Tanzania imeshika nafasi ya 49 kati ya nchi 50 ambazo Shirika la Open
Doors la Marekani katika ripoti yake ya mwaka "2014 Watch List" imesema
ndio nchi hatari zaidi duniani kwa wakristo kuishi. Katika ripoti hiyo
Open doors wameiweka Tanzania katika kundi ambalo wakristo huishi kwa
wasiwasi huku pia likitoa idadi ya nchi 10 ambazo ni hatari zaidi
duniani kuwa Mkristo. Open doors hujishughulisha na kusaidia wakristo
waliopo vifungoni wakiwa katika hatari ya kuuwawa kutokana na kutetea
ama kuhubiri injili ya Yesu Kristo.
Katika orodha iliyotoa, shirika hilo limeonyesha nchi ambazo wakristo
wanaishi kwa kujificha, manyanyaso, kutekwa lakini pia wakiwa katika
hatari ya kuuwawa na serikali za nchi hizo ama vikundi hatari vya dini
vya watu wenye msimamo mkali wa dini.
Hii ni listi ya nchi hatari zaidi duniani kwa wakristo kuishi, ambao
hadi Tanzania kushika '50 bora', basi hakika hilo ni jambo la kuombea
kwa nguvu zote, na kama hufahamu, Baraza la Makanisa ya Kipentekoste
nchini limeshatangaza maombi ya kufunga na kuomba kwa siku 40 kuanzia Januari 6, hili ni mojawapo ya jambo linalostahili kushughulikiwa.
Taarifa za nchi tano duniani ambazo ni hatari zaidi kwa wakristo kuishi ni kama ifuatavyo;
1. NORTH KOREA/KOREA KASKAZINI
- Ni kosa la jinai kuwa mkristo au kushiriki katika shughuli za za Kikristo
- Katika vizazi vitatu mpaka sasa mmoja kati ya wanafamilia kuna uwezekano wamefungwa kwa kosa la kumiliki Biblia.
- Takribani wakristo 70,000 wapo gerezani wakitumikishwa kwa shughuli mbalimbali
2. SOMALIA
- Wakristo wanahusishwa kushirikiana na upande wa mataifa ya kikoloni yenye nguvu ya Ulaya
- Imependekezwa adhabu ya lifo kea mtu kuwa mkristo
- Kutokana na ukosefu wa serikali makini fujo zinazoletwa na vikundi vinavyopinga ukristo vinapewa nguvu na majeshi ya nchi.
3. SYRIA
- Makumi elfu wamekuwa wakihama makazi kutokana na vitisho na vurugu
- Takribani 50-60,000 ya wakristo katika mji wa Homs wameondolewa
- Makanisa mengi yamelipuliwa.
4. IRAQ/Iraki
- Idadi ya wakristo wanaoishi kwenye mateso inazidi kuongezeka toka vita ya kwanza ya Juba mwaka 1990
- Ongezeko la vitendo vya utekaji nyara, vitisho na mauaji tokea vita ya Gulf mwaka 2003.
- Asilimia 25 tu ndio wakristo sawa na idadi ya mwaka 1990
5. AFGHANISTAN
- Serikali imetoa vitisho vya adhabu ya kifo kwa yeyote atakayeacha Uislamu
- Kuna wakristo 1,200 nchi nzima
- Hakuna makanisa.
Imeandikwa awali na Christian Post, ukitaka kuona idadi kamili ya nchi 50 duniani ambako wakristo wapo hatarini bonyeza hapa.
CHANZO: gospelkitaa.blogspot.com