m

"If you want to conquer fear, don't sit at home and think about it. Go out and get busy. "

-- Dale Carnegie, motivational expert

Sunday, 23 June 2013

Ajabu; Gari lililomsafirisha Mandela liliharibika

Mandela akiwa na Mkewe Graca
Gari la wagongwa lililokuwa likimsafirisha hospitalini rais wa zamani wa Afrika Kusini Nelson Mandela wiki mbili zilizopita, liliharibika likiwa njiani kwenda hospitalini.
Msemaji wa rais wa Afrika Kusini Mac Maharaj, amethibitisha kuwa gari hilo lilikumba na matatizo na kuwa ilibidi rais huyo wa zamani kuhamishwa hadi gari lingine.
Hata hivyo Bwana Maharaj, amesema tukio hilo halikuwa na tishio lolote kwa afya ya Bwana Mandela, kwa sababu alikuwa na madaktari wa kutosha.
Shirika la habari la Marekani CBS limenukuu vyanzo kadhaa vikidai kuwa Mandela alisalia katika eneo hilo kwa zaidi ya dakika arubaini kabla ya usaidizi kufika.
Shirika hilo la CBS limesema kuwa wakati Bwana Mandela alipokuwa akihamishwa hadi gari lingine viwango vya joto vilikuwa chini sana.
Mandela, mwenye umri wa miaka 94, alikuwa akisafirishwa kutoka hospitali moja mjini Johannesburg hadi Pretoria, wakati wa tukio hilo lililotokea tarehe nane Juni mwaka huu.
Mandela alilazwa hospitalini huku hali yake ikiwa mbaya kutokana na maambukizi ya mapafu ya mara kwa mara na tangu wakati huo amekuwa katika chumba cha wagonjwa mahututi.
Hii ni mara ya tatu kwa Bwana Mandela kulazwa hospitalini mwaka huu.
Chanzo; BBC

Rais Kagame afanya mabadiliko ya jeshi


Rais Kagame wa Rwanda
Rais Kagame wa Rwanda

Rais Kagame afanya mabadiliko kwenye uongozi mkuu wa jeshi na kumteua Jenerali Patrick Nyamvumba kuwa mkuu mpya wa majeshi.

Jenerali Patrick Nyamvumba amechukua nafasi ya jenerali Charles Kayonga aliyeshikilia nafasi hiyo tangu mwaka 2002.
Mkuu mpya wa majeshi ya Rwanda,alikuwa kamanda wa kikosi cha umoja wa mataifa cha kulinda amani UNAMID katika jimbo la Darfur nchini Sudan tangu mwaka 2009.
Mabadiliko hayo pia yameshuhudia wadhifa mpya katika uongozi wa jeshi la Rwanda, ambao ni wadhifa wa mkaguzi mkuu wa jeshi uliopewa Brigedia jenerali Jack Nziza baada ya kupandishwa cheo na kuwa meja jenerali.Jack Nziza amekuwa akihudumu kama mkurugenzi mkuu katika wizara ya ulinzi.Pia mkuu wa zamani wa idara ya upelelezi wa nje kanali Dany Munyuza ameteuliwa kuwa naibu kamishna mkuu wa polisi ya Rwanda.Sababu za mabadiliko hayo hazijawekwa wazi.
Chanzo; BBC

Jasusi Snowden atua Moscow

Edward Snowden

Ndege iliyombeba mtaalamu wa zamani wa shirika la ujasusi la Marekani, Edward Snowden imetua mjini Moscow baada ya kusafiri kutoka Hong Kong.

Chanzo kutoka ndege hiyo ya taifa la Urusi kimesema bwan snowden anayetakiwa na Marekani kwa mashtaka ya wizi wa siri za serikali,
Amepanga kuondoka hapo kesho jumatatu kuelekea nchini Cuba kabla ya kuelekea Venezuela ambako amepanga kuomba hifadhi.
Mamlaka ya Hong Kong imesema bwana Snowden aliondoka kwa hiyari yake mwenyewe na kisheria baada ya kugundua njama za kutaka kumkamata zinazofanywa na mtandao wa kijasusi wa marekani kambi ya Uchina.
Hong Kong imesema imeyakataa maombi ya marekani ya kutaka kumkamata na kumrejesha bwana Snowden nchini Marekani kwa nguvu kwa kuwa maombi hayo hayaendani na sheria za ndani za nchi hiyo.
Chanzo; bbcswahili.com