m

"If you want to conquer fear, don't sit at home and think about it. Go out and get busy. "

-- Dale Carnegie, motivational expert

Wednesday, 3 April 2013

Kitendawili cha Kuchinja Nyama Nchini Tanzania

Kitendawili cha Kuchinja Nyama Nchini Tanzania
Ndugu Mtanzania kwa miezi kadhaa sasa kumekuwepo na mvutano mkubwa juu ya uchinjani nyama chini Tanzania, yaani nani mwenye haki ya kuchinja kati ya muislamu na mkristo. Mvutano huo umepelekea mgogoro kule Geita na sasa Tunduma.  Jambo hili limekuwa KITENDAWILI maana kinahitaji jibu na mwenye kutupa jibu hatuna hakika kama analo au la maana yupo kimya. Binafsi ninao mtazamo juu ya jambo hili na ningependa kuchangia. Kwanza ningependa kueleza ukweli usiojulikana kwa wengi yaani kwa wakristo walio wengi na pengine waislamu na wapagani pia. Nauita ukweli usiojulikana kutokana na kwamba baada ya mvutano huo kutokea nikajaribu kuhojiana na watu kadhaa juu ya jambo hili, ajabu ni kuwa walio wengi walionekana kutofahamu lolote juu ya machinjio yetu nchini, mmiliki na hata mchinjaji halali. NCHINI TANZANIA MACHINJIO HALALI KISHERIA YANAMILIKWA NA HALMASHAURI ZA MIJI NA WACHINJAJI HALALI NI WAISLAMU. Kwa upeo mdogo nilionao ni kwamba kwa muislamu mnyama aliyechinjwa na mtu asiye muislamu au pasipo swala basi nyama hiyo itakuwa kibudu(nyama haramu). Kwa mkristo ninajua jambo moja kwamba damu iliyomwagika msalabani ina nguvu ya kutakasa na zaidi wamepewa mamlaka ya kukanyaga ng’e na nyoka tena kula vitu vya kufisha na kwamba havitawafisha kabisa, tena wameambiwa wafanikiwe katika katika mambo yote na kuwa na afya njema kama roho ifanikiwavyo(Marko 16:16-18, 3Yohana 1:2).
Ninavyoelewa ni kwamba serikali yetu ina tamka wazi kuwa haina dini lakini inasisitiza kuheshimu imani kwa kila mtu. Ni jambo jema kabisa kwa serikali ambayo ina watu wa dini tofauti tena kwa makundi makubwa kujitenga na dini ili kila mtu awe huru kuabudu anachotaka. Zipo nchi nyingi za kidini (Non secular states) kama Saudi Arabia na hata Uingereza kwani yenyewe inajihusisha zaidi na kanisa lake la Anglikana. Swali langu ni kwamba serikali yetu nzuri inayotamka wazi haina dini imewezaje kutumia kigezo cha dini katika machinjio yake? Inawezaje kuamini kwamba muislamu ndiye halali kuchicha na si mkristo wakati yenyewe haina dini? Ninachofahamu ni kuwa serikali ilijitenga na dini si kuruhusu tu uhuru wa kuabudu chochote kwa watu wake bali pia kuondoa migogoro ya kidini. Mtu akijifanya kuficha tone la mafuta ndani ya maji litaelea tu! Na sasa ndo hilo linaelea baada ya kufichwa kwa miaka mingi na limekuwa kitendawili na jibu lake lahitaji mji.
Kama kitendawili hiki ningetegewa mimi ningejibu hivi; serikali haina dini na kwa kuwa machinjio ni ya serikali basi iamue pia kutokuwa na dini hata katika machinjio, yaani iajiri wachinjaji pasipo kufuata imani awe muislamu, mkristo na hata mpagani maana serikali yetu inawatambua, si wapo wabunge waioapa kwa korani wala Biblia Takatifu? Suala la dua, swala, maombi au maombezi ya nyama yabakie kwa mlaji, mlaji baada ya kununua nyama awajibike kuitakasa ili iwe halali sawa na imani yake. La sivyo serikali ijitenge na machinjio jambo ambalo ni hatari zaidi kwani ni vigumu kutenga nchi nzima machinjio ya wakristo, waislamu, wahindu, wapagani na watu wa imani nyinginezo maana zipo nyingi. Ikitenga machinjio itabidi itenge na mabucha na hapo ndo utakuwa mwanzo wa ubaguzi wa kidini.
Naishauri serikali kuchukua hatua za haraka juu ya jambo hili ili kuepuka majuto.
Huu ni mtazamo wangu, si wa dhehebu wala dini yangu.
Wako katika safari,
Mwl Peter Kapagi

Friday, 29 March 2013

Maana ya Pasaka na Maombi yake.

Maana ya Pasaka na Maombi yake.
Mpendwa watu wengi sasa wanatamka pasaka lakini ajabu ni kwamba wanaitamka kwa desturi tu, wengine hata ukiwahoji pasaka maana yake nini hawaelewi chochote. Hakika laiti wangelijua maana ya pasaka wangeliomba mambo makubwa kabisa kwani ndo majira ambayo mageuzi makubwa yanafanyika kwa mwanadamu.
Maana ya Pasaka
Pasaka haikuanza baada ya kuzaliwa Kristo au baada ya mateso ya Kristo bali wakati wana wa Israeli wa lipokuwa Misri.
Kutoka 12:11 ...nanyi mtamla kwa haraka; ni pasaka ya Bwana.
Bwana alipokuwa anataka kuangamiza wazaliwa wa kwanza wa wana na wanyama wa wamisri akatafuta namna ya kuwaokoa wana wa Israeli kutoka maangamizi hayo na ndipo anawaamuru wachinje mnyama asiye na ila, damu yake wapake katika milango na wamle pasaka. Na wakakumbushwa wafanye hivyo kama ukumbusho vizazi na vizazi.
Kwanini Mateso ya Bwana Yesu Krito wa Nazareth yaitwe Pasaka?
Kwanza mateso yalitukia majira ya Pasaka ile sikukuu ya mikate isiyotiwa Chachu (Pasaka ya ukumbusho wa Bwana alivyowakoa kule Misri zidi ya maangamizi ya mzaliwa wa kwanza) Luka 22 :1-2 ikakaribia sikukuu ya mikate isiyotiwa chachu, iitwayo sikukuu ya pasaka. Na wakuu wa makuhani  na waandishi walikuwa wakitafuta njia ya kumwua, maana walikuwa wakiwaogopa watu.
Kwa hiyo Mafarisayo walipanga kumuua majira ya pasaka japo waliogopa kuiharibu pasaka kwa sababu kuu moja kwamba kama wangemuua majira mengine nje ya pasaka basi wangesababisha kuwepo pasaka mbili yaani ile ya mikate isiyotiwa chachu na ya mateso na kuuawa kwa Bwana Yesu. Nasema hivi kwa sababu Pasaka ya kwanza ilikuwa taswira ya pasaka ya pili pasaka halisi ya ukombozi wa wanadamu wote.
Je kuna uhusiano wa Pasaka hizi mbili?
Ndio kwa sababu pasaka ya kwanza ilihitajika ili kuwaokoa wana wa Israel na pasaka ya mateso ya Kristo kwa ajili ya kuwaokoa wanadamu wote.
Mathayo 1:21 Naye atazaa mwana nawe utamwita jina lake Yesu,  yeye ndiye atakayewaokoa watu wake na dhambi zao.
 Pasaka ya kwanza ilimhitaji mwanakondoo asiye na ila yaaani asiye na kosa wala jeraha na ya pili inamhitaji mtu asiye na ila, uovu wala jeraha katika maisha yake ndio Yesu Kristo wa Nazareti. Kwamba hakuwa na uovu haikuthibitishwa na wanafunzi wake( maana wangemtetea) bali alithibitisha Pilato mwenyewe.
Mathayo 27:24 …mimi sina hatia katika damu ya mtu huyu mwenye haki… pia Luka 23: 22 … huyu ametenda uovu gani?....
Kwa hiyo Pasaka ni sikukuu ya ukombozi wa wanadamu si kuwaokoa tu kutoka dhambi bali kuwakomboa kutoka maangamizi ya Yule muovu Ibilisi pamoja na mateso yake maana Bwana Yesu aliteswa ili wanadamu wasiteseke akawa mtu wa huzuni wanadamu wawe na furaha na amani tele. Isaya 53 inafafanua vizuri kabisa mateso aliyopata Bwana yesu kwa ajili ya mwanadamu.
Maombi wakati wa Pasaka
Yamfaa mtu aombe kuokoka yaani amkiri Bwana Yesu Kristo wa Nazareti kuwa Bwana na mwokozi wa Maisha yake. Amtwike mizigo yake.
Mathayo 11:28. Njooni kwangu, ninyi nyote msumbukao na kuelemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.
 Baada ya kuokoka na kwa mwamini WAKATI WA PASAKA NDO MAJIRA MUHIMU SANA KWA MKRISTO NA YAMPASA  AOMBE MAMBO MUHIMU ZAIDI NA SI TU YALE ANAYOAMINI BWANA ATATENDA BALI YALE ANAYOHITAJI. Aombe mambo ambayo hayakuwezekana kwa miaka mingi lakini sasa autazame msalaba mahali ambapo Bwana Yesu alitamka alikamilisha wokovu.  Naandika hivi kwa kumaanisha kwa sababu kuna waamini wanaomba lile waloamimini Bwana anaweza kutenda kwa hiyo kama imani yake ni ndogo basi ataomba vitu vidogo vidogo tu, lakini aombe mambo anayohitaji yatokee, na Bwana atayafanya kwani aliwekwa msalabani kwa ajili ya mwanadamu siteseke tena.
Wako katika safari,
Mwl Peter Kapagi

Wednesday, 27 March 2013

Maombi kama mazungumzo na Mungu


Luka 11.1 - "Bwana, tunakuomba utufundishe kusali kama Yohane mbatizaji alivyowafundisha wanafunzi wake."
Luka 18.1 - Yeye akawaambia mfano, kama bado zinahitajika ili kuomba na si kutoa juu:
Je, ni maombi?
Kuwa na maisha ya kiroho na nguvu ya kiroho, sisi ni hai kwa kushirikiana na Baba wetu wa mbinguni. Ingawa ni enea mawazo yake, hata wakati sisi kufikiri kuhusu kazi yake, neema yake na baraka, tunahitaji kuwa na ushirika na Mungu, ni lazima kugeuka kwake kwa ushauri juu ya mambo ya maisha ya kila siku.
Maombi ni wa ufunguzi wa moyo kwa Mungu kama rafiki. Hakuna haja ya ugavi wa maombi ya Mungu, sisi, lakini tunaweza kuchukua kwa moyo. Sala haina kuleta Mungu kwetu, lakini huleta sisi na Mungu. Watu zaidi ya miaka ya nyuma aliamini Mungu, na kutamani kwa ajili yake. Wao waliona kuwa walihitaji uhusiano na Mungu. Mpaka karne iliyopita, kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia imeleta kubwa kugeuka. Watu hakuna tena haja ya Mungu. Lakini mmoja anahisi instinctively kwamba mahitaji ya maombi, ni indelibly encoded katika moyo wa binadamu katika wakati wa haja kubwa au hatari kwa mtu yake mara nyingi anarudi.
Maombi ni nadra ushirika kati ya mtu wa kawaida na utukufu wa nafasi, Muumba wa ulimwengu. Katika sala sisi uzoefu na uwepo wa Mungu hapa duniani. Maombi ni mazungumzo kati ya mtu na Mungu: Mtu sasa mawazo yake kwa Mungu, na Mungu ni kusubiri majibu. Maombi ni kinga ya nafsi, kujenga imani kwa makusudi iimarishwe connections na chanzo cha nguvu na hekima. Yesu Kristo ni mfano wetu na tafsiri yetu ya asili na alisema na umuhimu wa maombi. Maombi ya Mungu maswali na kuthibitishwa na maneno ya manabii wa Agano la Kale.
Yeremia 33.3 - Call me na I'll jibu, nami nitakuonyesha siri kubwa, ambayo hamjui.
1 Wathesalonike 5.17 - daima kuomba. Aidha, ni muhimu pia kina maombi binafsi.
MASHARTI kusikia maombi yetu
1 Maombi ya imani.
Ni uthibitisho wa ndani kwamba Mungu na kwamba anatupenda na anataka sisi kuishi maisha ya kwamba tunataka kudumisha urafiki.
Waebrania 11.6 - Bila imani alifanya umaarufu wake hakuna faida moja. Yeye ajaye kwa Mungu lazima aamini kwamba Mungu ni zawadi na kwamba wale wanaoomba.
2 Sala katika Kristo Yesu.
Mungu anakubali yetu kwa ajili ya wema ubora wetu, na uaminifu. Sisi ni katika mtazamo wa Mungu dhambi sana. Mungu anakubali nasi katika Yesu Kristo.
Yohana 14:06 - "Mimi ni Njia, Kweli na Uzima," Yesu akajibu. "Hakuna mtu haji kwa Baba ila kwa kupitia kwangu.
Matendo 4.12 - katika hakuna mtu mwingine kuna wokovu hakuna - watu katika dunia ni kupewa jina jingine, ambayo sisi tunaweza kuokolewa! "
Yohana 14,13-14 - chochote mtakachoomba kwa jina langu, mimi, ili Baba atukuzwe ndani ya Mwana.
3 Kutambua na mapenzi ya Mungu.
Wakati kuwasilisha maombi yangu kwa Mungu, daima ambatisha ya Kristo "si mapenzi yangu bali mapenzi yako yafanyike."
1 Yohana 5.14 - Hii ni ujasiri tulio nao ni: Kila mara sisi kuomba kwa ajili ya kitu katika mapenzi yake, yeye hutusikiliza.
4 wakati, mahali na njia ya maombi.
Yesu alionyesha yetu kwa mfano kwamba ni vizuri kuomba katika sekta binafsi na hasa wakati wa asubuhi. Katika sala ya asubuhi, mtu anapata nguvu ya kiroho kwa siku. Basi, na bora kutekeleza majukumu yao, na kushikilia nje ya majaribu. Kuwatumikia wengine kwa uaminifu na wajibu wa kuamua.
Mathayo 6.6 - Badala yake, wakati wa kuomba, kwenda katika chumba yako, kufunga mlango na umwombe Baba yako ambaye ni siri.
Marko 1.35 - Katika asubuhi aliamka muda mrefu kabla ya alfajiri na kwenda nje. Akaenda mahali pa faragha, akaomba huko.
Kama sisi mbinu katika maombi kwa Mungu Mkuu ulimwengu, tunapaswa kufanya wazi kwa mtazamo wao. Ni nzuri kwa kupiga magoti maombi binafsi, hasa karibu na macho yako na mikono clasp. Mwisho wa maombi ya kusema: "Amina."
Daniel 6.10 - alipiga huko mara tatu kwa siku na kuomba kwa Mungu wake na kumpa sifa kama kabla.
5 Kwanza, ya kusamehe wengine.
Bwana Yesu katika sehemu nyingi umeonyesha kuwa mwanzo sisi kuwasamehe wengine.
Mathayo 5, 23-24 - hiyo kama kuletwa zawadi yako mbele ya madhabahu na hapo ukakumbuka kwamba ndugu yako ana ugomvi nawe, iache sadaka yako mbele ya madhabahu na kwenda kwanza ukapatane na ndugu yako. Na kwa hiyo katika "Baba yetu" ni maneno, na utusamehe makosa yetu kama nasi tunavyowasamehe waliotukosea.
6 ya aina ya msingi ya maombi.
1 Timotheo 2,1 - Kwanza, tafadhali, kushikilia maombi na sala, na, maombezi na shukrani kwa ajili ya watu wote, kwa ajili ya wafalme na ngazi zote mwandamizi, tupate kuishi maisha ya utulivu na amani pamoja na uchaji wa Mungu na mwenendo mwema.
Wrong mawazo kuhusu maombi
Hata sala ina sheria yake na hali ya kuwa walifuata. Yesu Kristo kama mfano wetu, kwa maombi mkubwa alisema na sababu kadhaa, kwamba kuzuia kusikia maombi.
1 sahihi sala, mu chanted kujifunza kwa moyo.
Maombi ni mazungumzo na Mungu, na haipaswi kujifunza na kurudia tena na tena. Hata sala ya "Baba yetu". Basi, Kristo alisema, kama kielelezo.
Yeremia 29,12-13 - Wakati simu yangu na kuja kwangu kwa maombi, mimi kusikia wewe. Nanyi mtanitafuta na kupata mimi wakati mnanitafuta Mimi kwa moyo wako wote.
2 sahihi kwa muda mrefu na verbose sala.
Mathayo 6.7 - Hivyo, wakati kuomba, wala kusema maneno kama tupu wapagani ambao wanadhani wao kuwa habari kwa ajili ya maneno yao. Maombi ni si kujaribu kuwafahamisha Mungu, lakini badala - kumwambia mawazo yao na maombi na kisha kujaribu kutambua na ufumbuzi.
3 Wrong ni gwaride kuvutia ya maombi.
Mathayo 6.5 - Pia, wakati wa kuomba, msiwe kama wanafiki. Wao ni furaha ya kusimama katika maombi katika masinagogi na mitaani pembe kuonyeshwa mbele ya watu. Kweli nawaambieni, hao wamekwisha pata tuzo yao.
4 haina maana sala kwa watu wa Mungu na wafu.
Ufunuo 19.10 - basi mimi akaanguka mbele ya miguu yake, mimi ibada yake, lakini yeye aliniambia: "Jihadharini, je, mimi ni mtumishi wa Mungu, kama wewe na ndugu zako walio na ushuhuda wa Yesu Mwabudu Mungu.!!"
Hatuna hata kuabudu malaika basi binadamu peke yake, hata kama ni alitangaza kuwa mtakatifu.
5 Hatuwezi kulazimisha mawazo yao kwa Mungu na mapenzi yake.
Kwa hiyo, maombi ya mfano ni maneno:
Mathayo 6.10 - "Utakalo lifanyike kama mbinguni na duniani."
Mathayo 26.42 - "Baba yangu, kama haiwezekani kikombe hiki yangu, lakini mimi kukinywa, basi ni kuwa wako!"
6 Ni mbaya wakati mtu pays Mungu tu wengine muda wake wakati wa uchovu.
Marko 1.35 - Katika asubuhi aliamka muda mrefu kabla ya alfajiri na kwenda nje. Akaenda mahali pa faragha, akaomba huko.
Yesu aliomba mara kadhaa kwa siku kwa sababu yeye hakusita kuamka mapema zaidi. Vile vile, Daniel aliomba mara tatu kwa siku angalau.

Scholarship Available here

http://www.manchester.ac.uk/international/finance/equity-and-merit/

Equity and Merit Scholarships for students from developing countries

Equity and Merit Scholarships aim to assist talented but economically disadvantaged students from some of the world’s poorest countries. The scholarships are jointly funded by the University and its alumni. The University waives the tuition fee in full and the generosity of alumni covers students' living costs and flights to the UK.

Sunday, 24 March 2013

Huyu ndiye Aliyeigiza Filamu ya Yesu

Filamu ya Yesu imekuwa na maajabu, imegusa hisia za watu na kufanikisha kupenyeza injili kwa kuakisi kabisa maisha ya Yesu, Ajabu wengine wamefikiri aliyeigiza (Brian Deacon) ni BWANA YESU KRISTO MWENYEWE. Ndo sababu ukipita nyumba nyingi utaona watu wabandika picha za muigizaji huyo wakijua ni Yesu na wengine wameziogopa picha hizo hata kuziabudu. Nimefurahi kukuletea leo UMJUE MUIGIZAJI wa filamu ya Yesu. Habari zote ni kwa msaada wa gospelkitaa.blogspot.com na mtandao kwa ujumla wake.Endelea kubarikiwa.



Brian Deacon akiigiza kama Yesu msalabani.
Ikiwa leo ni Ijumaa kuu,siku ambayo wakristo ulimwenguni wanakumbuka mateso ya mkombozi wa ulimwengu Yesu Kristo aliyekuja duniani takribani miaka 2000 iliyopita.Gospel kitaa imeamua basi kuwaletea historia ya mtu ambaye ameigiza filamu ya Yesu inayofahamika kwa jina la ''JESUS'' ambayo iliigizwa mnamo mwaka 1979 huko nchini Israel, GK imeamua kufanya hivi baada ya kuona ni kwa jinsi gani filamu hiyo imekuwa ikigusa maisha ya watu wengi kiasi kwamba baadhi ya watu wanasahau kwamba mtu aliyemo kwenye filamu hiyo ni mwigizaji tu na siyo Yesu.hata yeye amekiri kwamba wakati wa uigizaji alikuwa akisuluhisha mambo yaliyokuwa yakijitokeza yeye na waigizaji wenzake baada ya wao kusahau kwamba yeye si Yesu bali anaigiza tu. KARIBU.

Brian Deacon ndani ya filamu ya ''JESUS''
Brian Deacon ndio jina lake mwigizaji huyo ambaye ni mwingereza aliyezaliwa mnamo tarehe 13/02/1949 huko Oxford nchini Uingereza akiwa ni mtoto wa pili katika familia yao baba yake akiwa fundi makenika na mama yake akiwa ni nesi ndoa yake ya kwanza na Rula Lenska ilivunjika ambapo alizaa na mkewe huyo binti yao aitwaye Lara Deacon,ndoa yake ya pili alioana na mwanamama Natalie Bloch mnamo mwaka 1998 mpaka sasa wapo kwenye ndoa hiyo.
Aliigiza filamu ya Yesu ambayo pia ilimfanya aokoke mara baada ya kuitazama akiwa na miaka 30,baada ya kupita kwenye mchujo mkali wa waigizaji zaidi ya elfu moja ambao walifanyiwa mahojiano huku 260 wakijaribishwa kuigiza(screen test)kuona kwamba wanafaa akiwa ni mwingereza pekee kati ya waigizaji Waisrael walioingia kwenye usaili huo akiwa chini ya kampuni iitwayo New shakespears ambako alikuwa akifanya sanaa za majukwaani na uigizaji.

Brian Deacon miaka iliyofuatia baada ya kuigiza kama Yesu.

Amesema kabla ya kuchaguliwa mtihani wake wa kwanza ulikuwa kutoka kwa wakala wake aliyemvunja moyo kwakumweleza hadhani kama yeye(Brian)atafaa kwenye kumwigiza Yesu,lakini anasema alifanikiwa,baada ya hapo akawa na wakati mgumu kutoka kwa watu ambao kila mmoja alikuwa anajaribu kumweleza jinsi anavyotakiwa kuigiza,sauti yake na mambo mengine,ingawa yeye alisema nitatumia sauti yangu na maelezo kutoka kwa muongozaji.Amesema wiki tatu kabla hawajaanza kurekodi filamu hiyo alisoma kitabu cha Luka mtakatifu zaidi ya mara 20 kwakuwa filamu hiyo imenukuliwa kutoka kitabu hicho ambapo Brian amesema kusoma kwake kulimpa nguvu sana na moyo wa kuigiza filamu hiyo na kuweza kumfahamu vyema Yesu kuwa ni mtu wa aina gani.

watu wakiangalia filamu ya Yesu ambayo bwana Brian Deacon ni mwigizaji mkuu.

Katika miezi saba waliyochukua kuigiza filamu hiyo Brian amesema,walikuwa wanaigiza kwa masaa mengi kuanzia saa kumi za alfajiri mpaka mwisho wa siku kiasi kwamba wakati mwingine aliwaambia wenzake kwamba wamsaidie kwani  amechoka sana hajui kwamba angeweza kuigiza kwa siku hiyo lakini anasema alikuwa anashangazwa na nguvu za ajabu alizokuwa akizipata na kuendelea kuigiza ingawa wakati huo nasema alikuwa mkristo jina wa kanisa katoliki,alikuwa anauwalakini kuhusu mafundisho na huduma ya Yesu kwa ujumla,siku moja wakati anaigiza alikuwa anawaombea watu mara mwanamke mmoja alishika mkono wake kumbe alikuwa na mapepo alimuombea na mapepo yalimtoka mwanamama huyo.


Siku nyingine waliokuwa wakiigiza kama wanafunzi wa Yesu wapatao 12 wakiwa ndani ya basi walikuwa wamepanga kugoma kutokana na malipo waliyokuwa wakipata cha ajabu Brian anasema director alikuja kumuomba yeye(Brian)azungumze nao warejee kazini akashangaa akamwambia mimi sio Yesu ni Brian Deacon,akaamua kuzungumza nao,baada ya masaa 36 walikubali kurudi kuendelea na kazi
Amesema mtihani mwingine ni siku alipokuwa hotelini Tel Aviv ghorofa ya 18 usiku mara kukawa na moto hotelini hapo baada ya mwingereza mmoja aliyekuwa akivuta sigara kusahau kuizima hivyo kusababisha moto,lakini anasema bahati nzuri hakuna aliyejeruhiwa ila walifanya kazi siku inayofuatia muda mrefu bila muongozaji kujali kwamba hawakulala vyema usiku.
watumishi wa Mungu wakiwa njiani kwenda kuonyesha filamu ya Yesu katika uinjilisti huko Kongo.
Amesema siku hiyo mmoja wa waigizaji anayeitwa Tom Panella alianzisha mada kwa kusema moto uliokuwa umetokea ni hila za shetani,na kusababisha mjadala wa muda mrefu ni vipi shetani anahusishwa kwenye swala hilo lakini jibu likawa,shetani hataki filamu hiyo irekodiwe ndio maana analeta hila zake.haikuwa kazi rahisi kurekodi filamu hiyo na pia si ujuzi wa kufurahia,baada ya kumaliza kurekodi kwa takribani miezi 18 ilianza kuonyeshwa kwa baadhi ya watu na ndipo hata yeye kwa mara ya kwanza akaona ni kwa jinsi filamu hiyo ilivyonanguvu,ukweli na kugusa mioyo ya watu.


Baada ya filamu hiyo Briana anasema alirudi kuigiza majukwaani na kwenye runinga, ambapo kwa miaka zaidi ya 30 sasa tangu kutoka filamu ya Yesu tayari imetazamwa na watu zaidi ya bilioni tatu katika nchi 233(kwa takwimu za mwaka 2001),zaidi ya watu milioni 117 waliamua kubadilisha maisha yao na kumpokea Yesu,filamu hiyo ambayo ilitengenezwa chini ya Campus Crusade for crusade ambao kwasasa wanaitwa Life Ministry pia nchini Tanzania wapo chini ya mkurugenzi Dismas Shekhalage.ambapo tayari imetafsiriwa katika lugha zaidi 500 huku nyingine zaidi ya 200 zikiwa njiani kutafsiriwa.

Brian anawaambia watu kwamba yeye ni mwigizaji tu na sio Yesu kama watu wengine na kuwataka watu hao kujua hivyo ambapo anasema ameendelea kupata barua mbalimbali za kumpongeza na kumshukuru kwa kazi nzuri aliyofanya kwenye filamu hiyo,ambapo kwa upande wake anasema anayo nakala ya filamu hiyo kwenye maktaba yake nyumbani kwao Uingereza,ambapo kwa takribani miaka 20 filamu hiyo imekuwa ikitazamwa duniani kote na kubadilisha maisha ya watu.

kati ya filamu alizowahi kushiriki ni pamoja na A zed & Two Noughts ya mwaka 1985,The Feathered Serpent ya mwaka 1976-1978 na Tamthilia ya iitwayo Lillie iliyoigizwa mwaka 1978 akitumia jina la Frank Miles.
Huyo ndiye Brian Deacon mwigizaji mkuu wa filamu ya ''JESUS''iliyoigizwa mwaka 1979 huko nchini Israel.
habari kwa msaada wa mtandao.

Thursday, 21 March 2013

Tanzania kuunda kamati baina ya dini kuhakiki sheria za kuchinja


Na Deodatus Balile, Dar es Salaam
Februari 19, 2013
  •  
Wakiristo wa Tanzania wamezuiliwa kwa muda kuchinja wanayama kwa ajili ya matumizi hadi serikali iteue kamati baina ya dini kutafuta ufumbuzi wa suala hili la uchinjaji kati ya Waislamu na Wakristo.
  • Mchinjaji akionyesha nyama halali kutoka machinjioni kwenye maeneo ya Mtoni Mtongani jijini Dar es Salaam. [Deodatus Balile/Sabahi] Mchinjaji akionyesha nyama halali kutoka machinjioni kwenye maeneo ya Mtoni Mtongani jijini Dar es Salaam. [Deodatus Balile/Sabahi]
Agizo hilo limetolewa baada ya miezi zaidi ya mitatu ya wasiwasi na mapigano katika mikoa ya Geita na Mwanza kuhusu uchinjaji wa wanyama.
"Kwa kawaida Waislamu [ndio ambao huchinja wanyama] katika nchi hii, lakini tuna mzozo huu na nimeunda kamati ya viongozi wa dini kutafuta suluhisho la kudumu," Waziri Mkuu Mizengo Pinda aliwaambia waandishi wa habari Jumamosi (tarehe 16 Februari) baada ya mkutano na viongozi wa Kiislamu na Kikristo katika mkoa wa Mwanza. "Kwa hiyo, [wakati] kamati hii itakapokuwa ikifanya kazi kwa juhudi kupata suluhisho la kudumu, Waislamu wataendelea kufanya kazi hii kwa ajili yetu sisi sote."
Kutoafikiana kulifikia kilele huko Buseresere tarehe 11 Februari wakati vijana wa Kiislamu walipopambana na kikundi cha Wakristo ambao walichinja ng'ombe na mbuzi wawili kwa ajili ya kuuza katika soko la ndani. Mapambano hayo yalisababisha mchungaji Mathayo Machila kukatwa kichwa, na kujeruhi wengine kadhaa na mali muhimu kuharibiwa.
Kaimu Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Geita Paul Kasabago alisema watu watatu wamekamatwa kuhusiana na tukio, akiwemo Mchungaji Pastor Isaya Rutta, ambaye alichinja mifugo katika viwanja vya kanisa. Watu wengine wawili wanaoshikiliwa ni wa upande wa kanisa la Rutta. Kasabago alisema watashitakiwa kwa kukiuka sheria za afya, wakiwachochea wananchi na kusababisha kifo cha Machila.
Polisi bado haijamkamata yeyote anayetuhumiwa kufanya vurugu dhidi ya Machila.
"Sheria inasema kwamba mnyama yeyote anayechinjwa aidhinishwe na mganga wa mifugo mwenye sifa [ili kuhakikisha] anafaa kuliwa na binadamu," Kasabago aliiambia Sabahi. "Kinyume na hivyo, unahatarisha afya za walaji."
Rais Jakaya Kikwete alilaani vurugu, akisema vita vya kidini sio maslahi mazuri ya Tanzania. "Tumeishi kwa zaidi ya miaka 50 bila ya kuwa na ugomvi unaohusiana na imani zetu kama Waislamu na Wakristo," alisema huko Dodoma.
"Ni ujinga kugombana kwa ajili ya haki ya kuchinja," alisema.
Kikwete alimtuma Waziri wa Mambo ya Ndani Emmanuel Nchimbi huko Buseresere kusuluhisha jamii zenye mgogoro kuhusu haki ya kuchinja wanyama.
Nchimbi aliiambia Sabahi kwamba hali sasa imedhibitiwa, kwa kuwa mazungumzo yanaelekea katika "mwelekeo mzuri". Aliomba kwamba wale wanaohusika na vurugu watakabiliwa na adhabu za kisheria.

Utoaji kazi za machinjioni waibua maswali ya kidini

Nchini Tanzania machinjio yanamilikiwa na halmashauri za miji. Kwa miaka 50, ilikuwa ni desturi kwa machinjio kuwa na wafanyakazi wa Kiislamu, kufuatia miongozo ya Kiislamu. Hatimaye nyama huuzwa katika mabucha kwa ajili ya uuzaji wa rejereja.
Juvenary Mwaikambo, mwenye umri wa miaka 46, ambaye huuza nguruwe katika Banana Bar huko Dar es Salaam, alisema anajua machinjio mawili maalumu ya nguruwe ambayo Waislamu hawatachinja, lakini watu wachache sana wanayatumia.
"Ninajua ni kinyume cha sheria kuchinja nguruwe nyumbani, lakini ni ghali sana kuchinjia machinjioni," Mwaikambo aliiambia Sabahi. "Wanatoza shilingi 5,000 (Dola 3.10) kwa ajili ya kuchinja na mganga wa mifugo anapaswa kuidhinisha nyama kwa kuigonga muhuri. Kama [mganga wa mifugo] asema haifai kwa matumizi ya binadamu, inatakiwa kufukiwa … kuna kero nyingi katika machinjio."
Aran Mashimba, mwenye umri wa miaka 48, mkazi wa Buseresere, alisema suluhisho la mgogoro huo ni kuwa na machinjio tofauti kwa ajili ya kuwahudumia wakazi wa imani zote.
"Sio tu kwa ajili ya kuwaridhisha waumini wa Kiislamu, ni zaidi ya hilo," Mashimba aliiambia Sabahi. "Uchinjaji wa nyama ni tasnia kubwa ambayo inazalisha ajira. Kufanyika na Waislamu tu ni kutunyima [Wakristo] fursa za ajira."
Sheikh Suleiman Mtindi wa Mwanza, ambaye alishiriki katika mkutano wa pamoja uliofanyika Jumapili pamoja na Pinda, pia alipendekeza kutenganisha machinjio. Pinda alilikataa wazo hilo, hata hivyo, alisema litasababisha mgawanyo mkubwa.
Chanzo; http://sabahionline.com/sw/articles/hoa/articles/features/2013/02/19/feature-02