m

"If you want to conquer fear, don't sit at home and think about it. Go out and get busy. "

-- Dale Carnegie, motivational expert

Wednesday, 7 September 2016

Wakonta Kapunda, binti aliyeandika kwa ulimi, apata kifaa


Wakonta Kapunda
Unamkumbuka Wakonta Kapunda? Binti Mtanzania mwandishi wa miswada ya filamu anayeandika kwa kutumia ulimi wake?
Wakonta alipata ajali siku ya mahafali yake ya kidato cha sita miaka minne iliyopita. Ajali hiyo ilimuacha akiwa amepooza kwanzia shingoni kushuka chini na kumfanya kutoweza kutumia mkono yake kuandika.
Wakonta Kapunda
Wiki kadhaa zilizopita, BBC iliporusha habari yake Msamaria Mwema mmoja aliguswa kumsaidia
Kupitia kipindi cha televisheni cha Focus on Africa katika BBC World Service, mwanadada Olivia Soko kutoka Afrika ya Kusini aliguswa kufanya kitu kumsaidia Wakonta.
Wakonta Kapunda, msichana anayeandika kwa ulimi
Akiwa mkurugenzi wa kampuni ya Whirlmarket Technologies, Olivia alijitolea kutoa msaada wa programu ya kompyuta iitwayo Nuance Dragon Naturally Speaking.
Jinsi Program hii inavyofanya kazi ni kwamba mtumiaji yeye anazungumza anachotaka kukiandika kupitia kipaza sauti chake halafu programu hii inaandika yenyewe katika kompyuta ya mtumiaji
Wakonta alijaribu kuitumia jana, akaifurahia, lakini bila shaka atahitaji muda zaidi ili aizoee vizuri.
Familia yake pia imefurahishwa sana na msaada huu.
Chanzo; bbcswahili.com

Trump aungwa mkono na wanajeshi wastaafu 88

Tofauti na watu wanavyobeza nguvu ya Mgombea urais wa Republican Bw. Trump BBC inaripoti kwamba anaungwa mkono na wanajeshi wastaafu 88.
Donald Trump
Image captionDonald Trump
Mgombea wa chama cha Republican Donald Trump ameungwa mkono na viongozi 88 wa zamani wa jeshi katika barua ya wazi kulingana na kampeni yake.
Kundi hilo lenye majenerali wastaafu pamoja na admirali waliamua kuwa kiongozi huyo ana uwezo wa kuwa kamanda mkuu wa jeshi.
Bwana Trump ambaye ameangazia maswala ya wazee wakati wa kampeni yake alitaja uungwaji mkono huo kuwa heshima kubwa.
Hatahivyo amepinga madai ya utumizi mbaya kuhusu ufadhili wa kisiasa kwa afisa mmoja wa Florida.
Gazeti la The Washington liliripoti siku ya Jumatatu kwamba mwaka 2013,mwanasheria mkuu wa Florida Pam Bondi alipendekeza mashtaka ya udanganyifu dhidi ya chuo kikuu cha Trump.
Lakini alisitisha uchunguzi huo baada ya mchango wa dola 25,000 kutolewa na wakfu wa Donald Trump kusaidia kampeni yake ya kisiasa.
Bwana Trump alipigwa faini kwa kuwa hakutangaza mchango wake kwa halmashauri ya ushuru nchini Marekani.

Kimungu mke (Goddess) achoka sauti

Hakika Mungu mkuu atabaki kuwa Mungu kwani mwimbaji Beyonce yule aliyejiita kimungu mke( goddess) kule marekani na kuanzisha kitabu chake alichofananisha na biblia kiitwacho beyble achoka sauti na kushauriwa na madaktari kupumzisha sauti. Je ni Mungu gani anayeshauriwa na wanadamu juu ya Afya yake akakubali?Habari kamili na bbcswahili;-

 

Beyonce ashauriwa kupumzisha sauti yake


Beyonce ashauriwa kupumzisha sauti yakeImage copyrightV
Image captionBeyonce ashauriwa kupumzisha sauti yake
Mwanamuziki Beyonce ameahirisha tamasha lake la New Jersey kwa jina World Tour baada ya madaktari kumshauri kupumzisha sauti yake.
Msanii huyo ambaye alisheherekea siku yake ya 35 ya kuzaliwa siku ya Jumapili alitoa taarifa akisema tamasha hilo halitafanyika mnamo tarehe 7 mwezi Octoba.
Hatahivyo ataendelea na tamasha nyengine katika miji ya Los Angeles,Houston,New Orleans na Atlanta kama ilivyopangwa.
Ziara hiyo ambayo inalenga kuuza albamu yake mpya Lemonade,ilianza mjini Miami mnamo tarehe 27 mwezi Aprili.
Ilitarajiwa kukamilika Nashvile mnamo tarehe 2 mwezi Octoba,lakini sasa inaonekana kwamba New Jersey itaanda tamasha lake la mwisho

Binadamu mzee Zaidi duniani huyu hapa


Mungu wa ajabu, wakati wengi wakifikiri wazee zaidi ni wale wenye miaka 80 na 90 shirika la habari la uingereza(bbc) linaripoti juu ya mzee wa miaka 145 aliyepo Indonesia

Mbah Gotho
Mzee huyu kwa jina Mbah Ghoto kutoka Indonesia anaamini ndiye binadamu mzee zaidi kuwahi kuishi duniani.
Anasema ameishi muda zaidi kushinda wake zake wanne, ndugu zake 10 na wanawe wote.
Anatokea kisiwa cha Java ya Kati.
"Huwa najaribu kuwa mvumilivu na kuamini kuwa kuna watu watakaonitunza," ameambia BBC.
"Nimeishi muda mrefu kwa sababu nina watu wanaonipenda na kunitunza."
Yeye bado huvuta sigara.
Mjukuu wake Suryanto anasema kwa mujibu wa stakabadhi rasmi za serikali, Mbah Gotho ana miaka 145. Alizaliwa 31 Desemba 1870.
"Tunaamini stakabadhi hizi ni halali, kwa mujibu wa nyaraka rasmi za serikali. Tunaamini tarehe yake ya kuzaliwa ni sahihi," anasema afisa wa serikali Wahyu Wiyanto.
Indonesia ilianza kunakili rasmi kuzaliwa kwa watu 1900 hivyo ni vigumu kuthibitisha tarehe kamili ya watu waliozaliwa kabla ya hapo.
Na kumewahi kutokea makosa awali.
Lakini Mbah Gotho anachukuliwa kama shujaa eneo analotoka.
"Siku ya Uhuru alikuwa akialikwa kusimulia yaliyotokea wakati wa vita. Anaweza kusimulia kuhusu vita dhidi ya wakoloni kutoka Japan na Uholanzi," anasema Wahyu Wiyanto.
Mjukuu wake anasema mzee huyo huwa hana masharti mengi na huwa haitishi chakula maalum.
"Kitu pekee alitutaka tufanye ni kununua jiwe la kaburi lake," anasema.
Mzee huyo anasema kwa sasa anaishiwa na nguvu na hawezi kutarajia aishi muda mrefu zaidi.
"Sina nguvu kama zamani. Hata kutembea ni shida. Nilikuwa mkulima na nilivua samaki mtoni. Sitaki kuendelea kuishi sana, ndio maana nimeandaa kaburi. "Ili nikifariki, kila kitu kiwe tayari," anasema.
"Kwa sasa nataka tu kufariki, lakini wakati wangu haujafika bado."
Mtu ambaye aliishi miaka mingi zaidi duniani kulingana na Guinness ni Jeanne Calment kutoka ufaransa ambaye aliishi miaka 122 na siku 164 . Aliaga dunia mwezi Agosti mwaka 1997.

Sherehe za kufungwa kwa Olimpiki Rio

Mashindano ya Olimpiki ya Rio yamemalizika rasmi, yakihitimisha siku 16 za matukio ya raha na karaha . Wakazi wa Rio walivumilia mvua na upepo mkali kushuhudia sherehe za mwisho za kufungwa kwa mashindano hayo.

Brasilien Olympische Spiele Rio 2016 21 08 Abschlussfeier
Sherehe za kufunga michezo ya Olimipiki ya Rio uwanjani -Maracana - Rio de Janeiro, Brazil -
Wakicheza densi aina ya Samba katika mitindo ya Ki-Brazil, wanamichezo mbali mbali pamoja na mashabiki waliaga mashindano hayo kwa mbwembwe za aina yake.
Wanariadha walimiminika katika uwanja huo wakipeperusha bendera za nchi zao katika msafara wa kuvutia huku wanariadha wa Brazil wakivalia viatu vilivyokuwa na nyayo zilizokuwa zikiwaka rangi tofauti kama vile nyekundu, nyeupe na samawati na mwanamiereka wa Tongan Pita Taufatofua akicheza jukwaani akiwa amevalia skati huku disco joka akicheza muziki na kuleta kumbukumbu ya wakati alipovutia umati mkubwa wakati alipopeperusha bendera ya nchi yake wakati wa sherehe za ufunguzi.
Kulingana na Rais wa Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki, Thomas Bach, mashindano hayo yalikuwa ya kuvutia katika mji wa kupendeza:
Kumbukumbu za michezo hiyo
Hata hivyo, michezo hiyo pia ilikuwa na kumbukumbu kwa wanariadha kutoka Brazil na wale wa nchi nyingine kote ulimwenguni. Timu ya kandanda ya Brazil iliicharagaza Ujerumani na kujishindia nishani ya dhahabu miaka miwili baada ya kushindwa kwa mabao 7-1 katika fainali ya kombe la dunia na kuwahuzunisha mashambiki wengi katika taifa hilo.
Brasilien Olympische Spiele Rio 2016 21 08 Abschlussfeier Thomas Bach
Rais wa kamati ya kimataifa ya Olimpiki Thomas Bach akitoa hotuba wakati wa sherehe za kufungwa kwa michezo hiyo katika uwanja wa Maracana huko Rio de Janeiro
Mwanasakarasi wa Marekani, Simone Biles, alijishindia dhahabu 4, mwogeleaji Michael Phelps akaongeza nishani nyingine 5 na Usain Bolt akiwa ni mkimbiaji bora zaidi duniani akijishindia nishani 3 za dhahabu siku chache kabla ya kusherehekea siku yake ya kuzaliwa atakapohitimu miaka 30.
Baadhi ya changamoto
Lakini pia kulikuwa na matukio ambayo hayakuridhisha kama vile tukio la kutunga la mwogeleaji wa Marekani, Ryan Lochte, la kuvamiwa na maswala kama vile vidimbi vya maji katika mashindano hayo ya olimpiki kugeuka rangi kutoka samawati hadi kijani kibichi.
Sherehe hizo za kufunga mashindano hayo katika uwanja wa Maracana pia zilimaanisha kutimiza jukumu rasmi la kutia saini hatua ya kupokeza bendera kwa Japan itakayoandaa mashindano yajao ya Olimpiki katika majira ya kiangazi ya mwaka 2020.
Kuna matumaini kwamba mashindano ya Japan yatakuwa bora zaidi kuliko yalivyokuwa nchini Brazil lakini pia kuna wasiwasi kwenye nchini Japan iwapo mashindano hayo yatazidi kusambaratisha uchumi wa nchi hiyo ambao umekuwa ukijikokota kwa miaka mingi.
Gavana wa Japan alipokea bendera hiyo kutoka kwa Rais wa Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki, Thomas Bach, na meya wa Rio Eduardo na kuashiria kukubalika Japan kuandaa mashindano hayo mwaka 2020.
Mwandishi: Tatu Karema/AP
Mhariri: Mohammed Khelef

Merkel asema Ujerumani ya sasa ni bora zaidi

Licha ya chama cha CDU kuangushwa vibaya kwenye uchaguzi la kwao la Mecklenburg-Vorpommern kutokana na sera yake ya wahamiaji, Kansela Angela Merkel anasema sera yake ni sahihi na kamwe hatarudi nyuma.

Kansela Angela Merkel akihutubia bungeni siku ya Jumatano (7 Septemba 2016).
Kansela Angela Merkel akihutubia bungeni siku ya Jumatano (7 Septemba 2016).
Vichwa vya habari katika magazeti na ripoti za televisheni na redio mara tu baada ya CDU kushindwa uchaguzi huo wa Jumapili, zilitazamiwa kumrejesha Kansela Merkel nyuma, na hotuba ya leo ilidhaniwa kuwa ingekuwa nyepesi na laini. Lakini hivyo sivyo ilivyokuwa, kwani kwenye hotuba ya bungeni ya leo Jumatano (7 Septemba 2016), ambapo alionekana kusimama imara.
"Hali yetu leo ni bora zaidi kuliko ilivyokuwa mwaka mmoja uliopita kwetu sote. Hapana shaka, bado kuna mambo ya kufanywa. Changamoto kubwa ikiwa kuwarejesha nyumbani wahamiaji ambao hawawezi kubakia hapa na sisi. Na kwa uadilifu kuwahudumia raia wetu, huku tukiwafahamisha kuwa tunapaswa kuwasiaidia wale wenye haki ya kusaidiwa," aliwaambia wabunge.
Katika hotuba hii, ambayo tayari imeshaonesha kuzua mjadala mkali, Kansela Merkel amesema si kweli kuwa mmiminiko wa mamia kwa maelfu ya wakimbizi nchini Ujerumani utapunguza mafao wanayopata raia wazawa wa Ujerumani, hoja ambayo imekuwa ikitumiwa na wapinzani wake wa kisiasa.
Chama chake, CDU, kiliangushwa kwenye uchaguzi wa mwishoni mwa wiki na chama kinachopinga wahamiaji nchini Ujerumani, AfD, katika jimbo la Mecklenburg-Vorpommern, kwa hoja hiyo hiyo dhidi ya wakimbizi.
Wapigakura kwenye jimbo hilo walitumia nafasi hiyo kumuonesha kutokubaliana na sera yake ya kufungua milango kwa wakimbizi na wahamiaji kutoka mataifa yenye Waislamu wengi, hasa baada ya matukio kadhaa ya mashambulizi kwenye miji ya kusini mwa Ujerumani, lakini kwenye hotuba yake ya leo bungeni, Kansela Merkel amesema ugaidi si jambo linalohusiana moja kwa moja na wakimbizi.
Kansela Angela Merkel wa Ujerumani na Rais Tayyip Erdogan wa Uturuki wakiwa kwenye mkutano wa kilele wa mataifa ya G20, mjini Hangzhou, China.
Kansela Angela Merkel wa Ujerumani na Rais Tayyip Erdogan wa Uturuki wakiwa kwenye mkutano wa kilele wa mataifa ya G20, mjini Hangzhou, China.
"Licha ya kuwa tulikumbwa na mashambulizi mabaya ya Ansbach na Wurzburg, ugaidi si jambo jipya lililokuja na wakimbizi kwetu. Hata kama si kila mkimbizi anakuja na dhamira njema, hatupaswi kuwahukumu kijumla-jamala. Kuifanya Ujerumani kuwa salama, ni pamoja na kuwaonesha wengine kwamba wanaadamu wenzetu wanaweza kututegemea sisi wanapokuwa na matatizo," alisema Kansela Merkel.
Makubaliano na Uturuki ni sahihi
Sambamba na hilo, alitetea pia namna anavyoliendea suala la mahusiano kati ya nchi yake na Uturuki, akiwakosoa wale wanaomwambia ameshinda kulaani hatua kali za ukandamizaji zinazochukuliwa na utawala wa Rais Tayyip Erdogan baada ya jaribio la mapinduzi yaliyoshindwa mwezi Julai.
Merkel amesema makubaliano kati ya Umoja wa Ulaya na serikali ya Uturuki yaliyolenga kuzuia mmimiko wa wahamiaji yalikuwa hatua muhimu na inayoweza baadaye kuigizwa kama msingi wa makubaliano na mataifa mengine.
Mdahalo wa jioni ya leo kuhusiana na hotuba hii iliyoshadidia msimamo na muelekeo wa Kansela Merkel kwa masuala ya wakimbizi, usalama, na sera yake ya nje unatazamiwa kuwa mkali sana.
Tayari msuguano ndani ya serikali yake ya muungano umeshadhihirika, huku mshirika wake mkuu, chama cha SPD kikionekana kujipanga kumpiku.
Upinzani mkali pia umo ndani ya chake mwenyewe cha CDU, huku chama ndugu cha CSU kikiwa tangu mwanzoni mbali sana na sera ya wakimbizi ya Kansela Merkel.
Chanzo: dw.de
Mwandishi: Mohammed Khelef/dpa/Reuters
Mhariri: Saumu Yussuf


Sababu ya wanawake marafiki kupata hedhi pamoja


Picha ya mwanamke aliye kwenye hedhi
Image captionPicha ya mwanamke aliye kwenye hedhi
Inaaminiwa kwamba wanawake wanaoishi pamoja hatimaye huwa na mizunguko inayofanana ya kila mwezi ya hedhi. Lakini je hili ni kweli ama ni jambo linalotokea kwa bahati tu?
Dhana kuhusu mizunguko hiyo ya hedhi ni kwamba vichocheo vya mwili vya mwanamke ama homoni vinavyosababisha hedhi kwa lugha ya kitaalamu-pheromones- hufanya kazi kwa wakati mmoja wanapokuwa na uhusiano wa karibu, na hivyo kuwasababisha kupata hedhi kwa wakati mmoja. Wanawake wengi wamejikuta katika hali hii.
"Nadhani suala hili ni kweli ," anasema Emma. "Tukisema ni suala linalojitokeza kwa bahati basi zitakuwa ni bahati nyingi sana ."
Emma, mwenye umri wa miaka 24, anaishi na wasichana wenzake watano katika chuo kikuu. Anasema kwamba katika kipindi cha miezi michache wote walipata hedhi zao kwa wakati mmoja.
"Ni suala linaloaminiwa na wengi," anasema Alexandra Alvergne, profesa wa masuala ya kibiolojia na maumbile ya binadamu katika chuo kikuu cha Oxford.
chati ya hedhi ya mwanamkeImage copyrightISTOCK
Image captionTafiti nyingine, kuhusu binadamu na watu waliowahi kuishi pamoja zinathibitisha kuwa wanawake wanaoishi pamoja hupata hedhi wakati mmoja
Kuna nadharia mbali mbali kuhusu sababu inayoweza kusababisha wanawake wanaoishi pamoja kupata hedhi wakati mmoja.
Utafiti wa Dkt Martha McClintock mwaka 1971 ulidokeza hili huenda lilikuwa ni kwa sababu wanawake waliokuwa wanaishi pamoja walikuwa na uwezekano kwamba homoni za kila mmoja ziliweza kuathiri za mwenzake miongoni mwa marafiki wa karibu.
Na kwa nini basi hili likawezekana? Nadharia ambayo inakubaliwa na wengi ilikuwa ni uwezo wa ushirikiano uliopo baina ya wanawake katika mambo na kwamba huenda walikata kushirikiana kuzuia kugeuzwa kuwa maharimu na mwanamume mmoja.
Kwa kuoanisha mizunguko yao ya hedhi, hii ina maana kwamba mwanamume mmoja aliye karibu nao hangeweza kuwatungisha mimba kwa pamoja kwani wakati mmoja angelikuwa anamwangazia mmoja na kabla amwangazie yule mwingine, kipindi chake cha kuweza kushika mimba kitakuwa kimepita.
Baadhi ya wasomi hivi karibuni waliamua kuchunguza kwa kina iwapo matokeo ya mzunguko wa hedhi kwa wanawake wanaoishi pamoja yanaweza kuwa ni ya kubahatisha.
Waliangalia taarifa za mizunguko ya hedhi walizokusanya katika kipindi cha miaka sita wakiangazia nyani, ambao wanakaribiana sana na binadamu.
" Walipendekeza nadharia mbili," anasema Alvergne. " Moja ni ya kutumia "msisimuko " ambayo pia ilifahamika kama "mpango wa mabadiliko," ambapo wanawake hubadilisha mzunguko ili kuungana na kushirikiana kama kinga dhidi ya mwanamume mbabe.
"Nadharia nyingine ni ya mtu anayeudhi. Ambapo mienendo yake inaweza kuelezwa kwamba inatokana tu na bahati."
WanawakeImage copyrightISTOCK
Watafiti walilinganisha nadharia hizo mbili kulingana na taarifa zinazochunguzwa.
Walibaini kwamba nadharia kwamba kulingana kwa mzunguko wa hedhi unaweza kuelezwa vyema kwa 'mtu wa kuudhi' ambapo ulinganifu ulitokea kibahati tu ndiyo iliyofaa zaidi.
Utafiti zaidi unaweza kufanyika siku zijazo ambao utafichua zaidi ushahidi kuhusu mizunguko ya hedhi ya wanawake. Lakini kwa sasa watafiti wana shaka kuhusu kuwepo utaratibu au sababu inayosababisha hili.
"Labda kusema ukweli, kile tulichokiona ni jambo la kibahati tu," anasema Alvergne.
Tafiti nyengine, kuhusu binadamu na watu waliowahi kuishi pamoja zilionyesha majibu yanayofanana na hayo.
Lakini kulikuwa na tafiti nyingine ambazo hazikupata ushahidi wa wanawake wanaoishi pamoja na kuwa na urafiki kupata hedhi kwa wakati mmoja.
chanzo: bbcswahili.com

Business and Blog Changes

Its time for Change from Kapagi Infomation Institute- KII to Kapagi Enterprise-Ke and our blog/pages to Kapagi pages-Kp

our motto from Habari ni Maisha to Open the new pages/ Fungua kurasa mpya

what we do is to extend more services from education and consulting to IT, Consultancy, news/media and business/sales/products.

Its a matter of time

We are moving to Great and best times ever.