
Baadhi ya watoto wa mitaani wakiwa wamelala nje kutokana na kukosa
sehemu za kulala.Baadhi yao kwa kutaka sehemu nzuri za kulala na chakula
kizuri huwa tayari kufanyiwa vitendo vibaya. Picha na Mkataba
Na Mussa Mwangoka, Mwananchi
Posted Jumatano,Decemba18 2013 saa 15:7 PM
Posted Jumatano,Decemba18 2013 saa 15:7 PM
Kwa ufupi
- Baadhi ya watoto wa mitaani wanakiri kufanyiwa unyama huo na watu mbalimbali.Vitendo hivyo hufanywa kwa siri kubwa, kutokana na ukweli kwamba watoto hao katika hali ya kujilinda wameaanzisha mkakati maalum kupambana na watu wanaolawiti na kuwabaka watoto.
Watoto kulawitiwa ili wapate hifadhi ya kulala
au kupewa chakula kizuri ni sehemu ya maisha ya baadhi ya watoto waishio
mitaani mjini Sumbawanga mkoani Rukwa.
Hii ni siri kubwa ambayo imejificha miongoni mwao,
ili uweze kupata siri hii inakulazimu lazima ujenge uhusiano wa karibu
na wa muda mrefu na watoto hao.
Watuhumiwa wakubwa wa kuwaingilia kinyume na
maumbile watoto hao ni baadhi ya walinzi wanaolinda katika maduka ya
biashara na vijana waliowazidi umri; vitendo hivyo vinaonekana kushika
kasi.
Uchunguzi wa kina uliofanywa na Mwandishi wa
makala haya kwa miezi kadhaa, umebaini kuwa vitendo vichafu
vimesababisha baadhi yao kuathirika kisaikolojia hivyo kujikuta wakiona
jambo hilo ni la kawaida na hulifurahia.
Watoto hao hufanyiwa vitendo hivyo hasa kipindi
cha masika ambapo mvua huwa zinanyesha, maeneo ambayo hupendelea kulala
nyakati hizo kwenye majumba ambayo ujenzi wake haujamalizika (Mapagala)
huwa yanavuja maji ya mvua hivyo hulazimika kuyazikimbia kujisalimisha
popote.
Watoto wa mitaani
Baadhi ya watoto wa mitaani waliozungumza na
mwandishi walikiri kwamba ni kweli kuna tabia hiyo lakini ni kwa usiri
mkubwa kwani iwapo itabainika mtu anamlawiti mtoto mwenzao huwa
wanapambana naye.
“Unajua sisi tunawasaidia walinzi katika malindo
yao nyakati za usiku, tulishakubaliana kama kuna mwenzetu analawitiwa na
anakubali tutamtenga.
Wapo watoto wawili tayari tumewatenga katika kundi
letu kwa tabia ya kupenda kulawitiwa, sasa kama wapo wengine
tukiwafahamu nao tunawatenga hata wakipata matatizo hatuwezi kuwasaidia”
mtoto mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Jose (siyo jina lake halisi).
Naye mtoto aitwaye Juma anasema kuwa
kinachowaponza watoto wengine ni tamaa na sio hifadhi ya kulala pekee
kwani wapo watoto ambao wamezitoroka familia zao kwa kisingizio cha
ugumu wa maisha na kukimbilia mitaani kufanya kazi ya kuombaomba ambapo
wamekuwa wakidanganyika kwa vyakula kama Chips na pombe katika baa za
usiku.
“Sisi wengine tupo huku mitaani kwa sababu
mbalimbali zikiwemo za kipato duni cha familia zetu, malezi mabaya kama
vile kulelewa na kina mama wa kambo ambao ni chanzo matatizo kwa sehemu
kubwa lakini sio sababu ya kukubali kulawitiwa.
Ila wapo wale wanaopenda pombe na chips ndio
wanajikuta wakishawishiwa na sio tu na walinzi lakini pia hata baadhi ya
watu ambao hutumia kisingizio cha ulevi wa pombe ili kufanya vitendo
hivyo,” anasema mtoto Maiko (siyo jina lake halisi).
Bofya hapa kwa habari zaidi http://www.mwananchi.co.tz/habari/habari-ya-ndani/Watoto-wa-mitaani-wanavyobakwa-Sumbawanga/-/1724700/2117114/-/s0l8dj/-/index.html
Bofya hapa kwa habari zaidi http://www.mwananchi.co.tz/habari/habari-ya-ndani/Watoto-wa-mitaani-wanavyobakwa-Sumbawanga/-/1724700/2117114/-/s0l8dj/-/index.html
No comments:
Post a Comment