Bwana asifiwe.
Wapendwa, kwanza nawashukuru tena kwa namna mlivyoshiriki kwa ajili ya ufanikisha ibada na kikao cha leo Uyole Sekondari.
Ninayo
furaha kuwataarifu Ex CASFETA wa Uyole Sekondari maarufu kama CASFETA
UYOLE VETERANS(CUV) kuwa kama tulivyopanga tumekutana leo na kushiriki ibada kuanzia saa 12:30-14:20 na pia tukamekaa kikao na kidato cha nne na viongozi wa tawi .
Kikao cha CUV kimeudhuriwa na wanachama wauatao;
1. Upendo Malle
2. Martha
3. Peter Kapagi
4. Elly Mangula
5. Abner Zephania
6. Ikupa Mwakaje
7. Sunny Michael
Waliotoa udhuru ni;
1. Edmund Mbwaga
2. Xaveria Jonas
Waliopo vyuoni na kutoa udhuru
3. Emmanuel Nasson
4. Catherene Vicent
5. Tulipo Asangalwisye
6. Shadrack Mwakyusa.
MAAZIMIO
tumekubaliana kuwa;
CUV kiwe chombo muhimu kutukutanisha wanaCASFETA wote tuliwahi kusoma shule ya sekondari Uyole na ambacho kitatusaidia kutuunganisha ili kuhudumiana katika mambo mbalimbali ya kiroho na kijamii na matukio muhimu katika maisha kama
-Masuala ya harusi
- ushauri katika masuala ya kiroho na kutiana nguvu kwa habari ya safari ya mbinguni.
-Kusadiana katika masuala ya kielimu kwa kuwa ni chombo kwa ajili ya yeyote aliyemaliza Uyole pasipo kujali kiwango cha elimu, kazi n.k
- kushauriana katika masuala ya kiuchumi yaani kazi, biashara na hata ujasiriamali
-Ni vema kila mwanaCUV akawa mjasiriamali endapo atakuwa ameajiriwa kazi katika sekta yoyote ili awe na uchumi safi kwa ajili ya familia yake na kanisa.
- Kila mwanaCASFETA aliyemaliza Uyole lazma athibitishe anakuwa nguzo muhimu katika kanisa lake yaani atumike vizuri.
-CUV itakuwa sehemu muhimu kabisa ya kufanikisha mahafali ya kila mwaka ya CASFETA Uyole sekondari ili yawe mahaali bora kabisa na yenye nguvu.
Mambo ya kutekeleza
-Bwana atufanikishe kuwa watekelezaji wa maazimio ya chama
-Tutafute mawasiliano ya wanaCASFETA wenye sifa za kuwa CUV ili tuweze kuwtumia taarifa muhimu na kwa ajili ya mkutano mwingine tutakaopanga hapo baadaye.
mawasiliano yawe namba za simu, email n.k na yatumwe kwa
Abner Zephania- 0765 316393
au tumia blog hii au email kakakapagi@gmail.com
Mwisho ni kuendelea kulea tawi letu la Uyole kila tupatapo nafasi na Bwana atatubariki.