m

"If you want to conquer fear, don't sit at home and think about it. Go out and get busy. "

-- Dale Carnegie, motivational expert

Tuesday, 16 October 2012

TAKWIMU ZA UCHOMAJI MAKANISA TANZANIA NA TAMKO LA TAG

TAKWIMU ZAONYESHA TANGU MWAKA 1985-2012 MAKANISA 46 YAMECHOMWA ,KUBOMOLEWA NCHINI


Askofu David Mwasota.

             
Imeelezwa  kuwa tangu kuibuka kwa wimbi la uchomaji wa  makanisa linalofanywa na watu wanaoaminika kuwa wanaharakati wa  Kiislamu katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limeyakumba zaidi ya makanisa 46.

Hayo yameelezwa na Katibu Mkuu wa  Baraza la Maaskofu wa Kipentekoste nchini Tanzania (PCT) Askofu David Mwasota wakati akizungumza na Gazeti Msemakweli akiwa Kisiwani Zanzibar.

Kiongozi huyo  alikuwa mmoja wa wajumbe  wa mkutano uliowakutanisha viongozi wa dini ya Kikristo, viongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ)na makamanda wakuu wa jeshi la Polisi ambapo ulijadili kwa kina juu ya vurugu zilizotokea visiwani Zanzibar.

Kwa mujibu ya Mwenyejiti wa kundi linaloendesha mihadhara ya Kikristo inayosahihisha upotoshwaji wa Maandiko Matakatifu ya Biblia unaofanywa na Wahadhiri wa Kiislamu Mwinjilisti Cecil Simbaulanga,  takwimu zinaonesha kwamba  makanisa yaliyoteketezwa na Waislamu tangu mwaka  1985 visiwani Zanzibar pekee ni 26,  huku Tanzania Bara yakifikia 20.

Askofu Mwasota alisema hadi  mapema wiki iliyopita wanaharakati wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar(JUMIKI) walipofanya vuruguru na kuchoma moto makanisa kisiwani Zanzibar, viongozi wa Kikristo  wamekuwa wakitoa taarifa za uhalifu dhidi ya makanisa na nyumba za wachungaji, lakini hakuna hatua zilizochukuliwa.

Katika mahojiano kwa njia ya simu na Msemakweli, Askofu Mwasota alisema kutokana na hilo, viongozi wa Kikristo waliokutana na viongozi wa SMZ katika Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) Kariakoo lililochomwa moto, alisema kimsingi viongozi hao kupitia Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Bwana Mohammed Aboud Mohammed,  waliahidi kuyalinda makanisa dhidi ya Waislamu wakorofi.

''Angalau kauli kama hiyo  imetupa moyo na kuturidhisha kwa vile haikuwepo siku za nyuma na kweli tunashuhudia  ulinzi umeimrishwa makanisani”, alisema Askofu huyo wakati akihojiwa na Msemakweli  kwa njia ya simu kutoka Zanzibar.
Alisema tayari watu 30 wamekamatwa kuhusiana na vurugu hizo.

Hata hivyo alipoulizwa  nini serikali inasema kilikuwa chanzo cha vurugu hizo, alisema bado uchunguzi unaendelea na kwamba  si vyema kukurupuka na kutaja chanzo hicho kabla ya uchunguzi makini kufanyika.

Kwa upande wake Waziri wa Mambo ya Ndani Dakta Emanuel Nchimbi aliyeshiriki katika mkutano huo, alionya kuwa suala  la amani na ulinzi  wa raia na mali zao halina mjadala na kuvitahadharisha vikundi vinavyohatarisha amani na kwamba   vitapambana na mkono wa Dola.

Mei 26 na 27 mwaka huu, vurugu kubwa zilitokea kisiwani Zanzibar  baada ya wafuasi wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara  ya Kiislamu  Zanzibar (JUMIKI), kushinikiza Jeshi la Polisi limuachie kiongozi wao Sheikh Mussa Issa ambaye alikamatwa.

Baada ya wafuasi hao kushindwa kuvamia kituo cha Polisi Madema, kufuatia Askari wa FFU kuwatawanya kwa mabomu ya machozi, waliamua kuingia mitaani na kufanya kitendo cha kushangaza cha kuharibu mali za makanisa mawili na kuyachoma  moto.

Katika kile kinachooneka kuwa  nyuma ya vurugu hizo kuna mkono wa udini na siasa, licha ya wafuasi wa JUMIKI kuchoma moto makanisa, pia walikuwa wakiwasaka watu kutoka Tanzania Bara  huku wakitamka kwamba hawautaki muungano.

Wakati kanisa la TAG lilichomwa moto Mei 27 mwaka huu, Porikia ya Kanisa Katoliki  Mpandae iliripotiwa kuchomwa moto  mchana wa Mei 28 mwaka huu na kundi la wafuasi wa JUMIKI lililokuwa likitoka katika Mahakama ya Mwanakwerekwe kusikiliza kesi ya wenzao waliokamatwa kwa kuhusika na  vurugu hizo.

Kati ya watu 30 waliokamatwa na kufikishwa mahakamani wamo  viongozi watatu wa JUMIKI akiwemo mkuu wake Sheikh Mussa Juma Issa, ambapo  wanatuhumiwa kukusanyika kinyume na sheria na kufanya fujo. Watuhumiwa hao hata hivyo wako nje kwa dhamana.

Naye Mwenyekiti wa Kundi la Biblia ni Jibu nchini Tanzania ambalo ni maarufu kwa kupigania imani ya Kikristo dhidi ya upotoshwaji unaofanywa na Wahadhiri wa Kiislamu Cecil Simbaulanga aliliambia Msemakweli kuwa vurugu za Zanzibar ni za kidini dhidi ya Ukristo.

“Ndio maana waliohusika ni  nazo ni Mashehe  wanaoeneza chuki  dhidi ya Ukristo. Haya yote nilishayaeleza  katika katika kitabu changu kinachozungumzia Mchango wa Kanisa katika miaka hamsini ya Uhuru, ambapo katika ukurasa wa 36 niliitaka serikali kuchukua hatua za kudhibiti wimbi la uchomaji makanisa”, alisema Simbaulanga.

Alisema kwa kilichotokea sasa  anaitaka serikali ya Jamhuri ya Muungano na ile ya Mapinduzi ya Zanzibar ifidie makanisa sita yaliyochomwa moto katika vurugu za  sasa kutokana na uzembe wake na kutosikiliza hoja za maana.

“Unajua haiingii akilini  kwamba  Waislamu Zanzibar ambao ni asilimia 99.9 inakuwaje walalimikie mfumo Kristo”, alisema Mwinjilisti Simbaulanga na kubainisha kuwa kinachofanyika ni mbinu tu za kusambaza chuki ili kuua Ukristo Zanzibar.

Alisema kwa hali ilivyo sasa ni lazima SMZ iache kufundisha watoto  Uislamu pekee  katika shule za msingi kama inavyofanya sasa, Kama kweli inataka haki itendeke.

Mwinjilisti Simbaulanga alilitaka Jeshi la Polisi na SMZ kutopotosha ukweli kwamba wanaofanya vurugu za uchomaji moto makanisa ni wahuni bali waeleze ukweli kwamba ni Waislamu.

“Haya mambo sisi tunajua. Tunazo DVD za wote waliopanga mambo haya kuanzia mwanzoni mwa mwaka huu,  kama ushahidi mzito na tunawajua. Tuko tayari kutoa ushahidi huo.Hawa sio wahuni ni viongozi wa wanaharakati wa Kiislamu wanaofahamika wazi”, alisisitiza Simbaulanga.
Akizungumza na Msemakweli Mwenyekiti wa Umoja wa Wainjilisti wa Kikristo nchini Tanzania (UWAKITA) Mwinjilisti Samson Bulegi ambaye pia ni Mwenyekiti wa kundi la Injili kwa Wote ambalo moja ya shughuli zake ni kusahihisha upotoshaji wa imani ya Kikristo unaofanywa na makundi ya Wahadhiri wa kiislamu, alisema vuguru za Zanzibar kwa sehemu kubwa zina mkono wa dini na siasa.

Alisema kisiasa JUMIKI na makundi mengine ya wanaharakati wa Kiislamu hayataki Muungano kwa vile Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatoa uhuru wa kuabudu ambao unakwamisha juhudi zao za kuunda dola la Kiislamu.

“Wanataka muungano uvunjike ili wapate fursa ya kueneza Uislamu  na kuua Ukristo  na ndio maana hawawataki watu wa bara,  huku pia wakichoma moto makanisa”, alisema Bulegi.

Alisema kuwa Muungano unasababisha watu kutoka Bara kuingia kwa wingi Zanzibar kuhubiri Injii na kufungua makanisa; hali inayosababisha  Waislamu wengi kuokoka na kuwa Wakristo,

 “Unajua mambo ndivyo yalivyo. Hata Makamu wa kwanza wa Rais wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Zanzibar Sheikh Maalim Seif Sharif Hamad, aliwahi  kukiri kwamba Wakristo wanabaguliwa Zanzibar.  Mimi naiomba SMZ kukomesha jambo hili kwani kila mtu ana haki ya kuishi kwa uhuru bila kubaguliwa”, alisema Bulegi.
“Bila kukomesha ubaguzi huu na unyanyasaji wa Wakristo, moto utawaka na kusambaa kila mahali na hali kuwa mbaya zaidi”, alitahadharisha Bulegi.