Shujaa Ariel Sharon enzi za uhai wake akiwa waziri Mkuu alipohudhuria kikao cha ulinzi Pentagon, Washington

Watu wakitoa heshima mbele ya mwili wa Ariel Sharon na Mwili wa Sharon ukiwa umebebwa na majenerali


Wageni waliofika kwa ibada maalum ya Sharon walimsifu kama kiongozi aliyepigania waisraeli
Aliekuwa waziri mkuu wa Isreal ,
Ariel Sharon amezikwa kwa heshima za kijeshi katika shamba la familia
yake kusini mwa Israel. Kundi la majenerali ndio walibeba jeneza lake.
Ulinzi uliimarishwa wakati waombolezaji
walipokuwa wanafika katika shamba hilo ambalo liko karibu na mpaka wa
eneo Gaza la waPalestina linalokaliwa na Israel.Rais Shimon Peres amemtaja Bw Sharon kama mwanajeshi shupavu aliyejua kushinda vita.
Awali ibada maalum ilifanyika nje ya majengo ya bunge la Israel.
Bwana Sharon atakumbukwa kwa kuwa miongoni mwa waanzilishi wa taifa la Israel lakini pia alikuwa mwanajeshi na mwanasiasa jasiri aliyechukiwa na wapalestina wengi.
Waliohutubia umati,wamemtaja Sharon kama mtu aliyejitolea kuhakikisha kuna usalama kwa watu wake.
Waziri mkuu Benjamin Netanyahu alisema kuwa Sharon alikuwa mmoja wa makamanda wakuu wa wayahudi na ambaye atakumbukwa zaidi ya wote.
Licha ya sifa hizo Bwana Sharon anachukiwa sana na waarabu hasa wapalestina kwa dhuluma alizowatendea chini ya utawala wake.
Kiongozi huyo aliaga dunia siku ya Jumamaosi akiwa na umri wa miaka 85 baada ya kuwa hali mahututi kwa takriban miaka minane.
Atazikwa baadaye leo katika shamba la familia yake jangwani Negev.
Maelfu ya waombolezaji walitoa heshima zao za mwisho kwa Sharon siku ya Jumapili wakati ambapo mwili wake ulikuwa umelazwa nje ya majengo ya bunge mjini Jerusalem.