
Inawezekana usielewe maana ya kichwa hapo juu lakini ukitazama darasa hili utabaini kuwa BRN utani. Big Results Now (BRN) nafikiri ni utani tu ulioanzishwa....ni utani kwani huwezi kuleta big results kwa mwezi mmoja tu, huwezi kuzungumzia big results bila kutaja tatizo la msingi la walimu. Hata kama itakuwa na matokeo mazuri lakini tafsiri ya BRN ni kuona matokeo mazuri na si elimu bora, inataka kuona matokeo ambayo hayataleta maandamano ya kupinga matokeo. Kuna matizo mengi katika mfumo wa elimu lakini hayapewi nafasi ya kujadiliwa na hata yakijadiliwa makaratasi hutupwa jalalani.