
Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa akiandaa nyaraka za ushahidi
dhidi ya viongozi waliofukuzwa kwenye chama hicho juzi, kabla ya
kuzungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana. Kulia ni
Mwanasheria wa Chadema, Tundu Lissu. Picha na Fidelis Felix
Na Fidelis Butahe na George Njogopa, Mwananchi
Posted Jumatatu,Januari6 2014 saa 8:9 AM
Posted Jumatatu,Januari6 2014 saa 8:9 AM
Kwa ufupi
- Yasema waraka wao wa mabadiliko ulikuwa na nia ya kukimaliza chama na viongozi wake wa juu
Dar es Salaam. Kamati Kuu ya
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) imewafukuza uanachama,
aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho, Mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba na
aliyekuwa Mjumbe wa Kamati Kuu, Dk Kitila Mkumbo.
“Tumewavua uanachama kutokana na makosa ya kuandaa
waraka wa Mkakati wa Mabadiliko 2013,” alisema Katibu Mkuu wa Chadema,
Dk Willibrod Slaa mbele ya waandishi wa habari.
Wakati hayo yakifanyika, imeelezwa kuwa aliyekuwa
Naibu Katibu Mkuu wake, Zitto Kabwe ataendelea na uanachama na ubunge
kwa sababu ya mahakama, siyo kwa matakwa ya chama hicho.
Zitto ambaye alitajwa kuwa mhusika mkuu katika
waraka huo amefungua kesi akiomba Mahakama Kuu izuie uanachama wake
kujadiliwa hadi rufani yake itakaposikilizwa na Baraza Kuu la chama.
Hatima ya maombi hayo itajulikana leo.
Maamuzi ya kikao
Akitangaza uamuzi wa kikao cha dharura cha Kamati
Kuu kilichokutana kwa siku mbili jijini Dar es Salaam jana, Dk Slaa
alisema, “Kuhusu Zitto Kamati Kuu haikujadili wala kuamua juu ya
mashtaka dhidi yake.”
Huku akiyataja makosa 11 ya Zitto, Mwigamba na Dk
Kitila yaliyotokana na waraka huo, Dk Slaa alisema, “Baada ya kumhoji Dk
Mkumbo alikiri wazi kuwa Zitto alikuwa akiujua waraka huu ambao
ulilenga kukiuka chama, kutengeneza tuhuma dhidi yangu na Mwenyekiti wa
Chadema, Freeman Mbowe.”
Katika mkutano huo Mwanasheria Mkuu wa chama
hicho, Tundu Lissu alisema Zitto ataendelea kuwa mwanachama wa Chadema
na mbunge kwa sababu ya mahakama na siyo matakwa ya Chadema.
Zitto ambaye ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini,
Mwigamba na Dk Kitila, Novemba 22 mwaka jana walivuliwa nyadhifa zao na
Kamati Kuu baada ya kukamatwa kwa waraka huo.
Waraka huo ulioandaliwa na Mwigamba na Dk Kitila,
uliolenga kufanya mabadiliko makubwa ya kiuongozi wakati wa uchaguzi
mkuu wa ndani wa chama hicho, huku Zitto akipendekezwa kuwania nafasi ya
uenyekiti.
Utetezi wa watuhumiwa
Katika ufafanuzi wake kuhusu utetezi wa
watuhumiwa, Dk Slaa alisema, “Dk Kitila pekee, ndiye alikuja kuhojiwa na
Kamati Kuu iliyokutana Januari 3 hadi 4 na kwamba alikubali kuandaa
waraka lakini alikataa kwa kuwa ulikiuka katiba na kanuni za chama. Pia
alikataa kumtaja kwa jina mwandishi mwingine wa waraka huo anayetajwa
kwa jina la M2.”
Soma zaidi http://www.mwananchi.co.tz/habari/Siasa/Chadema-yawatimua-Dk-Kitila--Mwigamba/-/1597332/2135732/-/k2po63/-/index.html
Soma zaidi http://www.mwananchi.co.tz/habari/Siasa/Chadema-yawatimua-Dk-Kitila--Mwigamba/-/1597332/2135732/-/k2po63/-/index.html