m

"If you want to conquer fear, don't sit at home and think about it. Go out and get busy. "

-- Dale Carnegie, motivational expert

Monday, 6 January 2014

Chadema yawatimua Dk Kitila, Mwigamba


Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa akiandaa nyaraka za ushahidi dhidi ya viongozi waliofukuzwa kwenye chama hicho juzi, kabla ya kuzungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana. Kulia ni Mwanasheria wa Chadema, Tundu Lissu. Picha na Fidelis Felix 
Na Fidelis Butahe na George Njogopa, Mwananchi

Posted  Jumatatu,Januari6  2014  saa 8:9 AM
Kwa ufupi
  • Yasema waraka wao wa mabadiliko ulikuwa na nia ya kukimaliza chama na viongozi wake wa juu

Dar es Salaam. Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) imewafukuza uanachama, aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho, Mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba na aliyekuwa Mjumbe wa Kamati Kuu, Dk Kitila Mkumbo.
“Tumewavua uanachama kutokana na makosa ya kuandaa waraka wa Mkakati wa Mabadiliko 2013,” alisema Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa mbele ya waandishi wa habari.
Wakati hayo yakifanyika, imeelezwa kuwa aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wake, Zitto Kabwe ataendelea na  uanachama na ubunge kwa sababu ya mahakama, siyo kwa matakwa ya chama hicho.
Zitto ambaye alitajwa kuwa mhusika mkuu katika waraka huo amefungua kesi akiomba Mahakama Kuu izuie uanachama wake kujadiliwa hadi rufani yake itakaposikilizwa na Baraza Kuu la chama.  Hatima ya maombi hayo itajulikana leo.
Maamuzi ya kikao
Akitangaza uamuzi wa kikao cha dharura cha Kamati Kuu kilichokutana kwa siku mbili jijini Dar es Salaam jana, Dk Slaa alisema, “Kuhusu Zitto Kamati Kuu haikujadili wala kuamua juu ya mashtaka dhidi yake.”
Huku akiyataja makosa 11 ya Zitto, Mwigamba na Dk Kitila yaliyotokana na waraka huo, Dk Slaa alisema, “Baada ya kumhoji Dk Mkumbo alikiri wazi kuwa Zitto alikuwa akiujua waraka huu ambao ulilenga kukiuka chama, kutengeneza tuhuma dhidi yangu na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe.”
Katika mkutano huo Mwanasheria Mkuu wa chama hicho, Tundu Lissu alisema Zitto ataendelea kuwa mwanachama wa Chadema na mbunge kwa sababu ya  mahakama na siyo matakwa ya Chadema.
Zitto ambaye ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Mwigamba na Dk Kitila, Novemba 22 mwaka jana walivuliwa nyadhifa zao na Kamati Kuu baada ya kukamatwa kwa waraka huo.
Waraka huo ulioandaliwa na Mwigamba na Dk Kitila, uliolenga kufanya mabadiliko makubwa ya kiuongozi wakati wa uchaguzi mkuu wa ndani wa chama hicho, huku Zitto akipendekezwa kuwania nafasi ya uenyekiti.
Utetezi wa watuhumiwa
Katika ufafanuzi wake kuhusu utetezi wa watuhumiwa, Dk Slaa alisema, “Dk Kitila pekee, ndiye alikuja kuhojiwa na Kamati Kuu iliyokutana Januari 3 hadi 4 na kwamba alikubali kuandaa waraka lakini alikataa kwa kuwa ulikiuka katiba na kanuni za chama. Pia alikataa kumtaja kwa jina mwandishi mwingine wa waraka huo anayetajwa kwa jina la M2.”
Soma zaidi http://www.mwananchi.co.tz/habari/Siasa/Chadema-yawatimua-Dk-Kitila--Mwigamba/-/1597332/2135732/-/k2po63/-/index.html