m

"If you want to conquer fear, don't sit at home and think about it. Go out and get busy. "

-- Dale Carnegie, motivational expert

Saturday, 1 June 2013

Zana za Hizbollah zapatikana Nigeria

  31 Mei, 2013 - Saa 08:30 GMT


Jeshi lilisema kuwa silaha hizo zilikuwa zimefichwa chini ya vumbi la mbao
Karakana ya silaha inayoaminika kumilikiwa na kundi la Hezbollah, nchini Lebanon imapatikana Kaskazini mwa Nigeria.
Kwa mujibu wa taarifa za jeshi na shirika la ujasusi la Nigeria raia watatu wa Lebanon wamekamatwa. Msemaji wa jeshi, Brigedia Gen Ilyasu Isa Abba, pia amethibitisha hilo.
Silaha hizo ikiwemo, risasi, zana za kukinga magari ya kivita dhidi ya mashambulizi na RPG, zilipatikana ktika karakana mjini Kano.
Maafisa wa usalama walisema kuwa silaha hizo zilinuiwa kutumiwa dhidi ya maslahi ya Israel na nchi za Magharibi.
Hii ni kazi ya Hezbollah," katibu mkuu wa usalama mjini Kano Bassey Ettang alisema.Na unaweza hata kuwa na uhakika kuwa ikiwa hili linafanyika, inawezekana wanasaidia makundi ya kigaidi wanaoendesha harakati zao nchini humu,'' alidokeza bwana Bassey.
Brig Gen Ilyasu Isa Abba alisema kuwa zana 11 za magari ya kivita, guruneti na makombora 21 bunduki 17 aina ya Ak-47 na maguruneti 76 ni baadhi ya silaha zilizopatikana.
Mmiliki wa karakana hiyo, ambako silaha zilipatikana, zikiwa zimefichwa chini ya vumbi la mbao, hakuwa nchini humo.
Kuna jamii kubwa ya walebanese wanaofanya kazi mjini Kano, mji wa kibiashara wa Nigeria Kaskazini.
Mji wa Kano eneo la Kaskazini Mashariki mwa Nigeria zimekubwa na mashambulizi ya mara kwa mara katika miaka mitatu iliyopita, tangu wapiganaji wa kiisilamu Boko Haram walipoanzisha harakati zao.
Bwana Ettang aliongeza kuwa "unaweza pia kuwa na uhakika kundi kama hili likiwa lipo, inaweza hata kuwasaidia wapiganaji wengine walioko nchini humo.''
Hezbollah ni kundi la Kishia pamoja na kuwa vuguvugu la kisiasa lenye makao yake nchini Lebanon. Linatambulika na Marekani kama kundi la kigaidi.
Boko Haram, ambalo jina lake lina maanisha tamaduni za kimagharibi zinapingwa, linasema, nia yake ni kuipindua serikali sasa na kubuni serikali ya kiisilamu.
Kuna wasiwasi mkubwa kuwa kundi la Boko Haram huenda linasaidiwa na mtandao wa kigaidi wa al-Qaeda katika nchi zengine
bbcswahili.com

Japani kuipa Afrika msaada wa dola bilioni 32




Waziri Mkuu wa Japani Shinzo Abe Jumamosi (01.06.2013) ameahidi kutowa msaada wa dola bilioni 32 kwa Afrika katika kipindi cha miaka mitano kusaidia ukuaji wa uchumi wa bara hilo kupitia sekta za serikali na binafsi.
Waziri Mkuu wa Japani Shinzo Abe ametoa ahadi ya masaada huo wakati wa ufunguzi wa mkutano wa kimataifa wa siku tatu kuhusu maendeleo ya Afrika unaofanyika katika mji wa Yokohama nchini Japani.
Msaada huo unajumuisha utowaji wa yeni bilioni 650 kwa ajili ya mikopo katika ujenzi wa miundo mbinu na mpango wa mafunzo kwa ajili ya vijana wa Afrika.Mpango huo utawapa fursa vijana 1,000 wa Kiafrika kujifunza katika vyuo vikuu vya Japani na kujifunza kazi katika makampuni ya Kijapani.
Abe amesema kuendeleza rasilmali ya nguvu kazi, huduma muhimu za matibabu na kukuza sekta ya kilimo ni mambo muhimu katika kuchochea ukuaji wa uchumi wa Afrika.Amesema kile inachokihitaji Afrika ni uwekezaji katika sekta ya binafsi ambapo ushirikiano kati ya sekta za umma na binafsi utatoa fursa ya kufaidikia na uwekezaji huo. #
Shauku ya Japani kuwekeza Afrika
Waziri Mkuu wa Japani Shinzo Abe wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Kimataifa wa Maendeleo ya Afrika (TICAD) mjini Yokohama Japani. Waziri Mkuu wa Japani Shinzo Abe wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Kimataifa wa Maendeleo ya Afrika (TICAD) mjini Yokohama Japani.
Tangazo lake hilo linaonyesha shauku ya Japani kuchuana na China katika masuala ya kuipatia msaada na kuwekeza Afrika bara lenye utajiri wa mali asili.
Licha ya uhusiano wa muda mrefu uliopo kati ya Japani na Afrika,umuhimu wa Japani kwa bara hilo umekuwa ukipunguwa kulinganishwa na ule wa China ambapo kiwango chake cha biashara na Afrika ikilinganishwa na Japani ni mara tano zaidi na mara nane zaidi katika uwekezaji wa moja kwa moja.
China huwa haitangazi kiwango cha msaada wake wa maendeleo lakini repoti zinadokeza kwamba hutoa hadi dola bilioni mbili kila mwaka.Kiwango ilichotangaza Japani Jumamosi kimepita sana kiwango hicho cha China.Uhusiano wa Japani kwa Afrika unatofautiana na mataifa mengine kwa bara hilo amesema Abe katika kauli inayoonekana kuikusudia China.
Serikali ya China imekuwa ikishutumiwa na baadhi ya nchi kwa kile mara nyengine kinachoonekana kuwa inachofanya barani humo ni kunyakua ardhi na kutohusisha uwekezaji na masharti ya kuboresha haki za binaadamu au kuzitaka nchi zinazopokea misaada kuwa wazi zaidi.
Waziri Mkuu huyo wa Japani amesema mali asili ya Afrika inasababisha kuwepo kwa fursa muhimu za biashara kwa nchi yenye uhaba mkubwa wa mali ghafi kama Japani lakini nchi hiyo haitotafuta na kuchimba rasilmali hizo kwa sababu tu ya kuzileta Japani.
Msaada ukuze uchumi
Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Desalegn na Waziri Mkuu wa Japani Shinzo Abe wakati wa ufunguzi wa mkutano wa TICAD mjini Yokohama Japani. Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Desalegn na Waziri Mkuu wa Japani Shinzo Abe wakati wa ufunguzi wa mkutano wa TICAD mjini Yokohama Japani.
Amesema wataisaidia Afrika ili kwamba mali asili za Afrika zisababishe ukuaji wa kiuchumi wa bara hilo.Abe pia ametoa wito wa kuanzishwa kwa kanuni za uwazi katika biashara na kuimarisha usalama kwa Wajapani wanaoishi na kufanya kazi barani Afrika.Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Desalegn ameitaka Japani kuimarisha uwepo wake barani Afrika.
Akizungumza katika kikao cha ufunguzi wa mkutano huo wa Kimataita wa Tokyo kuhusu Maendeleo ya Afrika (TICAD), amesema ni jambo la kushangaza kwamba kuhusika kwa Japani katika fani ya uwekezaji barani humo kuko nyuma kabisa kuliko vile ingelipaswa iwe kwa hivi sasa kulinganisha na nchi mpya ambazo hivi sasa zimekuwa zikijihusisha katika harakati nyingi.
Afrika lazima ibadilike
Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini. Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini.
Suala la uwekezaji katika sekta ya binafsi limekaribishwa na wajumbe ambapo Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini amesema uchumi wa bara hilo hauna budi kuendelezwa. Amesema Afrika lazima ibadilike kutoka kuwa na uchumi unaotegemea usafirishaji nje wa bidhaa na kuwa na uchumi wenye kuongozwa na viwanda pamoja na kutanuwa njia mbali mbali za kiuchumi.Zuma amesema mambo matatu ni muhimu kufikia maendeleo nayo ni : kuunganisha masoko, kuendeleza viwanda na kuendeleza miundo mbinu.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon pia amehudhuria mkutano huo ambapo amesema malengo ya mkutano huo ni malengo ya Umoja wa Mataifa.Amesema wamejizatiti kuisaidia Afrika itimize Malengo ya Maendeleo ya Milenia yakiwemo kutokomeza umaskini na njaa ifikapo mwaka 2015.
Mkutano huo wa TICAD utaendelea kufanyika hadi Jumatatu ambapo wajumbe kutoka zaidi ya nchi 50 za Afrika watakuwa wanajadili na Japani jinsi ya kuhakikisha ukuaji wa uchumi endelevu barani Afrika.Mkutano huo unaandaliwa kwa ushirikiano wa mashirika ya kimataifa kama vile Umoja wa Mataifa,Benki ya Dunia na kwa mara ya kwanza Umoja wa Afrika.Mkutano huo umekuwa ukifanyika kila baada ya miaka mitano nchini Japani tokea ulipoanzishwa hapo mwaka 1993.
Mwandishi : Mohamed Dahman/AFP,dpa
Mhariri :Caro Robdw
dw.de

Ziara ya Obama nchini yazua malumbano

ZIARA ya Rais Barrack Obama wa Marekani imewagawa Watanzania huku wengi wao wakionyesha hofu kubwa ya viongozi wa mataifa makubwa kuwa wanakuja kwa nia ya kupora rasilimali za nchi. Wakati Watanzania wakiwa na hofu, Wakenya wamelalamika kupitia mitandao ya jamii kitendo cha Rais Obama kuwatenga wakati chimbuko la baba yake ni kutoka Kenya.
Wakizungumza na MTANZANIA kwa nyakati tofauti jana baadhi ya wananchi walisema wanashangazwa na ziara ya Rais Obama ikiwa ni miezi michache baada ya ziara ya Rais Xi Jimping wa China ambaye alitia saini mikataba 17 ya maendeleo.

Naibu Katibu Mkuu Bara wa Chama cha Wananchi (CUF), Julius Mtatiro alisema kitendo cha nchi kupokea wageni wakubwa wa mataifa makubwa ni heshima kwa nchi lakini inategemea kiongozi huo amebeba ajenda gani.

Naye Katibu Mkuu wa Baraza la Vijana wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (BAVICHA), Deogratus Munishi alisema Tanzania ni uwanja wa mapambano kwa mataifa makubwa kutokana na rasilimali zake.

Munishi alisema uchumi wa mataifa makubwa unategemea soko na rasilimali za mataifa madogo na akisisitiza kwamba madini ya uranium ndiyo chanzo cha viongozi wakubwa kukimbilia Tanzania.

Katika ziara yake ya kwanza katika Afrika, Rais Obama aliitembelea Ghana.

MATOKEO YA KIDATO CHA SITA YAPAA

Baraza la mitihani limetangaza matokeo ya kidato cha sita mwaka 2013. Matokeo hayo ni mazuri kulinganisha na matokeo ya kidato cha nne yalileta mtikisiko mkubwa. Kwa mujibu wa baraza la mitihani

Asilimia 93 ya waliofanya mtihani huo wa kidato cha 6 wamefaulu.

Shule ya kwanza iliyoongoza ni Marian Girls ya mkoani Pwani na ya pili ni Mzumbe ya Morogoro.

Mwanafunzi wa 1 wa kiume kwa sayansi ni Erasmi Inyase kutoka Ilboru, na kwa wasichana ni Lucylight wa Marian girls.

Upande wa masomo ya Biashara mwanafunzi wa 1 ametoka shule ya Tusiime anaitwa Erick Robert.

Wanafunzi 89 matokeo yao yamezuiliwa kwa sababu mbalimbali.

Wanafunzi watakaothibitika kuwa walikuwa na matatizo ya kiafya, watapewa nafasi ya kurudia mtihani.

Bofya hapa chini ujionee matokeo

http://www.necta.go.tz/matangazo2013/tangazo-usajili-ACSEE2014.pdf