Hafla hiyo fupi iliyoambatana na baadhi ya Viongozi wa Serikali kama vile Mh. Professa James Mark Mwandosya ( waziri asiyekuwa na wizara maalumu), Mh. Profesa Anne Tibaijuka (waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi) na Mh. Mwigulu Mchemba (mbunge CCM).
Mh. Pinda alipata wasaa wa kuzungumza na Viongozi hao mambo mbalimbali; miongoni mwa mambo aliyoyatilia mkazo wakati akizungumza na viongozi hao ni suala la Changamoto ya ajira nchini. Mh. Waziri Mkuu alisema "hivi sasa uwezo wa serikali kuwaajiri wataalam wa kada mbalimbali wanaomaliza Vyuo Vikuu hapa nchini umekuwa mgumu baada ya ongezeko la wasomi nchini hivyo aliwaomba wanazuoni hao kujiandaa kisaokolojia katika jitihada za kujiajiri kuliko kuajiriwa" katika kulielezea suala hili aliainisha baadhi ya fursa zilizopo ambazo watu hawazichangamkii wakati zingeweza kuwa komboa kiuchumi. fursa hizo ni Ufugaji wa Nyuki na Kuku wa kienyeji vitu ambavyo hata gharama ya Kilimo hiki si ghali kama ufugaji wa Ng'ombe n.k. Mh. Waziri Mkuu aliwapongeza Viongozi hawa kwa ueledi walionao katika ushiriki wa kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wanafunzi wenzao wawapo katika majukumu yao. Hali ambayo inaonekana kuleta amani katika Chuo hicho tofauti na Miaka mitatu iliyopita
Pichani ni Waziri Mkuu pamoja na Viongozi wa Serikali ya Wanafunzi UDOM
Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda akisalimiana na Mh. Janus Bernard (Rais wa Chuo cha Sanaa, Lugha na Sayansi za Jamii Chuo Kikuu cha Dodoma) |