m

"If you want to conquer fear, don't sit at home and think about it. Go out and get busy. "

-- Dale Carnegie, motivational expert

Wednesday, 25 December 2013

Nafasi ya Tanzania imeonekana msiba wa Mandela

Share bookmark Print Email Rating
 
Na Kelvin Matandiko, Mwananchi

Posted  Jumatano,Decemba18  2013  saa 13:10 PM
Kwa ufupi
  • Fursa iliyoipata Tanzania ya kuhutubia na aina ya hotuba iliyotolewa na Rais Kikwete kwenye mazishi ya Mandela imeipaisha nchi kidiplomasia na kufanya historia yake ijulikane dunia nzima. 


Matukio mbalimbali yaliyotokea Jumapili kwenye mazishi ya Rais wa kwanza mzalendo wa Afrika Kusini, Nelson Mandela yamenikumbusha yaliyotokea katika sherehe za miaka 50 tangu kuanzishwa OAU, sasa Umoja wa Afrika (AU).
Katika maadhimisho hayo, Tanzania ilimwagiwa sifa kedekede kutoka kwa wakuu wa nchi mbalimbali walioshiriki, wakiwamo Rais wa Senegal, Mark Sall, Waziri Mkuu wa Ethiopia, Hailemariam Dessalegne na Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini.
Rais Zuma alitoa hisia zake kwa Tanzania, akisema wazi kuwa wananchi wa nchi Afrika Kusini hawatausahau mchango wa Tanzania katika kuwakomboa na kuwafikisha walipo sasa. “Tulisaidiwa na nchi nyingi, lakini Tanzania ilitusaidia kwa namna ya kipekee.”
Sifa hizo ziliwekewa uzito katika hotuba ya Rais Jakaya Kikwete kwenye mazishi, alipoamua kueleza kwa uwazi historia ya Tanzania katika ukombozi wa Afrika Kusini na Afrika kwa jumla.
Awali, ilipofanyika ibada ya kumbukumbu ya Mandela ambapo viongozi mbalimbali zaidi ya 100 kutoka maeneo mbalimbali duniani walishiriki, Watanzania hawakuelewa kuona mchango wa Tanzania hauelezwi wazi katika tukio hilo muhimu wala kupewa fursa ya kuhutubia, lakini bila shaka nyoyo zao zilisuuzika baadaye Jumapili, fursa hiyo ilipopatikana siku ya mazishi.
Kauli ya Prof Mpangala
Miongoni mwa walioweka wazi dukuduku lao ni Profesa Gaudence Mpangala wa Kitengo cha Sayansi ya Jamii, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), akisema Tanzania ilitakiwa kupewa nafasi ya kuzungumza lolote kutokana na ukaribu wa nchi hizo.
Anasema Tanzania ni moja ya nchi duniani zenye historia kubwa na ujenzi wa taifa la Afrika Kusini.
“Na baada ya kutoka gerezani mwaka 1990, Tanzania ilikuwa nchi ya kwanza Mandela kuitembelea kwa lengo la kutoa shukrani zake, tukampatia na heshima ya jina lake kuitwa barabara muhimu, Mandela Road,” anasema Profesa Mpangala na kuongeza;
Sasa sijui ni utaratibu gani uliotumika kuangalia vigezo vya kuhutubia, kwa sababu siku zote rafiki yako wa karibu ndiye anayestahili nafasi ya kuzungumza siku ya msiba wako,” anasema.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) Usu Mallya anasema kutokana na mazingira hayo, kuna kila sababu ya Watanzania kujiuliza kwa sasa, iwapo thamani iliyokuwapo katika harakati za ukombozi bado inatambuliwa.
Anaongeza kuwa ni muhimu kukumbuka kwamba Tanzania ilikuwa kitovu cha harakati za ukombozi na kituo cha kuandaa fikra mbadala kwa ajili ya kutumika katika harakati za kuleta mabadiliko kwa ndani na nchi nyingine za Afrika.
Kusoma zaidi bofya hapa http://www.mwananchi.co.tz/Makala/Nafasi-ya-Tanzania-imeonekana-msiba-wa-Mandela/-/1597592/2117016/-/cnsj5cz/-/index.html

No comments:

Post a Comment