Watu wengi wamekuwa na wasiwasi na matumizi y afaceboo na wengine wakijisahau kabisa wanapotumia faceboo. Baada ya maswali mengi juu ya facebook zifuatazo ni Dondoo Muhimu:
1. Facebook ipo kwa uwazi (Transparency) hivyo kila ulifanyalo hubaki kuwa wazi zaidi kwa marafiki na hata jamii.
2. Chukua maamuzi sahihi kujiunga na facebook ukiwa na tahadhari na ufahamu kidogo juu ya facebook.
Maisha ya facebook huonesha uhalisia wa mtu tofauti na wengi ambao hufikiri maisha ya facebook ni mengine mbali na maisha ya halisi. Kumbuka Jmabo utakalolifanya Facebook watu watakutafsiri hivyo. Mfano kama uta-like picha ya ngono utatafsiriwa kuwa mzinzi na kama ni picha ya msalaba utaoneka ni wa dini.
4. Tafakari kabla huja-like, comment au share jambo lolote kwani utakavyofanya hata kwa bahatii mbaya watu watakutafsiri kuwa ndiyo desturi yako.
5. Jambo lolote ulifanyalo facebook tafakari kwanza athari zake kwa mwajiri wako, wateja wako, mpenzi wako, chama chako, timu yako, kampuni yako n.k Je watalipenda jambo ulilolifanya ?