m

"If you want to conquer fear, don't sit at home and think about it. Go out and get busy. "

-- Dale Carnegie, motivational expert

Wednesday, 24 October 2012

Muuaji wa MWangosi afikishwa mahakamani

MTUHUMIWA WA MAUAJI WA DAUDI MWANGOSI AFIKISHWA TENA MAHAKAMANI LEO

Mtuhumiwa Pacficus akipelekwqa mahakamani chini ya ulinzi mkali 

Mtuhumiwa wa mauaji ya aliyekuwa mwandishi wa habari wa kituo cha televisheni cha Channel Ten Daud Mwangosi leo amefikishwa tena katika Mahakama ya Hakimu Mfawidhi ya Wilaya kujibu shitaka lilalomkabili.Huku akiwa chini ya ulinzi mkali wa askari.

Akisomewa shitaka lake na mwendesha mashtaka wa serikali Mkuu lilian Ngilangwa , amesema mtuhumiwa huyo ambaye ni askari mwenye namba G2573 Pasificus Cleophace Simoni (23) mkazi wa FFU Iringa, anakabiliwa na shitakala la mauaji ya makusudi.

Amesema mtuhumiwa huyo mnamo 02 Septemba mwaka huu katika kijiji cha Nyololo Wilaya ya Mufindi Mkoa wa Iringa alimuua Daudi Mwangosi kwa makusudi kinyume na kifungu cha sheria namba 148 kifungu kidogo 5A.i cha makosa ya jinai.

Mbele ya Hakimu Mkuu Mwandamizi wa mahakama ya hakimu Mfawidhi ya Wilaya Dyness Lyimo mtuhumumiwa hakutakiwa kujibu chochote kwa kuwa mahakama hiyo haiwezi kusikiliza kesi za mauaji.

Kwa mujibu wa kesi za jinai, sheria kifungu 196 kanuni ya adhabu Cap. 16 iliyofanyiwa marejeo mwaka 2002, kinakataza mtuhumiwa wa mauaji ya kukusudia kupewa dhamana.

Mtuhumiwa amerudishwa mahabusu kutokana na kesi yake kukosa dhamana kisheria na kesi hiyo imeahirishwa hadi 7 Novemba mwaka huu itakapotajwa tena mahakamani hapo.

Mtuhumiwa huyo aliletwa chini ya ulinzi mkali wa polisi kaitka gari la polisi lenye number za usajili PT 1467.

Huku waandishi wa habari wakizuiwa kupiga picha jambo lililosababishwa kusukumwa kwa mwandishi wa majira Elias Ally na mmoja wa Polisi hao.

Saturday, 20 October 2012

Maandamano ya Kutetea????? na Polisi

Dar kwachafuka, ni vita si maandamano maana hata jeshi limetumika. Jamani Uislamu naambiwa maana yake nia amani inakuwaje Dunia nzima vurugu zisababishwe na waislamu tu. Inachosha kusikia vurugu za waislamu dunia nzima, Hebu Tanzama karibu nchi zote zinazopigana duniani ni za kiislamu, twende Niaijeria, Sudani, Misri, Syria, Afghanistan, Mali, Libya, packstani n.k Mahali popote penye uislamu amani iemkuwa tatizo kubwa. Tuinuke tuombe Mungu maana la sivyo hali itakuwa tete. Waamuzi 6:27-32 inajibu juu ya madai ya kiislamu kwamba kama Mungu wao au mtumu wao ni Mungu basi na ajitetee mwenyewe iwaje atetewe. Kama Mungu anahitaji kutetewa kiasi atawezaje kutatua matatuzo makubwa ya kibinadamu, atawezaje kuponya ikiwa hawezi kumuwajibisha mwanadamu anayemdhihaki au kumkejeli( Huyo atakuwa siyo Mungu, huyo ni sawa tu na Baali.

hapa kuna matukio kwa mujibu wa globalpublishers

Kapagi.

MAANDAMANO YA WAISLAMU YALIVYOCHAFUA HALI YA HEWA JIJINI DAR LEO

Wananchi wakitawanyika wakati wa vurugu eneo la Msimbazi, Kariakoo jijini Dar.
Polisi wakiimarisha ulinzi eneo la Kariakoo leo.
Hivi ndivyo hali ilivyokuwa leo katika maeneo ya Kariakoo jijini Dar es Salaam baada ya polisi kuzuia maandamano yaliyotaka kufanywa na baadhi ya waumini wa dini ya Kiislamu kitendo kilichopelekea mabomu ya machozi kulipuliwa na baadhi ya waumini hao kutia nguvuni na polisi.
Magari ya Jeshi la Wananchi Tanzania yakielekea Kariakoo kwa ajili ya kuimarisha ulinzi eneo hilo.
Jamaa huyu alidakwa na polisi wakati wa maandamano hayo.
Polisi wakiwatangazia wananchi waliokuwa eneo la Kariakoo kutawanyika mara moja wakati wa vurugu hizo.
Mama huyu alipoteza fahamu baada ya milipuko kadhaa kutokea eneo hilo.
Polisi wakiwa kazini kuzuia maandamano hayo.
Baadhi ya waandamanaji waliokamatwa wakati wa vurugu hizo wakiingizwa kituo cha polisi Msimbazi.
(PICHA: MAKONGORO OGING', HARUNI SANCHAWA NA RICHARD BUKOS / GPL)

Thursday, 18 October 2012

VURUGU ZA UAMSHO ZANZIBAR NA SHEHE PONDA AKAMATWA



Wednesday, 17 October 2012 21:34

Kiongozi wa Kundi la Uamsho, Sheikh Farid Hadi Ahmed
GARI, BAA VYACHOMWA MOTO, NI BAADA YA KIONGOZI WA UAMUSHO KUTEKWA, PIA SHEHE PONDA KUTIWA MBARONI
Waandishi Wetu, Dar na Zanzibar
POLISI mkoani Dar es Salaam na wale wa Kisiwani Zanzibar, jana walitumia mabomu ya machozi na maji ya kuwasha kusambaratisha makundi ya watu wanaodaiwa kuwa waumini wa Dini ya Kiislamu, waliopanga maandamano kushinikiza kuachiwa kwa viongozi wao.

Kisiwani Zanzibar vurugu kubwa ziliibuka baada ya kusambaa taarifa kuwa Kiongozi wa Kundi la Uamsho, Sheikh Farid Hadi Ahmed alitekwa nyara juzi saa 3 usiku akiwa kwenye gari lake na dereva wake.

Vurugu hizo zilisababisha uharibifu wa mali kadhaa ikiwamo Maskani Kaka ya Kisonge inayomilikiwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambayo ilichomwa moto na waandamanaji.


Waandamanaji hao pia walichoma moto baa za Darajani na Mbawala eneo la Mikunguni na baadhi ya nyumba za kulala wageni, kabla Vikosi vya Kutuliza Ghasia (FFU) na Kikosi cha Zima Moto kudhibiti vurugu hizo kwa mabomu ya kutoa machozi.

Pia magari kadhaa yalichomwa moto na kuharibiwa vibaya yakiwa yameegeshwa katika maeneo mbalimbali, huku mipira na matairi vikichomwa katika barabara kadhaa.

Katika maeneo ya Mjini baadhi ya njia zilifungwa na watu waliokuwa wakitoka kazini walishindwa kwenda nyumbani. Maeneo yaliyoathirika zaidi ni yale ya Malindi, Darajani hadi Michenzani ambako njia zilifungwa na mabomu yalisikika yakipigwa mfululizo.

Katibu wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (Jumiki), Sheik Abdallah Said alisema,
“Taarifa tulizonazo ni kwamba Sheikh Farid ametoweka katika mazingira ya kutatanisha…Alitoka kwake Mbuyuni katika gari yeye na kijana wake wa hapo nyumbani, lakini baadaye kuna gari ikamfuata na kusimama na ndipo alipoingia katika hilo gari jingine na hakuonekana tena. Hatujui ni kina nani waliomchukua na hatujui ilikuwaje akaingia katika hilo gari ...”

Polisi waliimarisha ulinzi katika baadhi ya maeneo hasa Msikiti wa Mbuyuni ambao uko jirani na makazi ya Sheikh Farid. Kamishna wa Polisi Zanzibar, Mussa Ali Mussa alisema polisi halihusiki na kukamatwa kwa Farid, lakini wao wanaamini kwamba ‘amejipoteza’ mwenyewe na kujificha.

Kamishna Mussa alisema polisi watawasaka wote waliosababisha vurugu hizo, na kwamba hadi sasa hawafahamu chanzo chake bado.

“Tunafanya uchunguzi zaidi kujua chanzo cha fujo hizo ingawa mimi sijui habari za kutekwa Farid, sasa tunasema tunachunguza chanzo cha vurugu hizo na tukishapata uthibitisho na waliosababisha tutawafikisha mahakamani kujibu mashtaka,” alisema kamishna huyo.

Ilivyokuwa Zanzibar
Vurugu hizo zilianza katika maeneo mbalimbali muda mfupi baada ya vijana kadhaa kukusanyika katika eneo la Darajani kando ya Soko Kuu majira ya asubuhi, kutokana na kuzagaa kwa taarifa kwamba Sheikh Farid alikuwa haonekani.

Idadi ya vijana hao ilikuwa ikiongezeka kadiri muda ulivyosonga, huku wengi wao wakiwa na silaha za aina mbalimbali zikiwamo magongo na mawe, hali iliyoibua hofu kwa wafanyabiashara wa eneo hilo, hivyo baadhi yao waliamua kufunga maduka.

Maeneo yalioharibiwa ni pamoja na baadhi ya nyumba za kulala wageni ambazo zimechomwa moto katika eneo la Amani, huku baadhi ya vijana wakionekana wakikimbia na kreti za pombe.

Katika eneo la Darajani, vijana kadhaa wakishirikiana na Wamachinga, walionekana wakivunja kisha kuingia katika moja ya maghala ya kuhifadhia bia, ambako walipora bidhaa zote zikiwamo kreti kadhaa za bia zilizokuwa zimehifadhiwa humo.

Baadhi ya wenye maduka walifunga na kutoweka, lakini waporaji waliiba baadhi ya bidhaa vikiwamo vyakula, kisha  kutokomea navyo kusikojulikana.

Katika maeneo ya Ng’ambo ambayo ni Amani, Mikunguni, Kwerekwe na Daraja Bovu vijana walioonekana kuwa na hamasa, waliingia kwenye makazi ya watu na kuiba vitu kadhaa, na kila mabomu yalipopigwa walikimbilia vichochoroni na baada ya muda walirejea tena.

Maeneo ya Malindi, Michenzani na  Rahaleo, kulikuwa na vurugu za urushaji mawe na kusababisha uharibifu mkubwa wa miundombinu katika maeneo hayo.

Matawi ya miti ilikatwa na kuunganishwa na magari mabovu kuwekwa barabarani kisha kuchomwa moto. Hali hiyo ilisabababisha uharibifu mkubwa katika baadhi ya barabara, na katika fujo hizo baadhi ya vijana walikamatwa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, Azizi Juma Mohammed alithibitisha kutokea kwa fujo hizo na kusema Jeshi la Polisi linafanya uchunguzi kujua chanzo chake na taarifa kamili zitatolewa baada ya kukamilika uchunguzi huo.

Ponda Dar
Jijini Dar es Salaam, baadhi ya watu walipanga kufanya maandamano hadi Makao Makuu ya Polisi, kupinga kukamatwa kwa Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu, Sheikh Ponda Issa Ponda aliyekamatwa juzi usiku na kushikiliwa kutwa nzima ya jana katika Kituo Kikuu cha Polisi.

Ponda alitiwa mbaroni kwa tuhuma za kuchochea vurugu na uvunjifu wa amani jijini Dar es Salaam, na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alisisitiza kuwa polisi wamechoka kuvumilia harakati zake za kutaka “nchi isitawalike”.

“Kuanzia leo uvumilivu kwa Jeshi la Polisi dhidi ya watu wasiofuata sheria za nchi umekwisha. Kwa kuwa Ponda ni mtu anayepotosha watu waliopo chini yake wanaotaka kuandamana bila utaratibu wasitulaumu kwa lolote lile litakalotokea,” alisema Kova.

Kova alisema hadi jana Ponda alikuwa bado anahojiwa katika Kituo Kikuu cha Polisi, Mkoa wa Dar es Salaam na kwamba ushahidi ukijitosheleza, atafikishwa mahakamani wakati wowote.

Alisema taasisi anayoingoza Sheikh Ponda haijasajiliwa kwa mujibu wa sheria kufanya shughuli za dini. Hivyo basi shughuli zote zinazoendesha na taasisi hiyo si halali.

"Natoa wito pia kwa wafuasi wa kiongozi huyo, walioshiriki katika vurugu mbalimbali za hivi karibuni, wajisalimishe haraka kwa kuwa sasa tupo katika mchakato wa kuwasaka, kuwakamata na baadaye kuwafikisha mbele ya sheria," alisema.

Tuhuma za Ponda
Kamanda Kova alidai kuwa Sheikh Ponda amekuwa akichochea vurugu na kuwashawishi wafuasi wake kuidharau Serikali na vyombo vya usalama.

“Ponda amekuwa ni mtu ambaye amefanya nchi hii, hasa katika Jiji la Dar es Salaam kukaa katika hali ya wasiwasi. Ijumaa imekuwa siku ya fujo badala ya kuwa siku ya amani,” alisema Kova.

Alisema vurugu hizo zinazoongozwa na Sheikh Ponda zimekuwa zikisababisha baadhi ya watu kushindwa kwenda kazini siku za Ijumaa na hali hiyo haivumiliki tena.

Kamanda Kova alitaja tuhuma nyingine dhidi ya Sheikh Ponda kuwa ni kuongoza kundi la watu kwenda kuvamia kiwanja namba 311/3/4 eneo la Chang’ombe ambacho kinamilikiwa  na kampuni Agritanza.

"Kiwanja alichokwenda kukivamia kilikuwa mali ya Baraza Kuu la Waislamu nchini (Bakwata) na kiliuzwa kihalali kwa kampuni hiyo," alisena.

Alitaja tuhuma nyingine kuwa ni kufanya maandamano kinyume cha sheria, ikiwamo kuweka kambi Makao Makuu ya Polisi bila kibali cha jeshi hilo wiki kadhaa zilizopita.

Kamanda huyo alisema Ponda anashikiliwa pia kwa kuwa mstari wa mbele kupambana na vyombo vya dola  na Serikali, ikiwa ni pamoja na kushawishi wafuasi wake kumdharau Rais wa nchi.

“Vilevile amekuwa akiendesha maandamano na kukusanyika Kiwanja cha Kidongo Chekundu, huku wakijitapa kuwa wana nguvu zaidi ya Jeshi la Polisi,” alieleza Kova.

Polisi pia wanamtuhumu Ponda kwa kuanzisha vurugu na vitisho dhidi ya Sheikh Mkuu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata), Mufti Shaaban Bin Simba na kutaka kumtoa madarakani kwa nguvu pamoja na kutaka kuvamia ofisi yake.

Alikamatwaje?
Kamanda Kova alisema Ponda alikamatwa na askari waliomuwekea mtego kutokana na yeye kuwa bingwa wa kutoroka kila akifanya matukio.

“Askari waliowekwa maalumu kwa ajili ya kumkamata walifanikiwa kumtia nguvuni saa 4:00 usiku karibu na eneo la maficho yake ambako alipelekwa na pikipiki,” alisema Kova.

“Hivi Ponda ni nani mpaka awe na uwezo wa kumpa Rais aliyechaguliwa na wananchi siku saba kuwaachia watu waliopo mahakamani yeye amechaguliwa na nani kuongoza taasisi aliyonayo na anatoa wapi nguvu za kufanya mambo yote hayo?,” alihoji Kova.

Alisema kulingana na matukio anayoyaongoza Ponda, wananchi wameanza kuona kama anaogopwa na vyombo vya dola, jambo ambalo siyo kweli.

Aliongeza kuwa polisi wana uwezo wa kumdhibiti, isipokuwa walikuwa wanatumia busara tangu alipoanza vurugu na kwa sasa uvumilivu umewashinda, hivyo wataanza kumshughulikia.

Vurugu zazuka
Kukamatwa kwa Sheikh Ponda kulizua vurugu jijini Dar es Salaam na kufanya baadhi ya wakazi wake hasa maeneo ya Mnazi Mmoja na Kariakoo, kuingiwa kiwewe baada ya polisi kutumia mabomu ya machozi na maji ya kuwasha ili kuwasambaratisha watu waliokuwa wanataka kuandamana kwa lengo la kushinikiza kiongozi huyo aachiwe.

Hali hiyo ilisababisha watu kukimbia ovyo katikati ya iji na kuongezeka kwa misongamano ya magari, jambo lililofanya usafiri wa daladala kuwa mgumu kwenda na kutoka katikati ya maeneo ya Jiji la Dar es Salaam.

Baadhi ya wafanyabiashara walifunga maduka yao wakihofia kuporwa mali wakati wa vurugu hizo, baada ya vibaka kujichanganya wakijaribu kufanya uhalifu huo.

Katika eneo la Mnazi Mmoja, polisi walirusha maji ya kuwasha kusambaratisha kundi la watu hao, huku wengine wakiwa wanadhibitiwa walipokuwa wakienda Makao Makuu ya Polisi ili kumtoa kiongozi huyo.

Baadhi ya mashuhuda walisema, mbali na Ponda watu hao walikuwa wanataka kwenda polisi kuwatoa watu waliokuwa wanashikiliwa kituoni hapo kwa tuhuma za kufanya vurugu na kuharibu makanisa katika Kata ya Mbagala wilayani Temeke.

Imeandikwa na Salma Said, Zanzibar, Zaina Malongo na Festo Polea, Dar.

E&P

Chanzo: Mwananchi

Tuesday, 16 October 2012

TAKWIMU ZA UCHOMAJI MAKANISA TANZANIA NA TAMKO LA TAG

TAKWIMU ZAONYESHA TANGU MWAKA 1985-2012 MAKANISA 46 YAMECHOMWA ,KUBOMOLEWA NCHINI


Askofu David Mwasota.

             
Imeelezwa  kuwa tangu kuibuka kwa wimbi la uchomaji wa  makanisa linalofanywa na watu wanaoaminika kuwa wanaharakati wa  Kiislamu katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limeyakumba zaidi ya makanisa 46.

Hayo yameelezwa na Katibu Mkuu wa  Baraza la Maaskofu wa Kipentekoste nchini Tanzania (PCT) Askofu David Mwasota wakati akizungumza na Gazeti Msemakweli akiwa Kisiwani Zanzibar.

Kiongozi huyo  alikuwa mmoja wa wajumbe  wa mkutano uliowakutanisha viongozi wa dini ya Kikristo, viongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ)na makamanda wakuu wa jeshi la Polisi ambapo ulijadili kwa kina juu ya vurugu zilizotokea visiwani Zanzibar.

Kwa mujibu ya Mwenyejiti wa kundi linaloendesha mihadhara ya Kikristo inayosahihisha upotoshwaji wa Maandiko Matakatifu ya Biblia unaofanywa na Wahadhiri wa Kiislamu Mwinjilisti Cecil Simbaulanga,  takwimu zinaonesha kwamba  makanisa yaliyoteketezwa na Waislamu tangu mwaka  1985 visiwani Zanzibar pekee ni 26,  huku Tanzania Bara yakifikia 20.

Askofu Mwasota alisema hadi  mapema wiki iliyopita wanaharakati wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar(JUMIKI) walipofanya vuruguru na kuchoma moto makanisa kisiwani Zanzibar, viongozi wa Kikristo  wamekuwa wakitoa taarifa za uhalifu dhidi ya makanisa na nyumba za wachungaji, lakini hakuna hatua zilizochukuliwa.

Katika mahojiano kwa njia ya simu na Msemakweli, Askofu Mwasota alisema kutokana na hilo, viongozi wa Kikristo waliokutana na viongozi wa SMZ katika Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) Kariakoo lililochomwa moto, alisema kimsingi viongozi hao kupitia Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Bwana Mohammed Aboud Mohammed,  waliahidi kuyalinda makanisa dhidi ya Waislamu wakorofi.

''Angalau kauli kama hiyo  imetupa moyo na kuturidhisha kwa vile haikuwepo siku za nyuma na kweli tunashuhudia  ulinzi umeimrishwa makanisani”, alisema Askofu huyo wakati akihojiwa na Msemakweli  kwa njia ya simu kutoka Zanzibar.
Alisema tayari watu 30 wamekamatwa kuhusiana na vurugu hizo.

Hata hivyo alipoulizwa  nini serikali inasema kilikuwa chanzo cha vurugu hizo, alisema bado uchunguzi unaendelea na kwamba  si vyema kukurupuka na kutaja chanzo hicho kabla ya uchunguzi makini kufanyika.

Kwa upande wake Waziri wa Mambo ya Ndani Dakta Emanuel Nchimbi aliyeshiriki katika mkutano huo, alionya kuwa suala  la amani na ulinzi  wa raia na mali zao halina mjadala na kuvitahadharisha vikundi vinavyohatarisha amani na kwamba   vitapambana na mkono wa Dola.

Mei 26 na 27 mwaka huu, vurugu kubwa zilitokea kisiwani Zanzibar  baada ya wafuasi wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara  ya Kiislamu  Zanzibar (JUMIKI), kushinikiza Jeshi la Polisi limuachie kiongozi wao Sheikh Mussa Issa ambaye alikamatwa.

Baada ya wafuasi hao kushindwa kuvamia kituo cha Polisi Madema, kufuatia Askari wa FFU kuwatawanya kwa mabomu ya machozi, waliamua kuingia mitaani na kufanya kitendo cha kushangaza cha kuharibu mali za makanisa mawili na kuyachoma  moto.

Katika kile kinachooneka kuwa  nyuma ya vurugu hizo kuna mkono wa udini na siasa, licha ya wafuasi wa JUMIKI kuchoma moto makanisa, pia walikuwa wakiwasaka watu kutoka Tanzania Bara  huku wakitamka kwamba hawautaki muungano.

Wakati kanisa la TAG lilichomwa moto Mei 27 mwaka huu, Porikia ya Kanisa Katoliki  Mpandae iliripotiwa kuchomwa moto  mchana wa Mei 28 mwaka huu na kundi la wafuasi wa JUMIKI lililokuwa likitoka katika Mahakama ya Mwanakwerekwe kusikiliza kesi ya wenzao waliokamatwa kwa kuhusika na  vurugu hizo.

Kati ya watu 30 waliokamatwa na kufikishwa mahakamani wamo  viongozi watatu wa JUMIKI akiwemo mkuu wake Sheikh Mussa Juma Issa, ambapo  wanatuhumiwa kukusanyika kinyume na sheria na kufanya fujo. Watuhumiwa hao hata hivyo wako nje kwa dhamana.

Naye Mwenyekiti wa Kundi la Biblia ni Jibu nchini Tanzania ambalo ni maarufu kwa kupigania imani ya Kikristo dhidi ya upotoshwaji unaofanywa na Wahadhiri wa Kiislamu Cecil Simbaulanga aliliambia Msemakweli kuwa vurugu za Zanzibar ni za kidini dhidi ya Ukristo.

“Ndio maana waliohusika ni  nazo ni Mashehe  wanaoeneza chuki  dhidi ya Ukristo. Haya yote nilishayaeleza  katika katika kitabu changu kinachozungumzia Mchango wa Kanisa katika miaka hamsini ya Uhuru, ambapo katika ukurasa wa 36 niliitaka serikali kuchukua hatua za kudhibiti wimbi la uchomaji makanisa”, alisema Simbaulanga.

Alisema kwa kilichotokea sasa  anaitaka serikali ya Jamhuri ya Muungano na ile ya Mapinduzi ya Zanzibar ifidie makanisa sita yaliyochomwa moto katika vurugu za  sasa kutokana na uzembe wake na kutosikiliza hoja za maana.

“Unajua haiingii akilini  kwamba  Waislamu Zanzibar ambao ni asilimia 99.9 inakuwaje walalimikie mfumo Kristo”, alisema Mwinjilisti Simbaulanga na kubainisha kuwa kinachofanyika ni mbinu tu za kusambaza chuki ili kuua Ukristo Zanzibar.

Alisema kwa hali ilivyo sasa ni lazima SMZ iache kufundisha watoto  Uislamu pekee  katika shule za msingi kama inavyofanya sasa, Kama kweli inataka haki itendeke.

Mwinjilisti Simbaulanga alilitaka Jeshi la Polisi na SMZ kutopotosha ukweli kwamba wanaofanya vurugu za uchomaji moto makanisa ni wahuni bali waeleze ukweli kwamba ni Waislamu.

“Haya mambo sisi tunajua. Tunazo DVD za wote waliopanga mambo haya kuanzia mwanzoni mwa mwaka huu,  kama ushahidi mzito na tunawajua. Tuko tayari kutoa ushahidi huo.Hawa sio wahuni ni viongozi wa wanaharakati wa Kiislamu wanaofahamika wazi”, alisisitiza Simbaulanga.
Akizungumza na Msemakweli Mwenyekiti wa Umoja wa Wainjilisti wa Kikristo nchini Tanzania (UWAKITA) Mwinjilisti Samson Bulegi ambaye pia ni Mwenyekiti wa kundi la Injili kwa Wote ambalo moja ya shughuli zake ni kusahihisha upotoshaji wa imani ya Kikristo unaofanywa na makundi ya Wahadhiri wa kiislamu, alisema vuguru za Zanzibar kwa sehemu kubwa zina mkono wa dini na siasa.

Alisema kisiasa JUMIKI na makundi mengine ya wanaharakati wa Kiislamu hayataki Muungano kwa vile Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatoa uhuru wa kuabudu ambao unakwamisha juhudi zao za kuunda dola la Kiislamu.

“Wanataka muungano uvunjike ili wapate fursa ya kueneza Uislamu  na kuua Ukristo  na ndio maana hawawataki watu wa bara,  huku pia wakichoma moto makanisa”, alisema Bulegi.

Alisema kuwa Muungano unasababisha watu kutoka Bara kuingia kwa wingi Zanzibar kuhubiri Injii na kufungua makanisa; hali inayosababisha  Waislamu wengi kuokoka na kuwa Wakristo,

 “Unajua mambo ndivyo yalivyo. Hata Makamu wa kwanza wa Rais wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Zanzibar Sheikh Maalim Seif Sharif Hamad, aliwahi  kukiri kwamba Wakristo wanabaguliwa Zanzibar.  Mimi naiomba SMZ kukomesha jambo hili kwani kila mtu ana haki ya kuishi kwa uhuru bila kubaguliwa”, alisema Bulegi.
“Bila kukomesha ubaguzi huu na unyanyasaji wa Wakristo, moto utawaka na kusambaa kila mahali na hali kuwa mbaya zaidi”, alitahadharisha Bulegi.

Sunday, 14 October 2012

UCHOMAJI MAKANISA MBAGALA

Ndugu msomaji
Shalom
Kumetokea tukio la ajabu na mbalo sasa linakuwa kawaida ka nchi yetu juu ya uchomaji makanisa, kabla jeraha la Zanzibar halijapoa makanisa mbagala matatu yamechomwa Mbagala. Sababu ikiwa ni mabishano ya watoto kwamba ukikojolea kuran atageuka Panya au paka, MTOTO (MKRISTO) naamini akisukumwa na imani akaamni kuwa hawezi kugeuka panya kwa kukojolea kuran na hivyo akaamua kuthibitisha kwa   kukojolea kuran na kama alivyoamni hakugeuka panya (MTOTO SHUJAA) Kwa sababu akawa amefichua uongo mkubwa kwamba kuran ina uwezo wa kumgeuza mtu panya wakaksirika na kutaka kujichukulia sheria mkononi wamuue lakini kakimbilia Kituo cha Polisi, kwa hasira wakakimbia kuchoma makanisa. Hatuwezi kusema nchi ina amani wakati makanisa yanaendelea kuchomwa moto, hatuwezi kusema nchi haiamni dini wakati dini fulani imekuwa ikituma mabavu kuinyanyasa dini nyingine kwa kuchoma makanisa. Kuchoma makanisa kuna athari mbaya kwa mkristo kwani sasa atashiriki ibada kwa wasi wasi na hata mazungyumzo baina ya muislamu na  mkristo yameingia dosari. Chonde kwa serikali kuhakiksha inawadhibiti hao wenye kuwa na chuki na ukristo.
IMANI THABITI ITADUMU MILELE HATA  MASINAGOGI YAKICHOMWA, TUTENDELEA KUYANENA TUNAYOYAAMINI

Hapa nimechapisha picha za matukio ya uchomaji makanisa mbagala na ziara ya Mhe. Raisi kwa mujibu wa blogu mbalimbali kama zilivyochapishwa chini ya kila habari au picha.


Mawe yametoboa vioo vingi
Katika madhabahu,pameharibiwa


Mabenchi yamepinduliwa na kuvunjwa
Mimbari imechomwa na kuharibiwa






Ofisi ya Kanisa imechomwa moto
Wachungaji wa kanisa hili wakisubiria taarifa kutoka polisi
Hawa wanafanya maombi na nimesikia wakiwaombea waislamu mungu awasamehe
Vifaa vya uimbaji vimechomwa moto
Washarika wakiwa kanisani kwao asubuhi hii
Gari la mchungaji pia limeharibiwa kabisa


RAIS JAKAYA KIKWETE ATEMBELEA MAKANISA YALIYOCHOMWA NA WAISLAM MBAGALA JIJINI DAR ES SALAAM

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia uharibifu mkubwa ulkiofanywa katika kanisa la Pentekoste la Mbagala jijini Dar es salaam wakati wa vurugu za Waislamu Ijumaa iliyopita kufuatia habari kuwa kuna mtoto amekojolea Msahafu
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akioneshwa na Katibu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Dar es salaam Bw. M Mkosimonga  uharibifu mkubwa uliofanywa kwenye kanisa hilo huko  Mbagala jijini Dar es salaam wakati wa vurugu za Waislamu Ijumaa iliyopita kufuatia habari kuwa kuna mtoto amekojolea Msahafu
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitoa pole kwa baadhi ya waumini wa  Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Dar es salaam kufuatia uharibifu mkubwa uliofanywa kwenye kanisa hilo huko  Mbagala jijini Dar es salaam wakati wa vurugu za Waislamu Ijumaa iliyopita kufuatia habari kuwa kuna mtoto amekojolea Msahafu
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akioneshwa na Mchungaji Alkwin Mbawi uharibifu mkubwa uliofanywa kwenye kanisa la Pentekoste la Mbagala jijini Dar es salaam wakati wa vurugu za Waislamu Ijumaa iliyopita kufuatia habari kuwa kuna mtoto amekojolea Msahafu
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akioneshwa na Mchungaji Alkwin Mbawi uharibifu mkubwa uliofanywa kwenye kanisa la Pentekoste la Mbagala jijini Dar es salaam wakati wa vurugu za Waislamu Ijumaa iliyopita kufuatia habari kuwa kuna mtoto amekojolea Msahafu
 
PICHA NA MUHIDIN MICHUZI