Kwa wiki kadhaa sasa tunashuhudia mvutano kati ya serikali na madaktari kuhusu mishahara na madai mengine. Nionavyo makosa yapo pande zote kwani naona madaktari wamefanya jambo lenye kushtukiza mno na hata kurukia hatua za juu kabisa kwa haraka. serikali ina mapungufu ya kutotekeleza madai ya wafanyakazi na hata kutowasikiliza. Ni jambo baya kabisa na zaidi tunaona wabunge wakizidi kuneemeka tu.
Nashauri madaktari wasingedai mishahara mikubwa moja kwa moja bali wangeishauri serikali kwa kuanzia tu mshahara na posho za madaktari zifanane sawa kabisa na wabunge, ingawa tofauti yao ni kubwa. Hapo tu panatosha kurekebisha madai ya madaktari. Tofauti ya mbunge na daktari ni kubwa kwani wakati mbunge anapata ubunge kwa mwezi mmoja tu wa kampeni daktari anapata udaktari kwa zaidi ya miaka 10. wakati mgomo wa mbunge haugharimu kitu lakini wa daktari unagharimu maisha ya watu.
Tafakuri kubwa kabisa inahitajika.