m

"If you want to conquer fear, don't sit at home and think about it. Go out and get busy. "

-- Dale Carnegie, motivational expert

Monday, 24 September 2012

FURAHA YA KANISA

Furaha ya Kanisa

Furaha ni hali isiyoshikika inayomtokea mtu pale anapopata jambo nzuri, habari njema au anapokuwa na amani moyoni, naweza kusema furaha si amani bali amani huweza kuoneshwa kwa furaha. Furaha inaweza kuwa ya muda mfupi(temporary) au kipindi kirefu (permanent).
Isaya 35:10 … na furaha ya milele itakuwa juu ya vichwa vyao..
Ukweli ni kwamba kuna kundi kubwa la watu ambalo halina furaha katika jamii ya kikristo, kuna wapendwa bado hawana furaha kanisani.
Hivyo ni lazima kufanyike jitihada ya pamoja kati ya mwamini/mshirika na kiongozi ili kuleta furaha kanisani au katika jumuiya ya kikristo.
Kwa mfano mwaka 2011 radio DW ilitangaza kwamba kanisa la RC nchini ujerumani linapoteza umaarufu kwa 70%, hapa suala si dhehebu bali ni ukristo. Unafikiri kwa nini ? Sababu kubwa ya kupoteza umaarufu ni kwamba waumini hawana furaha tena kanisani na hivyo wanaamua kutafuta furaha mahali pengine. Kama waumini wanaona kanisa(si RC bali kanisa lolote la kikristo) limeingia udhalimu kazi yake kukusanya sadaka na mbegu tu, kama kanisa limeingiza ndoa za jinsia moja na unajisi kwa watoto, kanisa linaona injili ya utajirisho na miujiza ndio imani  sahihi, litakuwa limewafanya waumini kuliona kama mahali pa wahalifu na wanyang’anyi wanaamua kulikimbia maana haliwapi furaha wanayoitaka.
Mathayo 21:13 akawaambia imeandikwa , Nyumba ya yangu haitaitwa nyumba ya sala; bali nivyi mmeifanya kuwa pango la wanyang’anyi.
Bwana Yesu mwenyewe anaona uharibifu ndani ya kanisa na hapendi kuona hali hiyo, hapendi kuona uhalifu wa ndani ya kanisa kama ifanyikavyo leo. Mfano mwishoni mwa mwaka 2011 nikakutana na mwanamke ambaye Bwana ake alidhulumiwa mamimilioni ya pesa na mtumishi mmoja huko Arusha, kwa kweli ukimuona yule mwanamke amechoka kabisa na maisha na nilipoongea naye akaoneka ni mkristo mwenye kulifahamu neno barabara na ndipo nikavutiwa kuzungumza naye na kunieleza jinsi walivyofanyiwa unyang’nyi na mtumishi na hata kupelekea bwana ake kufukuzwa kazi benki. Ipo mifano mingi ya nyang’anyi ufanyikao kanisani hata kupoteza furaha kwa waumini. Hata hivyo nikutie moyo kwamba bado kuna kanisa la kweli na furaha ya kweli tena iliyo thabiti.
Je furaha ya mkristo ni katika kutajirika, kuoa, kuoa na kuolewa au mafanikio yoyote?
La hasha Matendo 8:5-8 inajibu …6na makutano kwa nia moja wakasikiliza maneno yale yaliyosemwa na Filipo walipoyasikia na kuziona ishara…..8ikawa furaha kubwa katika mji ule.
Ni dhahiri kuwa furaha ya mkristo inaanzia kusikiliza maneno na hatimae kuziona ishara za maneno hayo. Furahaa ya mkristo ni matokeo ya kulisikiza na kulisoma neno safi la kristo na utendaji wa neno hilo na si propaganda nyingine.
Tena Yohana 16:24 inasema …ombeni nanyi mtapata, furaha yenu iwe timilifu.
Kumbe kupata kwa Bwana kunaikamilisha furaha na si kwamba ndiyo furaha yenyewe.
Kwa mfano injili ya utajirisho haina nguvu Ulaya na Arabuni maana wana utajiri mkubwa lakini bado wapungukiwa furaha ya kweli bado wana hofu na mambo mbalimbali. Kama ni mafanikio ya Nyanja zote wameyapata katika elimu, uchumi, sayansi na hata siasa lakini furaha bado ni tatizo la msingi kwao. Wao wanahitaji Yesu halisi ahubiriwe maana wengine ni wasomi bado wana hofu juu ya hatima ya maisha yao. Ikiwa kuna jehanam au la na nini hatima yao baada ya kifo.   
Hebu tupitie mambo matano yanayoleta furaha kwa mkristo
1.      Kumkaribia Mungu
Ni jambo la pekee kwa mkristo maana wakristo wengi wapo mbali na Mungu na imekuwa chanzo cha kutoiona furaha ya ukristo
Zaburi 73:28.. Mfalme Daudi anasema nami kumkaribia Mungu ni kwema kwangu…
Jambo jema kabisa kwa mkristo ni kumkaribia Mungu kwa maneno, matendo na kila jambo.
2.      Kwenda madhabahuni.
Huku ni kupiga hatua kuzungumza na Mungu kwa sala na maombi, kusifu, kuabudu na hata shukrani.
Zaburi 43:3-4 …4 Hivyo nitakwenda madhabahuni kwa Mungu, kwa Mungu aliye furaha yangu na shangwe yangu….
Kumbe ni Mungu(Yesu Kristo) ndiye furaha ya mkristo na MUngu huyu napatikana madhabahuni, na hapa madhabahu ni sehemu yoyote ifaayo kumsifu, kumuabudu na kumuomba Mungualiye hai.
3.      Kumwona Yesu
Baada ya kumkaribia na kwenda madhabahuni jambo linalofuata ni kumwona Yesu.
Yohana 20:20 inasema …basi wanafunzi wakafurahi walipomwona bwana.
Hapa ni zaidi ya kuona kwa macho ya nyama bali kushiriki na katika matendo mbalimbali, huduma na maombi na zaidi kuomba na kujibiwa. Wakristo wengi wamepata furaha baada ya kuona matokeo ya maombi na imani katika maisha yao. Kujibiwa maombi si imani yenyewe tu bali kunachochea imani na furaha ya mkristo.
4.      Kumkaribisha Bwana.
Kumkaribisha bwana ni kule kumfanya awe sehemu ya maisha yako, awe wa kwanza kwa kila jambo, kila mahali na wakati wote kutembea na bwana Yesu.
Luka 19:5-6 habari ya zakayo ..6 akafanya haraka, akashuka, akamkaribisha kwa furaha.
Ni hakika kuna wakristo wengi hawajamkaribisha bwana Yesu katika maisha yao, nyumba, kazi na biashara zao na hivyo siku zote zimekuwa za taabu na mashaka. Fanya haraka kama Zakayo ambaye aliposikia Bwana Yesu anataka kuingia nyumbani kwake na kushinda humo akamkaribisha kwa furaha.
5.      Kujifunza kwa Bwana Yesu
Mkristo ni lazima akubali kujifunza kwa Bwana wakati wote na hatua kwa hatua ili aone furaha kamili ya ukristo.
Yeremia 15:16 inanena maneno yako yalionekana, nami nikayala: na maneno yako yalikuwa ni furaha kwangu maana nimeitwa kwa jina lako, Ee Bwana wa majeshi.
Mnenaji hapa si kwamba tu aliona maneno bali aliyala, akayatendea kazi na hata kujifunza kwa maneno hayo na ndipo akapata furaha na shangwe na hata kutambua kuwa ameitwa kwa jina lake(Bwana) sawa kabisa na wa wakristo wa leo ambao kwa sababu wamegoma kujifunza neno basi hata hawatambui kwamba wameitwa kwa jina la Bwana (Kristo).
Ninaweza kumaliza maneno machache kwamba kuna kanisa la Kweli, ukristo wa kweli na ambao umejaa furaha kwelikweli. Karibu katika furaha ya milele ya wokovu.
Filipi 4:4 inaisistiza furahini siku zote.
Katika safari
Kapagi

CASFETA UYOLE VETERANS (CUV)

Bwana asifiwe

Wapendwa, kwanza nawashukuru kwa namna mlivyoshiriki kwa ajili ya ufanikisha mahafali 8 ya CASFETA Uyole Sekondari.
Ninayo furaha kuwataarifu Ex CASFETA wa Uyole Sekondari maarufu kama CASFETA UYOLE VETERANS(CUV) kuwa tumekubaliana kukutana siku ya ijumaa ya tarehe 28 sept, 2012 kwa ratiba ifuatayo;
Saa 12:20-13:30- Tutashiriki ibada ya tawi la Uyole (Nyumbani kwetu)
Saa 13:30-13:45- Tutazungumza na uongozi wa tawi CASFETA Uyole Sek.
Saa 13:45-14:30- Tutakuwa na kikao chetu binafsi wanaCUV ili kujadili mustakabali wetu na ajenda mbalimbali zitakazoletwa na wanachama( akiwemo wewe unayesoma sasa taarifa hii)
Tafadhali mpendwa USIPUUZE HATA KIDOGO yapo mambo mazuri na zaidi umoja kwa kazi njema ya Huduma.
Efeso 4:5
Upatapo habari hii mtaarifu na mwingine.

N.B MwanaCUV ni mwanaCASFETA yeyote aliyemalza Uyole Sekondari mwaka wowote na kwa jinsia zote wanaoendelea na uanafunzi na hata wasio shuleni.

Ubarikiwe.

Kumfuata Yesu

KUMFUATA YESU KUNAH1TAJI MAAMUZI NA KUFAHAMU KUWA : 
(LUKA 14:27-33)
WANATAKIWA WATU WALIO TAYARI KUJITESA/KUTESWA NA KUFANYA KAZI NYINGI TENA NDOGO NDOGO NA KWA MDA MREFU USIOJULIKANA NA KWA MALIPO YASIYOJULIKANA NA KWA MSHAHARA USIOJULIKANA AMBAO UTALIPWA KWA MDA USIOJULIKANA.
NA ALIYE TAYARI LAZIMA AWE NA SIFA ZIFUATAZO:-
1. AWE TAYARI KUFANYA KAZI ZAKE MWENYEWE ILI ASIWALEMEE WENGINE ISIPOKUWA KAMA WATAMPA KWA KUPENDA (SIO KWA UJANJA UJANJA WA KUWATISHIA LAANA). 1THES. 4:11-12, 2 THESA. 3:10-12, 2 KOR.8:1-5,9:7-8,
2. AWE TAYARI KUPOTEZA HESHIMA YAKE UTU WAKE NA HATA MALI/KAZI YAKE KWA SIKU ZA MWANZO AU HATA MPAKA MWISHO WA MAISHA YAKE.(MATH.19:27-29 FIL.3:7,8)
3. AWE TAYARI KUKONDA KWA SIKU ZA MWANZO NA HATA MPAKA MWISHO WA MAISHA YAKE (JAPO SI WOTE WANAOKONDA) KWA KUJITESA NA KUJIWAJIBISHA MWENYEWE KWA KUFUNGA "MARA KWA MARA" (ILA KWA KUZINGATIA NA KUFUATA KANUNI ZA KUFUNGA/KUFUNGUA ILI ASIDHURIKE KWA SABABU ZA UJINGA). KUKESHA KWA MAOMBI, AU KWA KUSOMA BIBLIA NA KUTAFAKARI UWEZO WA MUNGU N,K. (1 KOR.9:27 2 KOR. 11:27.) (NINAPOSEMA MARA KWA MARA NAMAANISHA ZAIDI YA SIKU MBILI KILA WIKI AU SIKU NANE KILA MWEZI HATA KAMA Nl ZA MASAA 12 YAANI ASUBUHI HADI JIONI.)
4. AWE TAYARI KUOMBA ZAIDI YA SAA MOJA KILA SIKU AU MASAA SABA KILA WIKI BILA KUJALI KAZI ANAYOIFANYA AU WATU WANAOMZUNGUKA.(1 THES.5:17)
5. AWE TAYARI KUTENGWA KUTESWA NA JAMAA AU NDUGU ZAKE KUFUNGWA GEREZANl AU KUUAWA NA WATU WA TAIFA LAKE AU JINGINE KWA SABABU YA IMANI YAKE HIYO.(YOH.16:1-4, MDO.21:13, 2KOR. 11:23-26, UFUN.6:9-11) NA KWA KIPINDl CHOTE HICHO ASIMTAMKIE WALA KUMTAKIA MTU YEYETE MABAYA. (MDO.7:59-60, EBR. 4:15,RUMI. 12:14,20)
6. AWE TAYARI WATU WAMWAGE DAMU YAKE LAKINI ASIFANYE DHAMBI. YAANI AJILINDE NA DHAMBI YA AINA YOYOTE AWAPO KATIKA HALI YOYOTE IWE YA TAABU, MISIBA AU SHEREHE, IWE YA NJAA AU RAHA, KUDHARAULIWA AU KUPENDWA N,K. (EBR.12:4, 2 KOR,6:3-10, RUMI.8:35-39)
7. AWE Nl MTU ANAYEJITUMA SANA KWA MAMBO YAONEKANAYO KUWA MADOGO MADOGO, BILA KUJALISHA ELIMU YAKE AU CHEO CHAKE AU UMRI WAKE AU JINSIA YAKE. BALI AJIFANYE KUWA MDOGO KULIKO WOTE KWA KUFANYA MAMBO YOTE MEMA KUWAZIDI WENGINE. NINAPOSEMA MADOGO MADOGO Nl KAMA;KUWAHI KUWEPO KATIKA KILA (KAZI) KIPINDl KINACHOMHUSU, KUFANYA USAFI KANISANI AU VYOONI, KUWATEMBELEA WATU WENGINE N,K. (MATH.20:27, LUK.19:17)
8 ASIPENDE VYEO WALA KUONEKANA WA MAANA KULIKO WENGINE WALA KUTAKA KUITWA MAJINA YADHANIWAYO KUWA NDO YA WAKUBWA YAANI KUITWA MTUME AU MCHUNGAJI, AU NABII, AU MWINJILISTI AU MWALIMU, AU ASKOFU AU MKURUGENZI AU MENEJA N,K. (YAK.1:9f MARK.9:33-37 MATH.20:25-27, MATH.23:9-12)