Suala la ununuzi wa mashine za TRA za kieletroni za risiti kwabei ya sh. 800,000/= limezua Tafrani kubwa jijini Mbeya. tfrani hiyo imesababishwa na bei ya mashine hiyo ambayo inauzwa kuanzia sh.800,000/- kiasi ambacho wafanyabioashara wanapinga kwa kigezo kuwa bei hiyo ni zaidi ya mtaji wa biashara. katika mahojiano baadhi ya wafanyabiasha eneo la Mwanjelwa na Sae wamezungumzia bei ya mashine hizo kuwa na uwizi mkubwa kwani wenyewe hawapinmgi matumizi yake isipokuwa wanahoji kwanini ziuzwe kwa gharama kubwa kiasi hicho.
Wengine wameenda mbali zaidi wakikosoa mchakato huo kwamba utawakwamisha wafanyabiashara wengi na kwamba kwa kuwa mashine hizo zitawafaidisha TRA kwa suala ulipaji kodi zingepaswa kutolea bure sawa na mita za maji na umeme kwani zitakuwa mali ya TRA. Baadhi ya watu wakahoji kwanini mashine hizo ndogo ziwe ghali kiasi hicho kuzidi gharama ya mashine kubwa za photocopy ambazo huuzwa kwa sh.600,000, Kompyuta na hata Printer ambazo gharama zake si zaidi ya 500,000/=
Kufuatia tamko hilo la TRA kuwataka wafanyabiashara wote wanaouza zaidi ya sh.45,000/= kwa siku kuhakikisha wananunua mashine hizo likasababisha mgomo wa wafanyabiasha wa Mwanjelwa ambao wakaandaa mkutano uliokua ufanyike Viwanja vya S/M Ruanda Nzovywe ambao hata hivyo ukazuia na polisi kwa ulipuaji wa mabomu ya machozi.
Hapa ni baadhi ya picha za matukio ya vurugu hizo;
Polisi
wakiwa wanasindikiza gari la matangazo kutangaza
kuomba Vurugu hizo na maandamano yasiyo na kibali yasitishwe
Polisi wakiwa wameimarisha ulinzi mkali
Wafanya biashara wakiwa viwanjwa vya Shule ya Msingi Ruanda Nzovwe kungoja kusikiliza nini hatma yao
Baadhi ya watu wakikimbia Mabomu ya machozi yalipoanza kurushwa ili kuepusha vurugu
Mawe yakiwa yamepangwa kuzuia magari yasiende kokote
Maduka yote yakiwa yamefungwa eneo la mwanjelwa kupinga ununuzi wa mashine hizo za TRA
Vijana hawa wakiwa wana nawa uso baada ya Bomu la machozi kuwapitia
Jiwe kubwa likiwa limewekwa katika Barabara magari yasipite
Matairi yakiwa yamewashwa barabarani kuanza vurugu kupinga mashine hizo