m

"If you want to conquer fear, don't sit at home and think about it. Go out and get busy. "

-- Dale Carnegie, motivational expert

Friday, 22 November 2013

Prof. Mwaluko Atakumbukwa

Photo: Prof. Mwaluko Atakumbukwa
===================
Kwa niaba ya KII na kwa niaba yangu mimi mwenyewe nimepokea taarifa za kifo cha Prof. Gabriel Mwaluko kwa majonzi makubwa. Prof Mwaluko mwanataaluma nguli katika fani ya udaktari na ambaye alikuwa mkuu wa chuo kikuu cha mt. Yohana (St. John's) amefariki dunia akiwa nchini India alikokuwa akipatiwa matibabu ya Saratani ya koo katika Hospital ya Appolo. Prof Mwaluko ambaye wakati wote alijawa na tabasamu na asiye na makuu ndani ya miaka miwili ya uwepo wake SJUT alikuwa na jitihada kubwa ya ya kukiendeleza chuo. Katiba hotuba ya alipotutembelea Kituo cha Mt. marko Dar Es Salaam aliahidi kukifanya kuwa cho kikuu kishiriki jambo ambalo ingekuwa hatua kubwa ya maendeleo ya chuo, Kwa kuanzia akakubali mahafali ya St. marks kwa mara ya kwanza kufanyika Dar es Salaam.
Binafsi nitamkumbuka sana lakini chuo cha Mt. Yohana kinapaswa kumbkumbuka kwa vitendo  kwa kuondoa urasimu katika utendaji na pili kufanikisha kukifanya kituo cha Dar es Salaam kuwa Chuo Kikuu Kishiriki ili kukipa nguvu zaidi jambo ambalo Prof Mwaluko alitamani litokee kabla mwaka huu haujaisha.
Bwana alitoa na Bwana Ametwaa... Jina la Bwana lihimidiwe. Kwa niaba ya KII na kwa niaba yangu mimi mwenyewe nimepokea taarifa za kifo cha Prof. Gabriel Mwaluko kwa majonzi makubwa. Prof Mwaluko mwanataaluma nguli katika fani ya udaktari na ambaye alikuwa mkuu wa chuo kikuu cha mt. Yohana (St. John's) amefariki dunia akiwa nchini India alikokuwa akipatiwa matibabu ya Saratani ya koo katika Hospital ya Appolo. Prof Mwaluko ambaye wakati wote alijawa na tabasamu na asiye na makuu ndani ya miaka miwili ya uwepo wake SJUT alikuwa na jitihada kubwa ya ya kukiendeleza chuo. Katiba hotuba ya alipotutembelea Kituo cha Mt. marko Dar Es Salaam aliahidi kukifanya kuwa cho kikuu kishiriki jambo ambalo ingekuwa hatua kubwa ya maendeleo ya chuo, Kwa kuanzia akakubali mahafali ya St. marks kwa mara ya kwanza kufanyika Dar es Salaam.
Binafsi nitamkumbuka sana lakini chuo cha Mt. Yohana kinapaswa kumbkumbuka kwa vitendo kwa kuondoa urasimu katika utendaji na pili kufanikisha kukifanya kituo cha Dar es Salaam kuwa Chuo Kikuu Kishiriki ili kukipa nguvu zaidi jambo ambalo Prof Mwaluko alitamani litokee kabla mwaka huu haujaisha.
Bwana alitoa na Bwana Ametwaa... Jina la Bwana lihimidiwe.

Tuesday, 19 November 2013

Harusi ya Sri Lanka yavunja rekodi ya Guinness kwa kuwa na wapambe wengi.

Katika Picha

katika picha  

 

 

 

 

Harusi ya Nisansala na Nalin iliyofanyika Negombo, Sri Lanka yavunja rekodi ya dunia ya Guinness kwa kuwa na wapambe wengi zaidi kuliko harusi nyengine yeyote ile. Nov 8 2013. Kulikuwa wasimamizi wanawake 126 na wapambe wanaume 25. 

Tuesday, 12 November 2013

Kapagi Information Institute-KII menu


Zitto: Nimechoka Kuzushiwa na kuchafuliwa


Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe
*Afichua siri ya kutishiwa kuuawa
*Asema anajipanga kwenda kortini
*Amwandikia Dk. Slaa kudai kauli ya Chadema

NAIBU Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Zitto Kabwe, ameibuka na kutoa kauli na tamko dhidi ya tuhuma mpya dhidi yake zilizosambazwa katika mitandao ya intaneti katika siku za hivi karibuni.

Zitto, ambaye pia ni Naibu Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni na Mbunge wa Kigoma Mjini, amefanya hivyo akitumia majukwaa mawili tofauti. Mwanasiasa huyo kijana ambaye amejipambanua kuwa mtetezi wa misingi ya utaifa, raslimali za nchi, uchumi na masuala ya utawala bora ndani na nje ya chama chake, alifanya hivyo kwa mara ya kwanza juzi jioni, wakati alipokuwa akihutubia mkutano mkubwa wa hadhara katika uwanja wa Kolimba wilayani Kariua, Mkoa wa Tabora.
http://rai.co.tz/index.php?option=com_content&view=article&id=721:zitto-nimechoka-kuzushiwa-na-kuchafuliwa-&catid=1:siasa&Itemid=2

SIRI SIRINI, SOMA HAPA



RIPOTI YA SIRI JUU YA ZITTO KABWE

KWA

CHADEMA

UCHUNGUZI WA MWENENDO WA KISIASA WA ZITTO Z. KABWE NDANI NA NJE YA CHADEMA.

UTANGULIZI:Tangu mwaka 2008 mwenendo wa kisiasa wa Zitto Zuber Kabwe ulianza kutiliwa shaka na wanachama wa CHADEMA ndani na nje ya chama, Hili lilipelekea kuibuka maneno ya chini kwa chini kuwa anakisaliti chama.
Hilo liliilazimu timu ya kijasusi ya chama kuanza kufuatilia nyendo zake kwa ukaribu zaidi usiku na mchana ili kujiridhisha pasipo kuacha chembe ya mashaka. Ifahamike kuwa chama kina idara ya ulinzi na usalama wa chama na viongozi wake yenye uwezo wa kufuatilia nyendo za majasusi wa nje na viongozi na wanachama wake popote walipo kwa masaa 24. Baada ya

kujiridhisha kuwa mwenendo wake ni wa mashaka, bila kusita timu ya ujasusi ilianza kazi rasmi ya ujasusi dhidi ya nyendo zote za Zitto Zuberi Kabwe

Monday, 11 November 2013

PINDA ASHIRIKI CHAKULA CHA JIONI NA VIONGOZI WA SERIKALI YA WANAFUNZI UDOM

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Peter Kayanza Mizengo Pinda siku ya jana tarehe 10 November 2013 aliwaalika Viongozi wa Serikali ya Wanafunzi Chuo Kikuu cha Dodoma kushiriki naye Chakula cha jioni katika makazi yake mkoani Dodoma.
Hafla hiyo fupi iliyoambatana na baadhi ya Viongozi wa Serikali kama vile Mh. Professa James Mark Mwandosya ( waziri asiyekuwa na wizara maalumu), Mh. Profesa Anne Tibaijuka (waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi) na Mh. Mwigulu Mchemba (mbunge CCM).
Mh. Pinda alipata wasaa wa kuzungumza na Viongozi hao mambo mbalimbali; miongoni mwa mambo aliyoyatilia mkazo wakati akizungumza na viongozi hao ni suala la Changamoto ya ajira nchini. Mh. Waziri Mkuu alisema "hivi sasa uwezo wa serikali kuwaajiri wataalam wa kada mbalimbali wanaomaliza Vyuo Vikuu hapa nchini umekuwa mgumu baada ya ongezeko la wasomi nchini hivyo aliwaomba wanazuoni hao kujiandaa kisaokolojia katika jitihada za kujiajiri kuliko kuajiriwa" katika kulielezea suala hili aliainisha baadhi ya fursa zilizopo ambazo watu hawazichangamkii wakati zingeweza kuwa komboa kiuchumi. fursa hizo ni Ufugaji wa Nyuki na Kuku wa kienyeji vitu ambavyo hata gharama ya Kilimo hiki si ghali kama ufugaji wa Ng'ombe n.k. Mh. Waziri Mkuu aliwapongeza Viongozi hawa kwa ueledi walionao katika ushiriki wa kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wanafunzi wenzao wawapo katika majukumu yao. Hali ambayo inaonekana kuleta amani katika Chuo hicho tofauti na Miaka mitatu iliyopita
 Pichani ni Waziri Mkuu pamoja na Viongozi wa Serikali ya Wanafunzi UDOM

Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda akisalimiana na Mh. Janus Bernard (Rais wa Chuo cha Sanaa, Lugha na Sayansi za Jamii Chuo Kikuu cha Dodoma)
.

Saturday, 9 November 2013

HEKA HEKA OFISINI KII

 Hapa ni mojawapo ya mabango ya shughuli zinazofanyika kwenye ofisi ya KII ambao pia ndo wachapishaji na wamiliki wa blog hii.
 Huu ni mwonekano unapingia tu ofisini


 Vitendea kazi vya KII vinavyoonekana, hapa ni baada ya ngamizi mama "main computer" ya Hitachi All in 1 kuwa katika maboresha Safari Computers.
 Java hayuko nyuma katika kusoma habari mbalimbali za mitandao zifaazo kwa ajili kuchambuliwa, kuhaririwa na hatimaye kuchapishwa.
 Huduma za kifedha pia zinapatikana kwani hapo ukutani ni namba ya wakala wa Mpesa, unaweza kulipia kwa Mpesa katika huduma zetu
 Melody, ambaye yupo katika mafunzo ya dharura kwa ajil uandishi wa habari KII

 Bw. Kapagi afisa mtendaji mkuu-KII na Mhariri mwandamizi wa Blogu ya kapagiii.blogspot.com na pia sasa ni mhariri na msanifu wa blogu ya Mazingira Natural Products (mazingiranp.blogspot.com)
 Java halali ofisini, hapa anatafakari mwenendo wa kazi

 KII huwezi kukosa habari, hapa ni baadhi tu ya nyaraka zinazopatikana Computer Dictionary, Katiba ya nchi, Biblia na vitabu kadha wa kadha na chini ni magazeti ya kila siku kwa ajili ya kujisomea na kupata habari mbalimbali
 "Chukua kazi yako na karibu tena" ni maneno ya mkurugenzi akitoa huduma.
 Juvenile naye hayuko mbali kukamilisha timu ya utendaji ya KII, yupo kazini katika uchapaji.

Mkurugenzi wakati wote ni shughuli tu, usiku ndo kwanza ni kama asubuhi.

Ujirani mwenza, maarufu kama kwa mama peter, kioski na genge kila kitu unapata hapo. Na ndo biashara iliyomsomesha Peter Kapagi na wenzake.
Leo nimekuletea baadhi tu ya hekaheka za ofisini kwa KII, njoo ujionee mwenyewe utendaji mahiri kabisa wa KII. Kamwe hutojuta na hutorudi kama ulivyo.
Kwetu habari ni Maisha

Thursday, 7 November 2013

Kikwete asema Tanzania haitajitoa A.Mashariki



Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania
Tanzania imesema hataitajitoa katika Jumuiya ya Afrika kama wengi walivyodhani na badala yake imedhamiria kuhakikisha Jumuiya hiyo inadumu na kustawi.
Akilihutubia bunge la Tanzania, mjini Dodoma, katikati mwa Tanzania, Rais wa nchi hiyo, Jakaya Kikwete amesema kwamba Tanzania haina mpango wala fikra za kujitoa katika Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa kuwa ni nchi inayoamini katika umoja na maendeleo na imekuwa ikitumia gharama kubwa kuhakikisha jumuiya hiyo inaimarika.
"Tanzania ni mwanachama mvumilivu, mtiifu na mwaminifu na tunatimiza wajibu wetu kwa jumuiya na kuhusika kikamilifu katika ujenzi wake." amesema Rais Kikwete.
Rais Kikwete ametumia muda mrefu katika hotuba hiyo kuchambua masuala mbalimbali ya msingi ya uhai wa jumuiya hiyo huku akisema ameshangazwa na nchi za Kenya, Uganda na Rwanda kuzitenga Tanzania na Burundi.
Amesema kuna masuala ambayo hayazifungi nchi wanachama katika mkataba wa umoja wao, hivyo kuwa na uhuru wa ushirikiano na nchi ndani ya jumuiya na hata nje.
"Naomba kwanza niweke wazi jambo moja, kwamba nchi mbili wanachama au zaidi hazikatazwi kuwa na makubaliano ya ushirikiano katika kufanya mambo mbalimbali. Hata sisi Tanzania tunao ushirikiano wa namna hiyo na nchi zote wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Lakini, nchi wanachama zinatakiwa kufanya hivyo kwa yale mambo ambayo hayako kwenye shughuli za Jumuiya kwa maana kwamba hayamo katika Mkataba au Itifaki au hakuna uamuzi wa msingi uliofanywa na vikao au taasisi za Jumuiya kuyashughulikia. Pia, tunaweza kufanya hivyo kwa mambo ambayo yalishaamuliwa na Jumuiya yatekelezwe na ruhusa imetolewa kwa nchi yo yote iliyokuwa tayari kutekeleza ama peke yake au kwa kushirikiana na nchi nyingine".
Hata hivyo Rais Kikwete amesema huenda mambo yanayoitenga Tanzania na nchi nyingine tatu za jumuiya ya Afrika Mashariki, ni msimamo wake kuhusu kuharakisha shirikisho, masuala ya ardhi, ajira, na uhamiaji.
Pia Rais Kikwete amesema Tanzania haina mpango wa kujitoa kwa kuwa inaamini na ina uhakika kuwa haijafanya jambo lolote baya dhidi ya jumuiya au nchi mwanachama yeyote wa jumuiya hiyo.
Chanzo; bbcswahili.com

Sunday, 3 November 2013

MATOKEO DARASA LA SABA 2013 HADHARANI

Wizara ya Elimu na mafunzo ya Ufundi yatangaza rasmi matokeo ya wanafunzi waliomaliza darasa la saba hivi karibuni. unaweza yatazama kwa kupitia kiungo kifuatacho.http://www.necta.go.tz/matokeo_html_2013/psle.htm

Sunday, 27 October 2013

Ofisi ya KII yafunguliwa rasmi

Tumeanza!!!
Ninayo furaha kubwa kwamba Ofisi yetu kuu ya Kapagi Information Institute -KII imefunguliwa rasmi hapo jana Jumamosi ya tar 25oct, 2013. Kila kitu kimeenda sawa kama nilivyokuwa nikitaarifu awali. Kwa niaba ya KII na mimi mwenyewe ninazo shukrani za pekee kwa Bwana Yesu Kristo na kwa wote walioshiriki kuniunga mkono na kuniamini hata kunichochea sana niweze kufungu ofisi japo wengi walipenda iwe Dar es Salaam.
Natamani kuwaorodhesha wote waliniunga mkono kwa hali, mawazo na mali hakika si wachache ni wengi lkn kwa neema nitaorodhesha japo wachache kwa niaba ya wengi.
Acha niwaorodheshe ijulikane kwamba wapo walio nyuma yangu na taasisi, wapo wanaoitakia mema, kuimbea, kushauri hata kuwa radhi kufadhili
Nianze kwa familia, dada John Janet Merinyo, Mauki, Furaha Samwel na Mr Chipanda, Sunny, Xaveria, Neema Michael, Abel Mwakyandwike, Uncle Mwasomola, Oswin Joctan, Rehema Chillery, Sia na Neem Stationery, Shangarai, Papalika, Mary Simon, Uncle Dickson (Computer Doctor), Teddy na Yamsebo Stationary, Bineth Printing bila Kumsahau Mama G wa ukweli (rehema Sanga) na Gladiness Stationery, Sae internet Cafe kwa Software, Mzee Chale na Marge (St. Marks Library), Janus Bernard,
Aaah, ni wengi na hili linanipa nguvu kwamba nimeanza na kuna watu wapo nyuma kwa ajili ya Taasisi hii Muhimu. Nisamehe ikiwa sikukuorodhesha na hiyo siyo maana kwamba sijaheshimu mchango wako. Una maana kwangu na kwa KII, na ikiwa una maana kwangu una kubwa kwa jamii nitakayoihudumia.
Niwe na tamko moja tu sasa kwamba nimeanza na sitorudi nyumba, nitaficha wapi sura yangu kwa kundi hili kubwa linaloniunga mkono usiku na mchana.
Niwe na Ahadi moja kwamba nilipofundisha ujasiriamali mara zote nimezungumzia kuwa "kwa wafanyakazi wenye mshahara wa msingi ujasiriamali ni njia ya kujipatia kipato cha ziada" LAKINI MIMI NITAENDA MBALI NATAKA KUFANYA UJASIRIAMALI KUWA JIPATO CHA MSINGI na mshahara kiduchu wa serikali na mashirika dhalimu kuwa kipato cha ziada. hili halitafanyika kwa njia nyingione isipokuwa kutumia kila furasa kuwahudumia watu na kuondoa matatizo ya msingi kwa jamii na taaluma.
Kwa kuwa ndo kama naanza nisiwe na mengi, Wakati ujao nitakuja na makala yenye Dira, Malengo na Wito wa Kapagi Information Institute-KII.
Tumeanza tukiwa dhaifu, tujipange kufanya Makubwa. Tanzania yenye huzuni inatusubiri ifanye sherehe ya kuzaliwa kwetu kama wakombozi.

Thursday, 24 October 2013

KII HEAD OFFICE IN MBEYA

KII Head Office going to be opened soon in Mbeya.
Am very happy to write these because i was waiting it for a long time as my supporters demand. Our head office will open on Saturday at Zambia rd/ Ituha st, Mbeya city.
The functions of office will be Ultimate Secretarial services, Entrepreneurship training, Computer software and maintainance as well as to search and provide information basing on religion, economics and politics.
KII NEED TO GO BIG NOW
Join and Support it
Habari ni Maisha
kapagiii.blogspot.com
FULL PROFILE ON KII IS COMING on Blog and our Facebook page...be patient

Wednesday, 2 October 2013

Mashine za TRA zazua tafrani jijini Mbeya

Suala la ununuzi wa mashine za TRA za kieletroni za risiti kwabei ya sh. 800,000/= limezua Tafrani kubwa jijini Mbeya. tfrani hiyo imesababishwa na bei ya mashine hiyo ambayo inauzwa kuanzia sh.800,000/- kiasi ambacho wafanyabioashara wanapinga kwa kigezo kuwa bei hiyo ni zaidi ya mtaji wa biashara. katika mahojiano baadhi ya wafanyabiasha eneo la Mwanjelwa na Sae wamezungumzia bei ya mashine hizo kuwa na uwizi mkubwa kwani wenyewe hawapinmgi matumizi yake isipokuwa wanahoji kwanini ziuzwe kwa gharama kubwa kiasi hicho.

Wengine wameenda mbali zaidi wakikosoa mchakato huo kwamba utawakwamisha wafanyabiashara wengi na kwamba kwa kuwa mashine hizo zitawafaidisha TRA kwa suala ulipaji kodi zingepaswa kutolea bure sawa na mita za maji na umeme kwani zitakuwa mali ya TRA. Baadhi ya watu wakahoji kwanini mashine hizo ndogo ziwe ghali kiasi hicho kuzidi gharama ya mashine kubwa za photocopy ambazo huuzwa kwa sh.600,000, Kompyuta na hata Printer ambazo gharama zake si zaidi ya 500,000/=

Kufuatia tamko hilo la TRA kuwataka wafanyabiashara wote wanaouza zaidi ya sh.45,000/= kwa siku kuhakikisha wananunua mashine hizo likasababisha mgomo wa wafanyabiasha wa Mwanjelwa ambao wakaandaa mkutano uliokua ufanyike Viwanja vya S/M Ruanda Nzovywe ambao hata hivyo ukazuia na polisi kwa ulipuaji wa mabomu ya machozi.

Hapa ni baadhi ya picha za matukio ya vurugu hizo;

Polisi wakiwa wanasindikiza gari la matangazo kutangaza kuomba Vurugu hizo na maandamano yasiyo na kibali yasitishwe
 Polisi wakiwa wameimarisha ulinzi mkali 

 Wafanya biashara wakiwa viwanjwa vya Shule ya Msingi Ruanda Nzovwe kungoja kusikiliza nini  hatma yao
 Baadhi ya watu wakikimbia Mabomu ya machozi yalipoanza kurushwa ili  kuepusha vurugu
 Mawe yakiwa yamepangwa kuzuia magari yasiende kokote
 Maduka yote yakiwa yamefungwa eneo la mwanjelwa kupinga ununuzi wa mashine hizo za TRA
 Vijana hawa wakiwa wana nawa uso baada ya Bomu la machozi kuwapitia 
 Jiwe kubwa likiwa limewekwa katika Barabara magari yasipite
  Matairi yakiwa yamewashwa barabarani kuanza vurugu kupinga mashine hizo