m

"If you want to conquer fear, don't sit at home and think about it. Go out and get busy. "

-- Dale Carnegie, motivational expert

Sunday, 19 January 2014

Serikali yawabeba waliofeli kidato cha pili


Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa. Picha na Maktaba 
Na Fidelis Butahe, Mwananchi

Posted  Jumapili,Januari19  2014  saa 2:0 AM
Kwa ufupi
  • Licha ya matokeo hayo kutotangazwa hadi sasa, imebainika kuwa waliofaulu mtihani huo uliofanywa Oktoba 7 hadi 21 mwaka jana ni asilimia 62 tu, asilimia 31 wakitakiwa kukariri (kurudia) kidato cha pili mwaka huu, huku asilimia saba wakishindwa mtihani huo kwa mara ya pili.
Dar es Salaam. Wakati Watanzania wakisubiri matokeo ya kidato cha pili mwaka 2013, imebaini kuwa Serikali imetoa agizo kwamba wanafunzi wote waliofeli mtihani huo kuendelea na masomo ya kidato cha tatu, huku wakisoma mafunzo ya kurudia mtihani wa kidato cha pili.
Licha ya matokeo hayo kutotangazwa hadi sasa, imebainika kuwa waliofaulu mtihani huo uliofanywa Oktoba 7 hadi 21 mwaka jana ni asilimia 62 tu, asilimia 31 wakitakiwa kukariri (kurudia) kidato cha pili mwaka huu, huku asilimia saba wakishindwa mtihani huo kwa mara ya pili.
Jumla ya wanafunzi 531,457 walitajwa na Wizara ya Elimu mwaka jana kuwa watafanya mtihani huo.
Uamuzi huo wa Serikali ni tofauti na ule uliotolewa na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa Novemba 4, mwaka 2012, kwamba kuanzia wakati huo mtihani wa kidato cha pili utakuwa ni wa mchujo na kwamba atakayefeli atatimuliwa.
Dk Kawambwa alisema matokeo ya mtihani wa kidato cha pili yatatumika kama kigezo cha kuchuja na kukariri kidato cha pili kwa watahiniwa watakaoshindwa kufikia wastani wa ufaulu wa alama 30.
Alisema mtahiniwa ataruhusiwa kukariri kidato cha pili mara moja tu na endapo mtahiniwa atashindwa mtihani kwa mara ya pili kwa mwaka utakaofuatia, itabidi aendelee na elimu ya sekondari nje ya mfumo rasmi.
Gazeti hili limeiona barua iliyoandikwa Januari 16 mwaka huu na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi na kusainiwa na Katibu Mkuu wake, Profesa Sifuni Mchome, kwenda kwa wadau wa elimu nchini, wakiwamo maofisa elimu wa mikoa na Chama cha Wamiliki wa Vyuo na Shule Binafsi (Tamongsco).
Katika barua hiyo, wizara hiyo imewataka wadau hao kuhakikisha kuwa wanafunzi watakaofeli mtihani huo, wanaendelea na masomo ya kidato cha tatu.
“Matokeo ya kidato cha pili yamepokewa na kufanyiwa uchambuzi ili kupata taswira ya taifa. Taarifa ya matokeo hayo imebaini kuwa watahiniwa waliofanya mtihani na kufaulu ni sawa na asilimia 62 tu,” inaeleza sehemu ya barua hiyo na kuongeza;
“Hali hii inaonyesha kuwa asilimia 31 ya wanafunzi watatakiwa kukariri kidato cha pili, 2014. Wale walioshindwa kwa mara ya pili ambao ni asilimia saba wanatakiwa kuendelea na masomo nje ya mfumo rasmi.”
Barua hiyo inaeleza kuwa wanafunzi waliofaulu kwa wastani wa alama 20 na kuendelea waendelee na masomo ya kidato cha tatu mwaka 2014, wakati awali Serikali ilitoa tamko kuwa watakaoshindwa kufikisha alama 30 watatimuliwa.
“Wanafunzi waliofaulu kwa wastani wa alama 20 hadi 39 wapewe mafunzo rekebishi ‘Remedial class’ wakiwa kidato cha tatu,” inaeleza sehemu ya barua hiyo
SOMA ZAIDI http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/-/1597296/2151230/-/utnth5z/-/index.html.

BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI LATAJWA

ASHA MIGIRO,NKAMIA NA SAADA WAULA,NCHIMBI,KAGASHEKI NJE, MAGUFULI APETA

Katibu kiongozi wa Serikali ya Tanzania oOmbeni Sefue kwa niaba ya rais Kikwete ametangaa baraza jipya la mawaziri.
                                         
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
UHAMISHO NA UTEUZI WA MAWAZIRI NA NAIBU MAWAZIRI
______________________________________________
            Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, amewahamisha na kuwateua baadhi ya Mawaziri na Naibu Mawaziri kama ifuatavyo:-
1.0              OFISI YA RAIS
Hakuna mabadiliko.
2.0              OFISI YA MAKAMU WA RAIS
2.1  Waziri wa Nchi (Muungano) - Hakuna mabadiliko
2.2   Mhe. Eng. Dr. Binilith Satano MAHENGE (Mb)
            Waziri wa Nchi (Mazingira).
2.3    Mhe. Ummy Ali MWALIMU (Mb)
                                                Naibu Waziri                            
3.0              OFISI YA WAZIRI MKUU
Hakuna mabadiliko
            4.0       WIZARA
           
                        4.1  WIZARA YA FEDHA
4.1.1        Mhe. Saada Mkuya SALUM (Mb)
            Waziri wa Fedha
                                    Mhe. Mwigulu Lameck NCHEMBA (Mb)           
                        Naibu Waziri wa Fedha
4.1.2        Mhe. Adam Kighoma Ali MALIMA (Mb)
                                                Naibu Waziri wa Fedha
                       
4.2              WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA
Hakuna mabadiliko
           
4.3       WIZARA YA KATIBA NA SHERIA
4.3.1    Mhe. Dkt. Asha-Rose Mtengeti MIGIRO (Mb)
                        Waziri wa Katiba na Sheria
4.3.2        Naibu Waziri - Hakuna mabadiliko
4.4      WIZARA YA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI
Hakuna mabadiliko
            4.5       WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA
           
4.5.1    Waziri - Hakuna mabadiliko
4.5.2    Mhe. Janet Zebedayo MBENE (Mb)
                                                Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara
            4.6       WIZARA YA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA
            Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi (Mb)
                                                Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa
           
4.7        WIZARA YA UJENZI
Hakuna mabadiliko
4.8       WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
4.8.1    Mhe. Mathias Meinrad CHIKAWE (Mb)
                        Waziri wa Mambo ya Ndani
                       
4.8.2        Naibu Waziri - Hakuna Mabadiliko
           

4.9       WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII
4.9.1        Mhe. Dkt. Seif Seleman RASHIDI (Mb)
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii
4.9.2        Mhe. Dkt. Kebwe Stephen KEBWE (Mb)
Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii
4.10     WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
4.10.1  Waziri:  Hakuna mabadiliko
4.10.2  Mhe. Jenista Joakim MHAGAMA (Mb)
                                                Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi
14.11   WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA NA WATOTO
14.11.1  Waziri: Hakuna mabadiliko
14. 11.2 Mhe. Dkt. Pindi Hazara CHANA (Mb)
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto
14.12  WIZARA YA MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVI
14.12.1 Mhe. Dkt. Titus Mlengeya Dismas KAMANI (Mb)
Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi
14.12.2 Mhe. Kaika Saning’o TELELE (Mb)
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi
14.13      WIZARA YA KAZI NA AJIRA
Hakuna mabadiliko
                                                              
14.14      WIZARA YA MAWASILIANO, SAYANSI NA TEKNOLOJIA
Hakuna mabadiliko
14.15   WIZARA YA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI
14.15.1  Waziri - Hakuna mabadiliko
14.15.2  Mhe. George Boniface Taguluvala SIMBACHAWENE (Mb)
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
14.16   WIZARA YA MAJI
14.16.1  Waziri - Hakuna mabadiliko
14.16.2  Mhe. Amos Gabriel MAKALLA (Mb)
Naibu Waziri wa Maji
14.17  WIZARA YA KILIMO, CHAKULA NA USHIRIKA
14.17.1  Waziri - Hakuna mabadiliko
            14.17.2   Mhe. Godfrey Weston ZAMBI (Mb)
Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika
            4.18     WIZARA YA UCHUKUZI
            Hakuna mabadiliko
4.19     WIZARA YA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO
4.19.1  Waziri -  Hakuna mabadiliko
4.19.2  Mhe. Juma Selemani NKAMIA (Mb)
Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo
4.20     WIZARA YA MALIASILI NA UTALII
4.20.1 Mhe. Lazaro Samuel NYALANDU (Mb)
Waziri wa Maliasili na Utalii
                        4.20.2 Mhe. Mahmoud Hassan MGIMWA (Mb)
                                                Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii
4.21     WIZARA YA NISHATI NA MADINI
4.21.1    Waziri - Hakuna mabadiliko
4.21.2    Naibu Waziri (Madini) - Hakuna mabadiliko
4.21.3  Mhe. Charles Muhangwa KITWANGA (Mb)
Naibu Waziri (Nishati)
     

Balozi Ombeni Y. Sefue
KATIBU MKUU KIONGOZI
Ikulu
DAR ES SALAAM
19 Januari, 2014