m

"If you want to conquer fear, don't sit at home and think about it. Go out and get busy. "

-- Dale Carnegie, motivational expert

Tuesday, 7 February 2012

Kikao cha Viongozi-SJUT DSM

Bwana asifiwe. 
Viongozi wote CASFETA chuo cha Sjut, tutakuwa na kikao kesho Saa 11:oo jioni ukumbi wa semina room- left wing. Kila kiongozi mhusika anaombwa kufika. Ni muhimu kwa ajili ya kumaliza Semister.


Mbarikiwe.








Mbeya CASFETA Ex-Members

Bwana asifiwe...
Hatimae kumefanyika kikao cha viongozi wa CASFETA waliowahi kuwa CASFETA mkoa  wa Mbeya. Mjadala ulikuwa juu ya kuanzisha ushirikiano kwa wanaCASFETA waliowahi kuwa Mbeya na sasa wanaishi au kusoma Dar. Mjadala ulikuwa safi na muhimu ikiwa ni pamoja na kuangalia namna tutakavyoweza kufanikisha kambi la Pasaka la Mbeya.

Nawakaribisha watu wote waliowahi kushiriki CASFETA mkoa wa Mbeya wanaoishi Dar kwenye kikao kitakachofanyika siku ya Jumamosi saa 10:00 jioni Landmark Hotel.

Kama unaona unahusika USIKOSE KABISA na mwalike na mwingine.
Mubarikiwe.






Mbeya Ex CASFETA


TANZANIA YOUTH MINISTRIES
TAYOMI











CHRIST’S AMBASSADORS STUDENT’S FELLOWSHIP OF TANZANIA
CASFETA
   
Mbeya CASFETA Ex-members

Kikao cha viongozi wastaafu wa CASFETA mkoa wa Mbeya
Tarehe:            Jumapili, 05.02.2012
Muda:              Saa 11:00-12:20 jioni
Mahali:            Chuo Kikuu cha Ardhi
Mwenyekiti wa Kikao:             1.Kasalile C.G             -0713968622, chriskasalile@yahoo.com 
Katibu:                                     2.Peter K Kapagi          -0764734620, kakakapagi@gmail.com
Washiriki wengine:                 3.Furaha Kabuje          -0719434317, furahakabuje@yahoo.com
                                                4. Peter Mwasunga      -0752222404, peterall27@yahoo.com
                                                5. Ndagile Denis          -0754940105, mpelndagile@yahoo.com
Utangulizi
Kikao kilifunguliwa na Bw. Kasalile C.G baada utambulisho kufanyika kama ilivyo hapo juu. Mratibu aliwasilisha ajenda kuu mbili (2) ambazo ni
1.                  suala la Kongamano la Pasaka la Mbeya (CEC)
2.                  Ujenzi wa ukumbi Mbeya na ununuzi wa uwanja wa ekari 10
3.                  Suala la ushiririkiano kwa wanaCASFETA waliokuwa mkoa wa Mbeya wanaoishi au kusoma Dar es Salaam.
Mjadala
  1. ajenda ya kambi la pasaka ilijadiliwa na namna kubwa ya kuliwezesha iliyokubaliwa ni kuwatafuta wanaCASFETA wengine waliopo Dar es Salaam ili tuweze kuchangia pesa. Njia za uchangiaji ni kuchangia mtu binfsi na pili ni kutumia njia ya barua rasmi zilizoandaliwa.
  2. pia ikiwezekana tunaweza kushiriki moja kwa moja (fully participation) katika kuhakikisha kambi linafanikiwa ikiwezekana tunaweza kwenda kambi la Mbeya wanaCASFETA wa Mbeya tuliopo Dar es Salaam.
  3. Tunatakiwa kuhakikisha Mbeya inafanikiwa kukua uwanja wa ekari 10, kwa sasa tayari zimenunuliwa ekari 2 na bado ekari 8.
4.   Tunatakiwa kuhakikisha CASFETA Mbeya inafanikiwa kujenga ukumbi wenye kuchukua watu elfu kumi (10000) ambao utawezesha yafuatayo
4.1       Kufanyika kwa kambi moja tu la CASFETA mkoa mzima wa Mbeya.
4.2       Kutumika kuiingizia kipato CASFETA mkoa wa mbeya na hivyo kuondoa utegemezi na tatizo la kifedha.
4.3       Baadaye kujengwa shule kuzunguka ukumbi.
5.   tunaweza kuanzisha ushirikiano wa watu wanaishi Dar es Salaam wawe wanafunzi au wafanyakazi ili kushirikiana katika matukio mbalimbali kama vile mahafali, harusu na mengineyo. Pia angalau tuwe tunakutana kama kunywa soda kama tulivyokutana kwenye kikao kama sehemu ya ushirikiano.
6.   Furaha Kabuje(rais mstaafu) akaona kwamba tunaweza kufanya mambo makubwa zaidi Easter Conference kama vile kufanya uwekezaji mkubwa au kubuni miradi mikubwa inayomilikiwa na ushirikiano huu utakaoanzishwa.
7.   kwa pamoja tunaweza kufanya mradi mkubwa hata kwa kuanzia tu kuwa na daladala(Hiace) ambayoitakuwa chini ya menegement fulani na kila mtu akwa anafaidika kutokana na mchango wake (Hisa) kwa mfano kama wakipatika watu 50 tukapeana jukumu la kuchangia S. 500,000/- kila mmoja tunaweza kupata 25,000,000/- ambazo tunaweza kuanzisha mradi.
Maazimio
  1. tuazimie kupena jukumu kwamba kila mtu akatafute watu angalau 10 kwa ajili ya kikao kijacho.
  2. tunaweza kuanzisha mtandao mkubwa na hata kuandaa “fund raise” na hata kuandaa website yetu itakayotukutanisha tukiwa sehemu mbalimbali duniani.
  3. Tukagawa barua za mchango kwa ajli ya Kambi la Pasaka Mbeya.
  4. Kufanya kikao kingine Jumamosi ya Tarehe 11.02,2012 eneo la Landmark Hotel saa 10:30- 12:00 jioni kikao kitakachoshirikisha watu tuliowaalika kufika.
Kikao kilimalizika na kufungwa na mwenyekiti wa kiko saa 12:25 jioni.