Ni lazima tuwasaidie watu namna watakavyoondokana na ugumu wa misha, lazima tubadilishe fikra za kusubiri mabadiliko kutoka mashariki na magharibi. tuueleze ulimwengu kuwa sasa tumesoma ama kusomesha, hatupo gizani tena na tunataka kujikomboa. Nchi ina shida kubwa watu wake wanasubiri mabadiliko na viongozi wake wanayafuata mabadiliko na kuyatumia wenyewe. Tuelezane kuwa mabadiliko hayasubiriwi kwenye vijiwe vya bao na pombe bali ni kazi, kila mtu kwa imani yake nataka nimkumbushe kuwa Mungu aliumba misuli mingi kabisa itumike kufanya kazi yeye (Mungu) aachiwe kazi ya kubariki tukifanyacho. Mbadiliko si Facebook na Twitter kwa wagunduzi wake hawakusubiri mabadiliko bali walihakikisha wanayaleta na kuubabadili ulimwengu.
Nchi ya China ambayo lepo tunasumbuliwa na bidhaa zao kibao watu wake wanala masaa 3 au manne tu wakifanya jitihada kubwa kuleta mabadiliko. Leo nawakumbusha tu japo mjadala utakuwa mrefu juu ya mabadiliko.
Endelea kufuatilia ukurasa huu na kapagiii.blogspot.com