m

"If you want to conquer fear, don't sit at home and think about it. Go out and get busy. "

-- Dale Carnegie, motivational expert

Wednesday, 25 December 2013

DALADALA ZA KENYA ZAJA NA UBUNIFU MPYA

Nairobi - Kenya - East Africa
Ukiwa kwenye jiji la Nairobi na ukaona magari yamechorwa rangi tofauti na graffiti, basi hizo ni daladala zao jijini Nairobi maarufu kama Matatu ambapo sasa hivi wamiliki wake wamekuja na ubunifu mpya ambao unawasaidia katika kufanya biashara zaidi na kuvutia wateja wengi sana.
Mtu wangu wa nguvu najua internet ni moja kati ya huduma unazotumia kila  siku na imekuwa inatumika kama kivutio cha biashara pia kwenye sehemu kadhaa ya biashara kama kwenye migahawa, Bar au Night club kwenye nchi zilizoendelea utakutana na internet ya bure kupitia WiFi. Basi wenzetu wa 254 Kenya wameanza kupiga hatua mbele kwenye kitu hiki baada ya matatu zao kuanza kutoa free internet kwa kutumia WiFi. fikiria na foleni hizi zilizopo Dar kama daladala zingekua na internet ya bure ndani yake watu wasingeuona ukali wa foleni kabisa… bila kusahau uhakika wa kufanya biashara ungeongezeka kwa sababu watu wengine wangechagua daladala zenye internet yenye speed. ukiwa katika jiji la Nairobi na simu yako ikiwa ina support WiFi, ukipanda matatu ni kama upo nyumbani au kazini. abiri wengi hivi sasa hutumia muda wa asubuhi kuelekea ofisini huku wakiangalia habari mbalimbali kwenye simu zao na kupitia mitandao ya kijamii..
Hivi sasa makonda wa matatuu wanaita abiria kwa kuongezea kionjo cha internet ya bure ipo, kwa mfano hata Dar kungekua na hiyo huduma ungemsikia konda tu anasema “Kariakoo Sokoni hiyoo mia nne na internet yenye kasi bureee”
Chanzo; http://feisaljumapinto.blogspot.com/2013/07/daladala-za-kenya-zaja-na-ubunifu-mpya.html

Aishi kwenye handaki kwa miaka minne

Chacha Makenge akitoka kwenye handaki lake. Picha na Florence Majani. 
Na Florence Majani, Mwananchi
  • Aliwahi kulazwa wodi ya wagonjwa wa akili Muhimbili

Tunaposikia handaki, fikra zinatupeleka moja kwa moja kwenye vita kwani aghalabu, mahandaki hutumiwa na watu kujificha wakati wa vita.
Hata hivyo, ugumu wa maisha umesababisha baadhi ya watu kuyageuza mahandaki kama makazi ya kuishi.
 Ni katika Barabara ya Sam Nujoma, natoka Ubungo kuelekea Mwenge, nashuka mita chache kabla ya kufika Mlimani City, naingia katika pori lililo nyuma ya Ukumbi wa Mlimani City.
 Hakuna njia maalumu ya kuingia katika pori hili. Hatua kwa hatua napita katikati ya vichaka na nyasi ndefu, hatimaye nafika katika eneo tofauti. Ni kama bustani iliyotengenezwa na mbunifu wa hali ya juu.
 Miti imefyekwa kwa utalaamu wa hali ya juu, baadhi ya vichaka vimepunguzwa  kwa umahiri na kutengeneza umbile zuri mfano wa maua yaliyotengenezwa. Lakini, mwisho kabisa wa mandhari hii kuna mianzi imelazwa chini na  pembeni kuna shimo.
 Shimo hilo ndilo handaki analoishi Chacha Makenge, kijana mwenye umri wa miaka 36, mzaliwa wa Mugumu Wilaya Serengeti Mkoa wa Mara kwa muda wa miaka minne sasa.
Hata hivyo, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Makenya Maboko anasema kuwa hana taarifa zozote kuhusu Makenge kuishi katika eneo hilo.
“Sina taarifa, wewe ni mtu  wa kwanza unanipa habari hizi, ngoja nilifanyie kazi,” anasema Profesa Maboko.
Jirani na handaki hilo namkuta Makenge akifyeka majani kwenye bustani yake. Ananikaribisha na tunaingia katika handaki hilo. Ni shimo refu, kwani tunatakiwa kushuka  ngazi tatu kubwa kwenda chini. Ndani kuna kitanda cha kamba na miti kilichofunikwa kwa magunia na shuka kadhaa.
 Ukuta ambao ni udongo, umechongwa mithili ya meza ndogo ambayo Makenge ameweka kioo, kitana, boksi lenye dawa mbalimbali na mswaki.
 Upande wa kulia wa handaki hili kuna  misumari iliyopigiliwa katika ukuta huo ambapo Makenge ametundika makoti na suruali, ambazo bila shaka ni zake.
Upande wa kushoto, Makenge kwa kutumia ukuta huo huo, ametengeneza meza nyingine ambayo imewekwa  chupa za plasitiki za maji  ya kunywa.
soma zaidi kwa kubofya hapa http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/Aishi-kwenye-handaki-kwa-miaka-minne/-/1597296/2120902/-/11ifsp3z/-/index.html

Nafasi ya Tanzania imeonekana msiba wa Mandela

Share bookmark Print Email Rating
 
Na Kelvin Matandiko, Mwananchi

Posted  Jumatano,Decemba18  2013  saa 13:10 PM
Kwa ufupi
  • Fursa iliyoipata Tanzania ya kuhutubia na aina ya hotuba iliyotolewa na Rais Kikwete kwenye mazishi ya Mandela imeipaisha nchi kidiplomasia na kufanya historia yake ijulikane dunia nzima. 


Matukio mbalimbali yaliyotokea Jumapili kwenye mazishi ya Rais wa kwanza mzalendo wa Afrika Kusini, Nelson Mandela yamenikumbusha yaliyotokea katika sherehe za miaka 50 tangu kuanzishwa OAU, sasa Umoja wa Afrika (AU).
Katika maadhimisho hayo, Tanzania ilimwagiwa sifa kedekede kutoka kwa wakuu wa nchi mbalimbali walioshiriki, wakiwamo Rais wa Senegal, Mark Sall, Waziri Mkuu wa Ethiopia, Hailemariam Dessalegne na Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini.
Rais Zuma alitoa hisia zake kwa Tanzania, akisema wazi kuwa wananchi wa nchi Afrika Kusini hawatausahau mchango wa Tanzania katika kuwakomboa na kuwafikisha walipo sasa. “Tulisaidiwa na nchi nyingi, lakini Tanzania ilitusaidia kwa namna ya kipekee.”
Sifa hizo ziliwekewa uzito katika hotuba ya Rais Jakaya Kikwete kwenye mazishi, alipoamua kueleza kwa uwazi historia ya Tanzania katika ukombozi wa Afrika Kusini na Afrika kwa jumla.
Awali, ilipofanyika ibada ya kumbukumbu ya Mandela ambapo viongozi mbalimbali zaidi ya 100 kutoka maeneo mbalimbali duniani walishiriki, Watanzania hawakuelewa kuona mchango wa Tanzania hauelezwi wazi katika tukio hilo muhimu wala kupewa fursa ya kuhutubia, lakini bila shaka nyoyo zao zilisuuzika baadaye Jumapili, fursa hiyo ilipopatikana siku ya mazishi.
Kauli ya Prof Mpangala
Miongoni mwa walioweka wazi dukuduku lao ni Profesa Gaudence Mpangala wa Kitengo cha Sayansi ya Jamii, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), akisema Tanzania ilitakiwa kupewa nafasi ya kuzungumza lolote kutokana na ukaribu wa nchi hizo.
Anasema Tanzania ni moja ya nchi duniani zenye historia kubwa na ujenzi wa taifa la Afrika Kusini.
“Na baada ya kutoka gerezani mwaka 1990, Tanzania ilikuwa nchi ya kwanza Mandela kuitembelea kwa lengo la kutoa shukrani zake, tukampatia na heshima ya jina lake kuitwa barabara muhimu, Mandela Road,” anasema Profesa Mpangala na kuongeza;
Sasa sijui ni utaratibu gani uliotumika kuangalia vigezo vya kuhutubia, kwa sababu siku zote rafiki yako wa karibu ndiye anayestahili nafasi ya kuzungumza siku ya msiba wako,” anasema.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) Usu Mallya anasema kutokana na mazingira hayo, kuna kila sababu ya Watanzania kujiuliza kwa sasa, iwapo thamani iliyokuwapo katika harakati za ukombozi bado inatambuliwa.
Anaongeza kuwa ni muhimu kukumbuka kwamba Tanzania ilikuwa kitovu cha harakati za ukombozi na kituo cha kuandaa fikra mbadala kwa ajili ya kutumika katika harakati za kuleta mabadiliko kwa ndani na nchi nyingine za Afrika.
Kusoma zaidi bofya hapa http://www.mwananchi.co.tz/Makala/Nafasi-ya-Tanzania-imeonekana-msiba-wa-Mandela/-/1597592/2117016/-/cnsj5cz/-/index.html

Watoto wa mitaani wanavyobakwa Sumbawanga

Share bookmark Print Email Rating
Baadhi ya watoto wa mitaani wakiwa wamelala nje kutokana na kukosa sehemu za kulala.Baadhi yao kwa kutaka sehemu nzuri za kulala na chakula kizuri huwa tayari kufanyiwa vitendo vibaya. Picha na Mkataba 
Na Mussa Mwangoka, Mwananchi

Posted  Jumatano,Decemba18  2013  saa 15:7 PM
Kwa ufupi
  • Baadhi ya watoto wa mitaani wanakiri kufanyiwa unyama huo na watu mbalimbali.Vitendo hivyo hufanywa kwa siri kubwa, kutokana na ukweli kwamba watoto hao katika hali ya kujilinda wameaanzisha mkakati maalum kupambana na watu wanaolawiti na kuwabaka watoto.
Watoto kulawitiwa ili wapate hifadhi ya kulala au kupewa chakula kizuri ni sehemu ya maisha ya baadhi ya watoto waishio mitaani mjini Sumbawanga mkoani Rukwa.
Hii ni siri kubwa ambayo imejificha miongoni mwao, ili uweze kupata siri hii inakulazimu lazima ujenge uhusiano wa karibu na wa muda mrefu na watoto hao.
Watuhumiwa wakubwa wa kuwaingilia kinyume na maumbile watoto hao ni baadhi ya walinzi wanaolinda katika maduka ya biashara na vijana waliowazidi umri; vitendo hivyo vinaonekana  kushika kasi.
Uchunguzi wa kina uliofanywa na Mwandishi wa makala haya kwa miezi kadhaa, umebaini kuwa vitendo vichafu vimesababisha baadhi yao kuathirika kisaikolojia hivyo kujikuta wakiona jambo hilo ni la kawaida na hulifurahia.
Watoto hao hufanyiwa vitendo hivyo hasa kipindi cha masika ambapo mvua huwa zinanyesha, maeneo ambayo hupendelea kulala nyakati hizo kwenye majumba ambayo ujenzi wake haujamalizika (Mapagala) huwa yanavuja maji ya mvua hivyo hulazimika kuyazikimbia kujisalimisha popote.
Watoto wa mitaani
Baadhi ya watoto wa mitaani waliozungumza na mwandishi walikiri kwamba ni kweli kuna tabia hiyo lakini ni kwa usiri mkubwa kwani iwapo itabainika mtu anamlawiti mtoto mwenzao huwa wanapambana naye.
“Unajua sisi tunawasaidia walinzi katika malindo yao nyakati za usiku, tulishakubaliana kama kuna mwenzetu analawitiwa na anakubali tutamtenga.
Wapo watoto wawili tayari tumewatenga katika kundi letu kwa tabia ya kupenda kulawitiwa, sasa kama wapo wengine tukiwafahamu nao tunawatenga hata wakipata matatizo hatuwezi kuwasaidia” mtoto mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Jose (siyo jina lake halisi).
Naye mtoto aitwaye Juma anasema kuwa kinachowaponza watoto wengine ni tamaa na sio hifadhi ya kulala pekee kwani wapo watoto ambao wamezitoroka familia zao kwa kisingizio cha ugumu wa maisha na kukimbilia mitaani kufanya kazi ya kuombaomba ambapo wamekuwa wakidanganyika kwa vyakula kama Chips na pombe katika baa za usiku.
“Sisi wengine tupo huku mitaani kwa sababu mbalimbali zikiwemo za kipato duni cha familia zetu, malezi mabaya kama vile kulelewa na kina mama wa kambo ambao ni chanzo matatizo kwa sehemu kubwa lakini sio sababu ya kukubali kulawitiwa.
Ila wapo wale wanaopenda pombe na chips ndio wanajikuta wakishawishiwa na sio tu na walinzi lakini pia hata baadhi ya watu ambao hutumia kisingizio cha ulevi wa pombe ili kufanya vitendo hivyo,” anasema mtoto Maiko (siyo jina lake halisi).
Bofya hapa kwa habari zaidi http://www.mwananchi.co.tz/habari/habari-ya-ndani/Watoto-wa-mitaani-wanavyobakwa-Sumbawanga/-/1724700/2117114/-/s0l8dj/-/index.html

Zitto ‘awalipua’ Dk Slaa, Mbowe

Share bookmark Print Email Rating
Mbunge wa Kigoma kaskazini, Zitto Kabwe akihutubia Wakazi wa Kijiji cha Bitale alipokuwa katika ziara ya kutembelea baadhi ya Vijiji.Picha na Anthony Kayanda 
Na Fredy Azzah, Mwananchi

Posted  Jumatano,Decemba25  2013  saa 9:21 AM
Kwa ufupi
Awataka waache kusambaza maneno ya uongo dhidi yake
SHARE THIS STORY
0
Share


Kigoma.Mbunge wa Kigoma Kaskazini,Zitto Kabwe, amejibu mashambulizi kwa viongozi wa Chadema, kutokana na kile alichosema wanazunguka na kusema maneno yasiyo ya ukweli.
Akihutubia maelfu ya wananchi waliokusanyika katika Uwanja wa Mwanga Centre, Kigoma mjini, alisema alichukua kadi ya uanachama wa Chadema mwaka 1993 wakati huo, Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Wilbrod Slaa akiwa bado yuko CCM.
“Wakati hao wenye midomo mikubwa wanaoongea sasa, walipokuwa wamekumbatia watawala, nyinyi mlikuwa mnapigwa mabomu kutaka mageuzi, eti leo wao wapinzani zaidi kuliko sisi na ndiyo maana hatuwezi kuwaachia.
Hatuwezi kukubali, hatutoki, demokrasia ni mchakato na mwenzenu nimekuwa kwenye mchakato huu. Kadi yangu ya Chadema nimeichukulia kwenye uwanja huu, tarehe moja mwezi wa nne mwaka 1993, nikiwa na miaka 16, wakati nachukua kadi yangu, Katibu Mkuu wa chama changu alikuwa yuko CCM.
Akizungumza kile alichosema ni uongo unaosambazwa na viongozi wa juu wa chama hicho, Katibu Mkuu Dk Slaa na Mwenyekiti wake Mbowe waligawana maeneo Mbowe akaenda Kanda ya Ziwa na Dk Slaa Kanda ya Magharibi.
Alisema kwenye mikutano hiyo, Mbowe anasema kuwa endapo mbunge huyo atarudi yeye Mbowe atajiuzulu, suala alilosema linaonyesha kuwa tayari ameshafukuzwa bila hata utetezi wake kusikilizwa.
Alisema baada ya viongozi hao kuzungumza na kusema mambo hayo na yeye aliamua kurudi nyumbani Kigoma na baada ya kuona hilo Dk Slaa akahoji mbunge huyo anafanya vikao hivyo kama nani.
“Mimi nimekata rufaa, wajumbe wa baraza kuu wa Mtwara, Ruvuma wanaandika barua wanataka mkutano mkuu, Katibu Mkuu akiwa Igunga anasema hiyo ni haramu na hao wafuasi wa Zitto watafanya Zitto afukuzwe, si __wamwamesha nifukuza? takachokuja kunijadili, hivyo si wameshanifukuza ?\
Chanzo'; mwananchi,co.tz