m

"If you want to conquer fear, don't sit at home and think about it. Go out and get busy. "

-- Dale Carnegie, motivational expert

Monday, 24 February 2014

Facebook kununua WhatsApp kwa Sh 30.9 trilioni



Usimamizi wa Facebook ulisema utalipa Dola4 bilioni pesa taslimu na Dola 13 bilioni kupitia ubadilishanaji wa hisa.PICHA|MAKTABA 
Na Mwandishi wetu, Mwananchi

Posted  Ijumaa,Februari21  2014  saa 24:0 AM
Kwa ufupi
WhatsApp ni maarufu miongoni mwa vijana wanaotafuta kuepuka kulipia huduma ya kutuma ujumbe mfupi wa simu (SMS).


Marekani. Kampuni ya Mtandao wa Jamii ya Facebook imesema itanunua mtandao wa mawasiliano wa ujumbe mfupi wa WhatsApp kwa Dola 19 bilioni za Marekani (Sh30.9 trilioni), ili kuimarisha umaarufu wake hasa miongoni mwa vijana.
Pia, wasimamizi wa Facebook walitangaza nyongeza zaidi ya Dola 3 bilioni zitalipwa waanzilishi wa Mtandao wa WhatsApp na wafanyakazi wake.
Hiyo ndiyo biashara kubwa zaidi ya ununuzi ambayo iliwahi kutekelezwa na Facebook kufikia sasa.
WhatsApp ni maarufu miongoni mwa vijana wanaotafuta kuepuka kulipia huduma ya kutuma ujumbe mfupi wa simu (SMS).
WhatsApp iliweza kuwasajili zaidi ya watumiaji milioni 450. Katika taarifa yake, Mwanzilishi wa Facebook, Mark Zuckerberg alisema mtandao huo upo kwenye harakati ya kuwaunganisha watu bilioni moja, jambo litakalofanya Facebook kuwa na thamani kubwa zaidi.
Zuckerberg alisema idadi kubwa ya watumiaji wa Facebook wanatumia simu za mkononi, hivyo mtandao wa WhatsApp ambao hutumiwa kwa simu utasaidia kuimarisha mawasiliano kwa gharama ya chini. Mitandao hiyo imekuwa na watumiaji wengi duniani.
Jan Koum alitangazwa kujiunga na bodi ya usimamizi wa mtandao wa Facebook.
Usimamizi wa Facebook ulisema utalipa Dola4 bilioni pesa taslimu na Dola 13 bilioni kupitia ubadilishanaji wa hisa.
Masharti
Watumiaji wa WhatsApp na Facebook ambao ni wengi katika mataifa ya Amerika na Canada walisifu hatua hiyo.
Mamlaka ya Facebook iliahidi kudumisha masharti ya WhatsApp na kutoa kitita cha 1milioni kulipa iwapo masharti hayo yatakiukwa.
Mapema mwezi huu Facebook ilisherehekea miaka 10 tangu kubuniwa na kufikia sasa ina watumiaji zaidi ya bilioni moja.
Soma zaidi http://www.mwananchi.co.tz/kitaifa/Facebook-kununua-WhatsApp-kwa-Sh1-36-trilioni/-/1597568/2215618/-/item/1/-/fqr6tj/-/index.html