Binafsi nimekuwa na wasiwasi mkubwa juu ya the Hegue ikiwa kweli ni mahakama ya kweli na ya usawa kwa watu wote, nahisi ipo kwa ajili ya waafrika na zaidi kuwachonganisha ili kuendeleza ukoloni mamboleo. Inawezekanaje Uhuru na Ruto wakutwe na kesi lakini Odinga aliyeamuru watu na zaidi vijana waingie mtaani kupinga matokeo? si mtaani ndiko ukageuka uwanja wa mapigano?
Aaah nashikwa na kigugumizi na hivyo acha nimalizie habari kuapishwa, jambo lililonigusa kwa Uhuru ni ule msimamo na kujiamini na zaidi kusimama yeye kama yeye, ndio marais waliokosekana Afrika watu wanaoweza kuonyesha msimamo na kutoa maamuzi mazito ya kuleta mageuzi katika nchi zao. Afrika sasa inahitaji viongozi ambao hawatakuwa tayari kutishwa na vijibwa vya kizungu ambavyo kwa ajili ya kudoea maliasili zetu vinaleta uchonganishi kila kukicha. Binafsi sipingi kushtakia kwa viongozi waahalifu bali nataka nione wakishtakiwa Afrika, nataka kuona ICC ya kiafrika kama ile ya Arusha ya Mauaji ya kimbari. Mbona Mahakama ya Arusha hatujasikia ikishutumiwa na imefanya kazi zake kwa amani pasipo mgogoro wowote? Waafrika tuhukumiane wenyewe hata sisi tuna roho kama za wazungu rangi siwape shida. Sasa nafikiri ICC itabidi wafikiri upya. Uhuru kaapishwa ICC kunani? lazima wapate kigugumizi
Pia sitakuwa nimetenda vyema kwa kutomgusa Odinga yule rafiki yangu wa mwaka 2007, nasema rafiki yangu maana nilimpigia chapu katika uchaguzi ule hasa katika hadithi zetu vijiweni. Lakini Odinga huyu ambaye kwa kushindwa kwake watu elfu walikufa baadaye akapewa cheo kipya cha Waziri Mkuu badala ya kutekeleza ahadi akashughulika na cheo chake tu, na hapo akajipandishia mshahara wananchi wakibaki kuhaha tu na umaskini. Leo Odinga pasipo aibu anarudia kusema ameibiwa kura, mimi si mkenya lakini naelewa fikra za wakenya hasa linapokuja suala la utawala na ukabila. odinga kachakachuliwa kula na kutotimiza Ahadi kwake na roho ya ukabila iliyotawala kenya nas si vinginevyo. Jambo la ajabu kabisa ni vile Odinga asivyokomaa kisiasa kwa kuamua kukimbilia Afrika Kusini wakati mwenzake akiapishwa, hakika kaonyesha kutokuwa Mzalendo na zaidi kuwa kwake muhimu ni cheo na si utumishi.
Nampa Hongera Uhuru na Ruto na zaidi wapate changamoto ya kuwathibitishia wakenya na ulimwengu kuwa wanaweza kuleta maguzi kinyume na matariajio ya The Hegue.