Limeandaliwa na Peter K. Kapagi Simu: 0764/0658-734620 Barua pepe kakakapagi@gmail.com blogu: http://www.kapagiii.blogspot.com/
Luka 9:18-20 …je makutano hao wanasema kuwa mimi ni nani?..
Y |
amkini hujatambua kuwa wewe ni nani, una nafasi gai, na jamii inakutambuaje na ndio maana upo hivyo ulivyo (ukifanya vizuri au vibaya unaona sawa tu)
Hebu tuangalie nafasi saba ulizonazo kama mkristo safi ;
1. WEWE NI UZAO/KIUMBE KIPYA
2kor 5:17 inasema …mtu akiwa ndani ya kristo amekuwa kiumbe kipya,.. ina maana kuwa mkristo tu ni mabadiliko kutoka uchakavu na kuwa mpya, na Yoh 1:12 inasisitiza …bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu… ina maana anakuwa baba yako halisi na wewe mwanae halisi.
- Anajaza sehemu maalumu katika moyo wako na kuwa na asili yake, maisha yake, upendo wake na yote aliyonayo yeye yapo kwa ajili yako. Ezekiel 36:26-27 (RSV)
- Yote uliyoyapoteza kupitia Adamu unarudishiwa kupitia Yesu.
- Huwezi kushindwa na shetani kwa namna yoyote ukisimama eneo lako katika Mungu
- Sasa ni wakati wa kumnyanyasa ibilisi na kuharibu kazi zake.
2. UMEHAMISHWA
Mpendwa wakati wa kuokoka unahamishiwa ufalme wa mungu. Kol 1:3…. Akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa mwana wa pendo lake.
Ametukirimia ahadi kubwa, tukisoma 2Pet 1:4 tena kwa hayo ametukirimia ahadi kubwa mno..
Tena ishara mbalimbali zitaambatana nawe kama kutoa pepo nqm kusem kwa lugha mpya. Marko 16:17
3. WEWE NI MTU MAALUMU.
Mtu yeyote aliyeokoka si mtu wa kawaida. Mdo 10:13-14. pia umetakaswa na Mungu, umekuwa taifa takatifu. 1Pet 2;10 … ni taifa la mungu… (RSV)
4. UPO JUU YA YOTE
Yeye ajaye kutoka juu , huyo yu juu ya yote. Kumbe mkristo aliyeokolewa na kristo amabaye alitoka juu na yupo juu, anakuwa juu ya yote. Hivyo hakuna cha kukusumbua iwe magonjwa, masikitiko, kufeli, n.k
5. WEWE NI MSHINDI
Neno linasema yeye awagusaye nyinyi anigusa mboni ya jicho lake(Mungu) Zek 2:8-9 na tena Mungu ni Bwana wa majeshi. Tena kwa kuwa umezaliwa na Mungu wewe ni mshindi tu. 1Yoh 5:4.umembeba mtu mkubwa ndani yako na Mungu hashindwi lolote.
6. NINYI NI MIUNGU(gods)
Zab 82:6 inasema mimi nimesema ndinyi miungu na wana wa aliye juu, nyote pia. Hivyo unaweza kufanya mabo yote aliyoyafanya Bwana yaani hata ishara na maajabu.
Mnaweza kuwa katika halia alizonazo Mungu yaani kustarehe, kutosumbuliwa na Magonjwa, kuwa watakatifu, kupenda ibada na hali nyingi alizonazo.
Nafasi yako ni ya uungu wa Mungu unaobeba amani yake, afya yake, hekima yake, maisha, furaha na nguvu yake.
Katika Yohana 10:34 tunaona kuwa hata Bwana Yesu anatambua uungu wako.
7. UPO TU KATIKA MFUMO WA MWANADAMU
Mpendwa upo kama mwanadamu wa kawaida lakini ni mtu wa tofauti uliyekubaliwa na Mungu. Mdo 3:22-25. asiyekusikiliza ataangamizwa na kutengwa na watu wake(atalaaniwa) kwa maana wewe ni uzao wa manabii waliobarikiwa.
Mpendwa usiwe mwongeaji sana (maneno yasiyo na faida) kwani Mungu haneni siri zake na waongeaji sana bali na watakatifu wa kweli.
Sasa nuia kuwa mtu Fulani katika jamii yako na mazingira uliyopo kwani Mungu ana mpango na wewe.
Remember Satan is a toothless Bulldog so never hurt you.
Kumbuka shetani ni mbwa dume asiye na meno hivyo hawezi kukudhuru kamwe.