m

"If you want to conquer fear, don't sit at home and think about it. Go out and get busy. "

-- Dale Carnegie, motivational expert

Saturday, 22 March 2014

UNABII WA TANZANIA KATIKA BIBLIA



Bwana Yesu asifiwe…
Mpendwa leo ninayo furaha kubwa sana kurejea tena ukurasa wetu na kichwa hapo juu.
JE WAJUA KUWA NCHI YETU TANZANIA IMETAJWA KATIKA BIBLIA TAKATIFU?
ISAYA 18:
 Mst 1. Ole wa nchi ya uvumi wa mabawa, Iliyoko mbali kupita mito ya Kushi;
2  Ipelekayo wajumbe wake kwa njia ya bahari, Na katika vyombo vya manyasi juu ya maji.
Nendeni wajumbe wepesi, kwa watu warefu laini, watu watishao tangu mwanzo wao hata sasa; Taifa la wenye nguvu wakanyagao watu, ambao mito inakata nchi yao.
3  Enyi watu mkaao katika ulimwengu wote, na wenyeji wa dunia, bendera ikiinuliwa milimani, angalieni; na wakipiga tarumbeta, sikieni.
4  Maana Bwana ameniambia hivi, Mimi nitatulia, na kuangalia katika makazi yangu, kama wakati wa mwangaza mweupe wa jua kali, mfano wa wingu la umande katika hari ya mavuno.
5  Maana kabla ya mavuno, maua yaangukapo, na maua yakawa zabibu zianzazo kuiva, ndipo atakapoyakata matawi kwa miundu, na kuviondoa vitawi vilivyopanuka na kuvikata.
6  Wote pamoja wataachiwa ndege wakali wa milimani, na hayawani wa nchi; ndege wakali watakaa juu yao wakati wa jua, na hayawani wote wa nchi watakaa juu yao wakati wa baridi.
7  Wakati huo Bwana wa majeshi ataletewa hedaya na watu warefu, laini; Watu watishao tangu mwanzo wao hata sasa; Taifa la wenye nguvu, wakanyagao watu, Ambao mito inakata nchi yao;

Mpendwa nilistaajabu mwaka 2011 nilipokutana na Mwl. Brown Mwakibete pale Kijitonyama, kwa kujiamini sana akanidokeza kwamba Tanzania imetajwa kwenye Biblia, imetabiriwa na nabii Isaya. Nami kwa nilivyokuwa namwamini nikaungana naye kutafakari kifungu hicho mara tu aliponitaka nifungue Biblia yangu.

Ndugu yangu ukitazama mstari wa kwanza wa Isaya 18 utaona unataja nchi ya uvumi iliyoko mbali kupita mito ya kushi. Katika Biblia Kushi ni nchi ya Ethiopia ya leo, ukitazama ramani utabaini kuwa nchi zilizo mbali na mito ya Ethiopia ni nchi za Afrika Mashariki na Somalia kidogo. (ukitokea kaskazini ambako ndio inapatikana Israel) TANZANIA ni mojawapo ya nchi hizo.

Mstari wa 2 unataja kuwa nchi hiyo inapeleka wajumbe wake kwa njia ya habari na katika vyombo vya mnyasi. Hapo utabaini kuwa nchi zinazopakana na bahari na kutumia ngalawa ni Kenya, TANZANIA na Somalia.

Sehemu ya pili inazungumzia watu wepesi lani watishao tangu mwanzo wao hata sasa. Hapa utaona kuna mkanganyiko kidogo kwa watu laini tunaweza tafsiri kuwa watu wapole wasio na makuu lakini wakati huohuo watu hao wanatisha tangu mwanzo. TANZANIA ndio nchi inayoongoza Afrika kwa ukarimu (hospitality) lakini pia ndio nchi pekee Afrika iliyoongoza mapambano dhini ya wakoloni kwa nchi zote za kusini mwa jangwa la Sahara, iliwatisha wakoloni ikiwa ina ujinga, maradhi na umaskini wakati wao wana silaha, elimu, utajiri na afya njema. TANZANIA ndio nchi pekee Afrika iliyopigana na nchi nyingine na kuishinda iliipiga Uganda ikakanyaga watu wao hadi kaskazini ikamng’oa Dikteta Idd Amini na kisha kuweka mtawala wao. Kabla ya Amiri Jeshi Mkuu kuruhusu vita alianza kwa kuwatisha waganda na dunia nzima. TANZANIA inatisha kwani wakati huo pia Malawi walitaka kunyang’anya ziwa Nyasa na Kenya wakaumendea mila Kilimanjaro lakini Nyerere akawatisha wakashindwa. Tanzania. Hakuna aisyeijua TANZANIA katika kusuluhisha migogoro, mfano Mauaji ya Kimbari ya Rwanda, Imedhibiti uasi visiwa vya Comorro, imetatua mgogoro wa Kenya 2007 na hatimaye madagascar

Mstari unaomaliza kwa kutaja kuwa mito inakata nchi yao, Afrika Mashariki ni TANZANIA pekee mbayo mito mikubwa inapita katikati, hebu tazama Mito mikubwa ya Ruaha, Pangani, Malagarasi, Ugalla, Rufiji, Wami  bila kusahau mito ya mipakani ambayo ni pamoja na Kagera, Mara, Ruvuma na Songwe. Bila shaka yeyote nchi inayozungumziwa hapa ni TANZANIA kwani Kenya na Somalia hazina mito mikubwa.

Mst wa 3 unazaungumzia kuinuliwa bendera mlimani na kupiga tarumbeta. Tanzania ndio nchi pekee barani Afrika ambayo ilipandisha bendera yake ju ya mlima Kilimanjaro. Na ikapiga tarumbeta kwani baada tu ya uhuru wa Tanzania ndipo nchi nyingi zikafuatia miaka ya 1962 na 1963 zikiwemo Uganda, Kenya na makoloni mengi ya kifaransa. Yote ni kwa kuwa nchi ya Tanzania ilisimama kidete kwa ajili ya ukombozi wa waafrika.

Mst 7 unazungumzia kwamba watu hao warefu laini watamletea Hedaya Bwana wa majeshi, tena unasisitiza kabisa Taifa la wenye nguvu, wakanyagao watu, amabo mito inakata nchi yao.
Ni nchi gani hiyo zaidi ya TANZANIA?

Huwezi kuombea vema kitu usichokujua, natamani unabii huu ukupe nguvu ya kuiombea nchi yetu TANZANIA.

Mpendwa leo nimedokeza kidogo tu unabii wan chi yetu TANZANIA kama ulivyotolewa na nabii Isaya. Nitafurahi kama utakuwa mwanzo tu wa mjadala juu ya nchi yetu katika ulimwengu war oho, wengine husema Tanzania ndiyo Israeli ya Afrika, je ni kweli? Kuna hoja gani?

Kama una masomo au hoja yoyote juu ya Tanzania yetu katika ulimwengu wa roho usisite kuwasilisha kupitia mawasiliano yafuatayo;
Simu: +255 685 306666, +255 764 734620

MUNGU IBARIKI TANZANIA

Wenu katika safari
Mwl Peter Kajolo Kapagi