m

"If you want to conquer fear, don't sit at home and think about it. Go out and get busy. "

-- Dale Carnegie, motivational expert

Sunday, 22 September 2013

DINI NA SIASA

Dini kujihusisha na siasa si jambo baya, ni jema sana hasa ikizingatiwa watu waadilifu walio wengi
wanapatikana kwenye dini maana na kazi ya dini ni kufundisha uvumilivu, uaminifu, upendo na heshima kwa Mungu na jamii nzima.
Lakini nikumbushe kuwa katika taasisi moja ya dini ni lazima kutakuwa na makundi tofauti na yenye itikadi na mtazamo tofauti za Kisiasa. Siasa si maandiko ambayo huwalazimisha watu wote wawe na msimamo mmoja juu ya andiko hilo.
Nasema hivi ili kuwaasa baadhi ya viongozi wa dini kulivaa vazi la siasa mwili mzima. Binafsi naamini kiongozi wa dini kazi yao ni Kutoa elimu ya siasa na hata uraia, hapo wafundishe siasa safi, sifa za kiongozi bora na habari ya sera. SI KAZI YA KIONGOZI YEYOTE WA DINI KUWAELEKEZA WATU WAKE KUPENDA AU KUCHUKIA CHAMA FULANI, SI KAZI YA KIONGOZI WA DINI KUWACHOCHEA WATU KUJIUNGA NA CHAMA FULANI CHA SIASA, KAZI YAKE INAISHIA KUWAELEKEZA SIFA ZA SIASA SAFI HALAFU WATU WANAAMUA CHAMA KIPI NI KISAFI.
Nimeshtushwa kwa mara nyingine kushuhudia tena baba yangu na askofu mkubwa kabisa kuchochea watu kuchukia chama fulani, Askofu Kakobe kushiriki kwake katika muungano wa viongozi wa upinzani na kutoa matamshi ya chuki juu CCM pale jangwani, hakika si kazi yake hata kidogo. Watu watakapoyapuuza maneno yake inaweza kuathiri hata juu ya mafundisho yake kwani watu wakizoea kukupuuza katika jambo fulani watakupuuza katika mengine na hapo kutakuwa na athari kubwa ya IMANI. naomba nimkumbushe Askofu juu ya matamko yake 1995 na NCCR, hakuishia hapo akatoa matamko 2000, 2005 na 2010 mara zote matamko yake yameenda kinyume na uhalisia.
Baba askofu kakobe anataka wafuasi wake mimi nikiwa miongozi mwao waamini chama gani cha siasa? NCCR, CHADEMA, CUF, CCM AU CHAMA GANI? Askofu anatuchanganya na matamko yake ya kisiasa. Namshauri kutoa elimu ya siasa na si kuwa mwanaharakati.
Binafsi nimekuwa kiongozi wa dini kanisani na hata kwa wanafunzi hadi ngazi ya chuo kikuu (CASFETA-TAYOMI) lakini sijawahi na siamini kabisa juu ya kuwachochea waumini juu ya chama fulani cha siasa, isipokuwa ninachofanya ni kuwachochea waumini kushiriki siasa safi na habari ya vyama huwaachia waumini uhuru wa kuchagua ni chama gani safi kwa mujibu wa mwongozo wa siasa safi niwapao.