m

"If you want to conquer fear, don't sit at home and think about it. Go out and get busy. "

-- Dale Carnegie, motivational expert

Tuesday, 24 September 2013

Ni somo kwetu, Vigogo wa siasa wawajibika Ujerumani

Wiki iliyopita nilishiriki ujumbe mmoja wa ukurasa wa facebook wa DW ambapo nichapisha kuwa Afrika tunaweza kujifunza siasa kutoka Ujerumani, taifa ambalo wakati wa uchaguzi watu huangalia utaifa zaidi ni kuwa watulivu wakati na baada ya kupiga kura. Hatimaye matokeo yametangazwa na mwanamke shupavu Kansela Angela Markel kuibuka mshindi na chama chake.Matokeo hayo yamepelekea chama cha FDP na uongozi wake kujiuzulu. Hii ni tofauti na hapa Afrika kwani baada ya matokeo wangeingia mtaani na kuzusha vurugu kubwa kupinga matokeo hata kama wameshindwa kihalali. Nikienda mbali zaidi ni kwamba kansela Angela markel pamoja kupata ushindi mzito bado karuhusu mazungumzo na upinzani kuunda serikali ya pamoja. Lengo lao wanasiasa wa Ujerumani ni kuona Ujerumani imara na kuonda maendeleo ya Taifa lao na si matumbo yao, familia na hata maswahiba wao kama ilivyo kwetu Afrika.
Habari zaidi fuatana na DW.DE hapa wanaripoti;
Siasa zimechemsha Ujerumani ambapo viongozi wa vyama mashuhuri vya kisiasa wa chama cha Free Demoktatik FDP wamejiuzulu na uongozi mzima wa chama cha Kijani kujizulu baada ya kushindwa vibaya katika uchaguzi.
Rainer Brüderle akiwa na Philipp Rösler. Rainer Brüderle akiwa na Philipp Rösler.
Kiongozi wa chama cha FDP Phillip Rösler ametangaza kujiuzulu hapo Jumatatu baada ya chama chake kushindwa vibaya kuwahi kushuhudiwa kabla katika uchaguzi wa Ujerumani uliofanyika Jumapili na kusababisha kuenguliwa kwa chama hicho katika bunge la Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani.
Rösler Naibu Kansela anayemaliza muda wake ambaye amejiuzulu kama kiongozi wa chama hicho chenye kupendelea wafanya biashara na waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Guido Westerwelle ni miongoni mwa mawaziri waliopoteza viti vyao katika uchaguzi huo ambapo chama chao kimeboronga vibaya.
Rösler mwenye umri wa miaka 40 ambaye alikuwa pia waziri wa uchumi katika serikali ya Merkel amesema wakati akijiuzulu kwamba huko ni kushindwa vibaya kabisa kwa chama hicho kuwahi kushuhudiwa katika historia.http://www.dw.de/vigogo-wa-siasa-wawajibika-ujerumani/a-17109452