiriamali. ukiitazama China ya leo ni tofauti na China ya miaka ya 60 tofauti kubwa ni kuwa wakati ule watu wake walijishughulisha na viwanda vidogo na huduma ndogondogo baadaye wakaunda viwanda vikubwa na hatimaye wanahudumia dunia.
Kama kila mtu akitafuta shughuli ya uzalishaji mali yoyote, akatumia ubinifu na ugunduzi ili kuboresha shughuli yake basi bila shaka yoyote tutaweza kuwa na uzalishaji mkubwa wa bidhaa ndogondogo ambazo zitapunguza ama kuondoa kabisa uagizaji wa bidhaa za nje na hapo tutakuwa tumetengeza ajira na kupunguza mfumuko wa bei.
WATANZANIA TUFANYE MAMBO MAWILI SAMBAMBA TUWE NA SHUGHULI ZA UZALISHAJI MALI WAKATI HUO HUO TUKIPAMBANA NA SIASA YAANI KUWALAZIMISHA WANASIASA WATENGENEZE SERA NZURI ZA KIUCHUMI ZITAKAWASAIDIA WATU KUENDESHA SHUGHULI ZAO NA KUWAPATIA MASOKO... Napinga kabisa watu wazima kwa vijana kukaa vijiweni wakicheza bao huku wakilaumu siasa za nchi hii eti haziwatoi.
Winston Churchill aliwahi sema huweza kufikia maono yako ikiwa utahangaika kuwatupia mawe mbwa wengi wanakubwekea...
==============================
TUKUTANE TENA KWENYE UKURASA HUU KIPINDI KIJACHO TUANGALIE JUU YA MFUMUKO WA BEI...