
Kutokana na Tanzania kufuata utaratibu wa maadili (moral) katika utawala
wake, inaweza kuwa chanzo cha ugumu wa utekelezaji wake.
Hukumu ya Kifo hutolewa chini ya Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai
(Criminal Procedure Act. 1985) ambayo inasisitiza kuwa utekelezaji wa
hukumu hiyo ni muhukumiwa kunyongwa na siyo vinginevyo.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema
Na Kelvin Matandiko, Mwananchi
Rais, ndiyo ataamua kusaini ama kutosaini, huwa kuna mambo mengi yanayoangaliwa
Wadhifa wa Urais wa Tanzania umeendelea kujikuta
njia panda kila unapofika wakati wa kuidhinisha kutekelezwa kwa adhabu
ya kifo kwa waliohukumiwa kunyongwa hadi kufa na mahakama, na suala hilo
limekuwa gumu kutekelezwa katika awamu zote nne za uongozi.
Hukumu hiyo ni kama haitekelezeki na pengine
mafaili yaliyobeba uamuzi wa mahakama wenye adhabu za vifo, yameendelea
kusubiri kusainiwa tangu enzi za uongozi wa awamu ya kwanza wa Hayati
Mwalimu Julius Nyerere na hata sasa Rais Jakaya Kikwete.
Watangulizi wengine wa Rais Kikwete ni Mzee Ali
Hassan Mwinyi aliyeongoza Serikali ya Awamu ya Pili na Mzee Benjamin
Mkapa, aliyeongoza Serikali ya Awamu ya Tatu. Wote wanatajwa kwamba
walikuwa wazito kuidhinisha utekelezaji wa hukumu hiyo ya kuondoa uhai
wa mtu.
soma zaidi kwa kubofya http://www.mwananchi.co.tz/Makala/Mamia-wanasubiri-kunyongwa-nchini/-/1597592/2127326/-/aiaaly/-/index.html
soma zaidi kwa kubofya http://www.mwananchi.co.tz/Makala/Mamia-wanasubiri-kunyongwa-nchini/-/1597592/2127326/-/aiaaly/-/index.html