![]() |
Pastor Peter Mitimimngi, mkurugenzi wa Voice of Hope Ministries (VHM) |
NIMEPOKELEWA KAMA MSUKUMA MKOKOTENI NA SIO MTUMISHI!
Siku moja niliitwa kufundisha mkoa fualani na ilikuwa ni kipindi cha Elninyo mnao kumbuka 1998 Mvua iliyoshuka. Ilinichukua siku 4 kufika mkoani badala ya siku 1. Nilipofika nilikwenda moja kwa moja kwa mwenyeji wangu ambaye alikuwa ni mchungaji aliyenialika kama MNENAJI MAALUM wa kingamano. Anaishi hapo hapo kanisani na familiya yake. Kwambahati mbaya sikumkuta ila nilimkuta mke wake. Nilikuwa nimejaa matope kila mahali unaweza ku "imagine" siku 4 barabarani mara tusukume basi, mara tukabate miti porini kukwamua basi kwenye matope nk.
Nilipofika hapo nyumbani mama mchungaji akaniambia "karibu, unasemaje?" nikamwambia namuhitaji mchungaji aliniangalia vile nilivyokuwa mchafu akani "judge" huenda huyu akawa ni msukuma mkokoteni. Hakutaka niingie sebuleni akaniletea kiti nikakaa hapo na begi langu. Ilikuwa ni mida kama ya saa sita mchana nilipofika hapo. Baada ya muda niliona baadhi ya wazee wa kanisa wakiingia na kutoka na nilisikia jinsi mama mtumishi alivyokuwa akiwashurutisha kwamba hawawezi kuondoka mpaka wamekula kwanza. Namimi pale nje niliendelea kupiga miayo tu.
Ilipofika mida ya saa tisa mchana watu walianza kumiminika na kuingina kanisani kwenye maombi kabla ya semina kuanza. Niliamua kubeba begi langu na vilevile nilivyokuwa mchafu na kuingia kwenye maombi. Badae ibada ilianza name nikakaa nyuma kabisa kwenye kona. Katikati ya uimbaji mchungaji aliingia akapitiliza mbele na baadaye akasimama na kusema nasikitika mgeni wetu MITIMINGI tulikuwa tunamtarajia hatujui nini kimetiokea hajafika mpaka mida hii. Nitaendelea kuendesha semina hii mpaka atakapokuja huenda kesho ataendelea.
Mtumishi aliendelea na kufundisha mpaka kama dakika kumi kabla ya kumaliza somo lake akatupa macho kwa mbali tukagongana macho. Akawa kama amepoteza mwelekeo kwa mshangao wa kuniona tena nikiwa mchafu. Akawa akijiuliza maswali haraka haraka. Inamaana mke wangu hajamuona kama amefika? Kwanini hakumpeleka katika chumba tulichomwandalia toka majuzi aoge na kubadilisha nguo?
Aliamua "kupoteza" na kumalizia ujumbe wake.
Baada tu ya kumaliza ujumbe alikumbia kuja nyuma bila kujali kwamba alikuwa amevaa suti safi alinikumbatia pamoja na matope niliyokuwa nayo. Watu waliokuwa jirani walikuwa wakimshangaa mbona mtumishi anakumbatia yule msukuma mkokoteni wanajuana kivipi? Mtumishi akaniuliza kwani umefika muda gani? nikamwambia tokea saa 6 mchana. Akasema oooh pole sana itakuwa mkewangu hakukuona jamani.Mtumishi akamuita mkewe kwa haraka. Mama Stella mbona mwalimu wetu anasema alikuwa hapa toka saa 6 mchana ilikuwaje mkapishana hukumuona? Mama mtumishi akajibu kwa mshangao mkubwa na aibu! Ha! kwani huyu ndio MITIMINGI akajibiwa yes ndio mwalimu tuliyekuwa tukimsubiria kutoka Dar mama mtumishi akasema ooh jamani mtumishi wa bwana huku akinipa mkono na kupiga magoti Bwana Yesu asifiwe kumbe ni wewe jamani lile begilako liko wapi? Karibu ndani jamani huku akibeba begi langu na kulipeleka katika chumba maalum nilichokuwa nimeandaliwa. Leo nimejisikia nikushirikishe experience niliyoipitia miaka kadhaa katika huduma. barikiwa
Chanzo: gospelkitaa.blogspot.com