m

"If you want to conquer fear, don't sit at home and think about it. Go out and get busy. "

-- Dale Carnegie, motivational expert

Thursday, 29 August 2013

Simanzi: Askofu Moses Kulola Afariki Dunia

Ni simanzi kubwa kuwa Askofu Moses Kulola ametutoka, taarifa ambazo zimetufikia hivi punde zinasema kuwa Askofu Mkuu wa Evangelistic Assemblies God Tanzania, Moses Kulola amefariki dunia.
Kwa mujibu wa taarifa  kutoka kwa watu wa ndani wa familia hiyo, zinaeleza kuwa Askofu Kulola amefariki katika hospitali ya AMI (African Medical Investments) iliyopo Slipway jijini Dar es Salaam.

Askofu Kulola, ambaye amezaliwa mwaka 1928, amekuwa akisumbuliwa na maradhi kwa muda mrefu na hata kufikia hatua ya kupelekwa nchini India kwa matibabu.

Askofu Moses Kuloka ambaye ndiye mwanzilishi wa kanisa la EAGT na ndiye mwinjilisti mkongwe ambaye kazi i wazi kwa ukubwa wake, kwani tayari kwa takwimu zisizo rasmi sana tayari kuna makanisa ya EAGT yasiyopungua 2200. Katika uhai wake, amepata watoto wengi wa kiroho ikiwemo Dr Daniel Kulola, Mchungaji Florian Katunzi, Zakaria Kakobe, Mzee wa Upako, Maboya, Mwasota na wengineo wengi.
huduma yake ya pekee ni somo kwa akila mwamini na hapo ndipo simanzi inapotawala kwamba kazi yake bado ilihitajiwa sana hasa katika wakati huu ambapo kanisa kwa ujumla wake linayumba na imani za ajabu kuzidi kumea na kukua kwa kazi.
 mengi zaidi juu ya Mwinjilisti, mtume, nabii, mchungaji, mzee wetu na askofu wetu Moses Kulola tutazidi kutaarifiana kupitia blog hii na ukurasa wa facebook.
Angalizo: Mwenyewe hakujiita huduma hizo nilizomtaja lakini binafsi ndivyo nionavyo kuwa alikuwa mwinjilisti, mtume, nabii, mchungaji na askofu wa kweli kwa msaada wa Kristo.
Bwana ametoa na Bwana Ametwaa, Jina la Bwana Lihimidiwe.