m

"If you want to conquer fear, don't sit at home and think about it. Go out and get busy. "

-- Dale Carnegie, motivational expert

Wednesday, 3 April 2013

Kitendawili cha Kuchinja Nyama Nchini Tanzania

Kitendawili cha Kuchinja Nyama Nchini Tanzania
Ndugu Mtanzania kwa miezi kadhaa sasa kumekuwepo na mvutano mkubwa juu ya uchinjani nyama chini Tanzania, yaani nani mwenye haki ya kuchinja kati ya muislamu na mkristo. Mvutano huo umepelekea mgogoro kule Geita na sasa Tunduma.  Jambo hili limekuwa KITENDAWILI maana kinahitaji jibu na mwenye kutupa jibu hatuna hakika kama analo au la maana yupo kimya. Binafsi ninao mtazamo juu ya jambo hili na ningependa kuchangia. Kwanza ningependa kueleza ukweli usiojulikana kwa wengi yaani kwa wakristo walio wengi na pengine waislamu na wapagani pia. Nauita ukweli usiojulikana kutokana na kwamba baada ya mvutano huo kutokea nikajaribu kuhojiana na watu kadhaa juu ya jambo hili, ajabu ni kuwa walio wengi walionekana kutofahamu lolote juu ya machinjio yetu nchini, mmiliki na hata mchinjaji halali. NCHINI TANZANIA MACHINJIO HALALI KISHERIA YANAMILIKWA NA HALMASHAURI ZA MIJI NA WACHINJAJI HALALI NI WAISLAMU. Kwa upeo mdogo nilionao ni kwamba kwa muislamu mnyama aliyechinjwa na mtu asiye muislamu au pasipo swala basi nyama hiyo itakuwa kibudu(nyama haramu). Kwa mkristo ninajua jambo moja kwamba damu iliyomwagika msalabani ina nguvu ya kutakasa na zaidi wamepewa mamlaka ya kukanyaga ng’e na nyoka tena kula vitu vya kufisha na kwamba havitawafisha kabisa, tena wameambiwa wafanikiwe katika katika mambo yote na kuwa na afya njema kama roho ifanikiwavyo(Marko 16:16-18, 3Yohana 1:2).
Ninavyoelewa ni kwamba serikali yetu ina tamka wazi kuwa haina dini lakini inasisitiza kuheshimu imani kwa kila mtu. Ni jambo jema kabisa kwa serikali ambayo ina watu wa dini tofauti tena kwa makundi makubwa kujitenga na dini ili kila mtu awe huru kuabudu anachotaka. Zipo nchi nyingi za kidini (Non secular states) kama Saudi Arabia na hata Uingereza kwani yenyewe inajihusisha zaidi na kanisa lake la Anglikana. Swali langu ni kwamba serikali yetu nzuri inayotamka wazi haina dini imewezaje kutumia kigezo cha dini katika machinjio yake? Inawezaje kuamini kwamba muislamu ndiye halali kuchicha na si mkristo wakati yenyewe haina dini? Ninachofahamu ni kuwa serikali ilijitenga na dini si kuruhusu tu uhuru wa kuabudu chochote kwa watu wake bali pia kuondoa migogoro ya kidini. Mtu akijifanya kuficha tone la mafuta ndani ya maji litaelea tu! Na sasa ndo hilo linaelea baada ya kufichwa kwa miaka mingi na limekuwa kitendawili na jibu lake lahitaji mji.
Kama kitendawili hiki ningetegewa mimi ningejibu hivi; serikali haina dini na kwa kuwa machinjio ni ya serikali basi iamue pia kutokuwa na dini hata katika machinjio, yaani iajiri wachinjaji pasipo kufuata imani awe muislamu, mkristo na hata mpagani maana serikali yetu inawatambua, si wapo wabunge waioapa kwa korani wala Biblia Takatifu? Suala la dua, swala, maombi au maombezi ya nyama yabakie kwa mlaji, mlaji baada ya kununua nyama awajibike kuitakasa ili iwe halali sawa na imani yake. La sivyo serikali ijitenge na machinjio jambo ambalo ni hatari zaidi kwani ni vigumu kutenga nchi nzima machinjio ya wakristo, waislamu, wahindu, wapagani na watu wa imani nyinginezo maana zipo nyingi. Ikitenga machinjio itabidi itenge na mabucha na hapo ndo utakuwa mwanzo wa ubaguzi wa kidini.
Naishauri serikali kuchukua hatua za haraka juu ya jambo hili ili kuepuka majuto.
Huu ni mtazamo wangu, si wa dhehebu wala dini yangu.
Wako katika safari,
Mwl Peter Kapagi