m

"If you want to conquer fear, don't sit at home and think about it. Go out and get busy. "

-- Dale Carnegie, motivational expert

Tuesday, 24 September 2013

Ni somo kwetu, Vigogo wa siasa wawajibika Ujerumani

Wiki iliyopita nilishiriki ujumbe mmoja wa ukurasa wa facebook wa DW ambapo nichapisha kuwa Afrika tunaweza kujifunza siasa kutoka Ujerumani, taifa ambalo wakati wa uchaguzi watu huangalia utaifa zaidi ni kuwa watulivu wakati na baada ya kupiga kura. Hatimaye matokeo yametangazwa na mwanamke shupavu Kansela Angela Markel kuibuka mshindi na chama chake.Matokeo hayo yamepelekea chama cha FDP na uongozi wake kujiuzulu. Hii ni tofauti na hapa Afrika kwani baada ya matokeo wangeingia mtaani na kuzusha vurugu kubwa kupinga matokeo hata kama wameshindwa kihalali. Nikienda mbali zaidi ni kwamba kansela Angela markel pamoja kupata ushindi mzito bado karuhusu mazungumzo na upinzani kuunda serikali ya pamoja. Lengo lao wanasiasa wa Ujerumani ni kuona Ujerumani imara na kuonda maendeleo ya Taifa lao na si matumbo yao, familia na hata maswahiba wao kama ilivyo kwetu Afrika.
Habari zaidi fuatana na DW.DE hapa wanaripoti;
Siasa zimechemsha Ujerumani ambapo viongozi wa vyama mashuhuri vya kisiasa wa chama cha Free Demoktatik FDP wamejiuzulu na uongozi mzima wa chama cha Kijani kujizulu baada ya kushindwa vibaya katika uchaguzi.
Rainer Brüderle akiwa na Philipp Rösler. Rainer Brüderle akiwa na Philipp Rösler.
Kiongozi wa chama cha FDP Phillip Rösler ametangaza kujiuzulu hapo Jumatatu baada ya chama chake kushindwa vibaya kuwahi kushuhudiwa kabla katika uchaguzi wa Ujerumani uliofanyika Jumapili na kusababisha kuenguliwa kwa chama hicho katika bunge la Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani.
Rösler Naibu Kansela anayemaliza muda wake ambaye amejiuzulu kama kiongozi wa chama hicho chenye kupendelea wafanya biashara na waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Guido Westerwelle ni miongoni mwa mawaziri waliopoteza viti vyao katika uchaguzi huo ambapo chama chao kimeboronga vibaya.
Rösler mwenye umri wa miaka 40 ambaye alikuwa pia waziri wa uchumi katika serikali ya Merkel amesema wakati akijiuzulu kwamba huko ni kushindwa vibaya kabisa kwa chama hicho kuwahi kushuhudiwa katika historia.http://www.dw.de/vigogo-wa-siasa-wawajibika-ujerumani/a-17109452

Sunday, 22 September 2013

DINI NA SIASA

Dini kujihusisha na siasa si jambo baya, ni jema sana hasa ikizingatiwa watu waadilifu walio wengi
wanapatikana kwenye dini maana na kazi ya dini ni kufundisha uvumilivu, uaminifu, upendo na heshima kwa Mungu na jamii nzima.
Lakini nikumbushe kuwa katika taasisi moja ya dini ni lazima kutakuwa na makundi tofauti na yenye itikadi na mtazamo tofauti za Kisiasa. Siasa si maandiko ambayo huwalazimisha watu wote wawe na msimamo mmoja juu ya andiko hilo.
Nasema hivi ili kuwaasa baadhi ya viongozi wa dini kulivaa vazi la siasa mwili mzima. Binafsi naamini kiongozi wa dini kazi yao ni Kutoa elimu ya siasa na hata uraia, hapo wafundishe siasa safi, sifa za kiongozi bora na habari ya sera. SI KAZI YA KIONGOZI YEYOTE WA DINI KUWAELEKEZA WATU WAKE KUPENDA AU KUCHUKIA CHAMA FULANI, SI KAZI YA KIONGOZI WA DINI KUWACHOCHEA WATU KUJIUNGA NA CHAMA FULANI CHA SIASA, KAZI YAKE INAISHIA KUWAELEKEZA SIFA ZA SIASA SAFI HALAFU WATU WANAAMUA CHAMA KIPI NI KISAFI.
Nimeshtushwa kwa mara nyingine kushuhudia tena baba yangu na askofu mkubwa kabisa kuchochea watu kuchukia chama fulani, Askofu Kakobe kushiriki kwake katika muungano wa viongozi wa upinzani na kutoa matamshi ya chuki juu CCM pale jangwani, hakika si kazi yake hata kidogo. Watu watakapoyapuuza maneno yake inaweza kuathiri hata juu ya mafundisho yake kwani watu wakizoea kukupuuza katika jambo fulani watakupuuza katika mengine na hapo kutakuwa na athari kubwa ya IMANI. naomba nimkumbushe Askofu juu ya matamko yake 1995 na NCCR, hakuishia hapo akatoa matamko 2000, 2005 na 2010 mara zote matamko yake yameenda kinyume na uhalisia.
Baba askofu kakobe anataka wafuasi wake mimi nikiwa miongozi mwao waamini chama gani cha siasa? NCCR, CHADEMA, CUF, CCM AU CHAMA GANI? Askofu anatuchanganya na matamko yake ya kisiasa. Namshauri kutoa elimu ya siasa na si kuwa mwanaharakati.
Binafsi nimekuwa kiongozi wa dini kanisani na hata kwa wanafunzi hadi ngazi ya chuo kikuu (CASFETA-TAYOMI) lakini sijawahi na siamini kabisa juu ya kuwachochea waumini juu ya chama fulani cha siasa, isipokuwa ninachofanya ni kuwachochea waumini kushiriki siasa safi na habari ya vyama huwaachia waumini uhuru wa kuchagua ni chama gani safi kwa mujibu wa mwongozo wa siasa safi niwapao.

Friday, 13 September 2013

KII Commitment

KII Committed to serve, Moving to reach you in IT solutions Specialized in PC Windows Booting, Program/Software Application Installation, Card designing (Wedding, Graduation, Send off, Business cards and related ceremonies), Poster etc.

Photo: Committed to serve, Moving to reach you in IT solutions Specialized in PC Windows Booting, Program/Software Application Installation, Card designing (Wedding, Graduation, Send off, Business card and related ceremonies), Poster etc.Find Us Now

Saturday, 7 September 2013

Kenya yapiga kura kujitoa katika Mahakama ya ICC

Hayawi hayawi sasa yamekuwa, DW.DE imechapisha habari kuwa wabunge wa Kenya wamepiga kura kujitoa katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC), lakini mahakama hiyo inasema kesi dhidi ya Rais Uhuru Kenyatta na Makamu wake, William Ruto, itaendelea kama kawaida.
Kura hiyo imepigwa siku chache tu kabla ya kesi dhidi ya Ruto kuanza mjini The Hague, Uholanzi, ikiifanya Kenya kuwa nchi ya kwanza kuitisha kura kama hiyo bungeni.
Hata kama kura hiyo ya aina yake inatoa onyo kwa mahakama ya kimataifa ya uhalifu, hata hivyo haina uzito kwa kesi ya viongozi hao wa nchi hiyo ya Afrika Mashariki.
Bunge la Kenya linabidi lipitishe mswaada huo wa sheria katika kipindi cha siku 30 zijazo ili kuhalalisha hatua za kujitoa katika mkataba wa Roma.
Bunge la Kenya
Mswaada wa "kusitisha,aina yoyote ya mshikamano,ushirikiano na msaada" pamoja na mahakama ya ICC umeungwa mkono kwa wingi wa kura.
Jumanne ijayo mahakama ya ICC imepanga kufungua kesi dhidi ya makamo wa rais William Ruto kwa madai ya kufanya uhalifu dhidi ya ubinaadam..Anatuhumiwa kuandaa machafuko ya baada ya uchaguzi mwaka 2007-2008 yaliyoangamiza maisha ya watu wasiopungua 1100 na kuwalazimisha wengineo zaidi ya laki sita kuyahama maskani yao.
  Pia rais Kenyatta pia anashitakiwa lakini kesi yake itakuwa miezi miwili baada ya ruto kufika mahakamani kwa madai ya uhalifu dhidi ya ubinaadam,ikiwa ni pamoja na mauwaji,ubakaji,mateso na kuwalazimisha watu wayahame maskani yao.
Wote wawili,Kenyatta na Ruto,wanaopinga tuhuma dhidi yao,walisema wako tayari kushirikiana kikamilifu na mahakama ya kimataifa ya ICC.
Mwengine anaetarajiwa kufikishwa mahakamani mjini The Hague ni mkuu wa kituo cha Radio Joshua Arap Sang anaetuhumiwa kuchochea matumizi ya nguvu.
Katika mjadala moto moto wa bunge mkuu wa kundi linalodhibiti viti vingi bungeni Aden Duale alisema "kujitoa katika ICC ni kuilinda katiba na kuitakasa hadhi ya Kenya."
Lakini kiongozi wa upande wa upinzani Francis Nyenze amehoji kujitoa katika ICC kutaichafulia Kenya hadhi yake kimataifa.
Mwendesha mashtaka mkuu wa ICC Fatou Bensouda
Wanasiasa wengi wa Kenya wanaiangalia mahakama ya kimataifa ya ICC kuwa ni chombo cha "ukoloni mambo leo" kinachowaandama waafrika tu.
Licha ya uamuzi wa bunge,kesi zitaendelea
Muungano wa Jubilee unaowajumuisha pia Kenyatta na Ruto unathibiti wingi wa viti katika bunge la Kenya na baraza la Seneti ambalo limepanga kulijadili suala hilo hilo wiki ijayo.
Juhudi zozote za kujitoa zitahitaji zipitie katika Umoja wa mataifa utaratibu ambao unaweza kudumu angalao mwaka mmoja."Kujitoa katika ICC hakutaathiri hata kidogo kesi wala mashtaka" amesema msemaji wa ICC Fasdi El Abdallah katika taarifa yake.
Kura ya maoni au uamuzi wa serikali hautabadilisha jukumu la Kenya kushirikiana kikamilifu na ICC kuambatana na sheria za kimataifa.
Taarifa ya wizara ya mambo ya nchi za nje ya Marekani imeitaka serikali ya Kenya iheshimu kikamilifu ahadi zake za kuhakikisha wahanga wa matumizi ya nguvu ya baada ya uchaguzi mwaka 2007-2008 wanatendewa haki."
Shirika linalopigania haki za binaadam la Amnesty International limelaani uamuzi wa bunge la Kenya na kuonya uamuzi huo unaweza kuinyima Kenya "kinga muhimu kabisa ya haki za binaadam."

Binafsi naunga mkono uamuzi wa kenya japo ni mapema mno kutokana na kesi inayowakabili viongozi hao wakubwa. Ikumbukwe katika moja ya machapisho yangu niliwahi kuhoji uhalali wa mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) kushughulika zaidi na viongozi wa kiafrika, kwanini? Mbona hatuoni ICC ikiwashtaki wazungu, je wahalifu ni viongozi wa Afrika pekee na kama ni hivyo mbona isijengwe Afrika. Nina maswali mengi juu ICC kama ilivyo kwa umma wa Afrika. Ieleweke kuwa siungi mkono uhalifu wa viongozi wa nchi za Afrika bali nataka kuona wakishtakiwa na waafrika wenyewe na wakiwa katika bara la Afrika kwa msaada wa jumuiya ya kimataifa. Mbona Afrika imeweza kuendesha mashtaka ya mauaji ya kimbari ya Rwanda katika mahakama ya Kimataifa ya Arusha, Tanzania? 

Kuwashtaki viongozi wa kiafrika kule The Hegue, Uholanzi ni muendelezo wa ukoloni mambo leo na kuwaona waafrika kwamba hawawezi kujiendeshe masuala yao muhimu katika ardhi yao. Nawapongeza wabunge wa kenya kutaka kujiondoa kwenye mahakama hiyo, lakini ninao ushauri kuwa waunge mkono wazo lililotolewa na Raisi Kikwete wa Tanzania kuendeleza mahakama ya mauaji ya Kimabari ya Arusha ili iwe mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu kama ilivyo ICC, hapo tena Arusha itakuwa The Hegue ya Afrika na itendesha kesi kwa viongozi wa Afrika wanaofanya uhalifu.

habari kwa msaada ya DW.DE

Wednesday, 4 September 2013

Askofu Moses Kulola aagwa na kuzikwa kitaifa

 NduguMsomaji ukitazama picha za kuagwa na mazishi ya Baba yetu Askofu Moses Kulola ni kama kama kazikwa kitaifa kutoka na mahudhurio ya viongozi mashuhuri wa makanisa na serikali. Ama kwa hakika hata Jeshi la ulinzi (JWTZ) limeshiriki kikamilifu katika msiba huo katika kuwasaidia watu waliokuwa wanazimia kutokana na maombolezo.  
Landcruiser za kubebea wagonjwa wanapozidiwa na kuwakimbiza hospitali ya Bugando zikiwa tayari kwa yeyote atayehitaji huduma hiyo.

Askofu Eliudi Isanja wa Arusha


RPC wa Mwanza, Ernest Mangu                                                                          Chanzo: gospelkitaa.blogspot.com       

Tuesday, 3 September 2013

UKOMBOZI: LAZIMA TUWASAIDIE WATU KUTOKA (2)

LAZIMA TUWASAIDIE WATU KUTOKA (2)
Siasa za Tanzania zinaharibu maendeleo ya nchi, kelele nyingi huwapoteza watu kufikiri namna ya kendelea.
Watanzania wamewekeza muda wao katika siasa uchwara za nchi hii, wanalo tumaini kuwa siku moja wanasiasa watawakomboa... wengine wamesubri muda mrefu na sasa wamekata tamaa kwa kuwa chama fulani hakijawafikisha mahali wanapotaka.
Ndugu zangu utafiti wangu usio rasmi unaonyesha kuwa nchi nyingi zimefanikiwa baada ya watu wake kujitambua, kutambua hali zao na ktafuta suluhisho, na suluhisho kubwa ni kila mmoja kuimarisha uchumi wake kwanza na hasa kwa njia ya ujasiriamali. ukiitazama China ya leo ni tofauti na China ya miaka ya 60 tofauti kubwa ni kuwa wakati ule watu wake walijishughulisha na viwanda vidogo na huduma ndogondogo baadaye wakaunda viwanda vikubwa na hatimaye wanahudumia dunia.
Kama kila mtu akitafuta shughuli ya uzalishaji mali yoyote, akatumia ubinifu na ugunduzi ili kuboresha shughuli yake basi bila shaka yoyote tutaweza kuwa na uzalishaji mkubwa wa bidhaa ndogondogo ambazo zitapunguza ama kuondoa kabisa uagizaji wa bidhaa za nje na hapo tutakuwa tumetengeza ajira na kupunguza mfumuko wa bei.
WATANZANIA TUFANYE MAMBO MAWILI SAMBAMBA TUWE NA SHUGHULI ZA UZALISHAJI MALI WAKATI HUO HUO TUKIPAMBANA NA SIASA YAANI KUWALAZIMISHA WANASIASA WATENGENEZE SERA NZURI ZA KIUCHUMI ZITAKAWASAIDIA WATU KUENDESHA SHUGHULI ZAO NA KUWAPATIA MASOKO... Napinga kabisa watu wazima kwa vijana kukaa vijiweni wakicheza bao huku wakilaumu siasa za nchi hii eti haziwatoi.
Winston Churchill aliwahi sema huweza kufikia maono yako ikiwa utahangaika kuwatupia mawe mbwa wengi wanakubwekea...
======================================
TUKUTANE TENA KWENYE UKURASA HUU KIPINDI KIJACHO TUANGALIE JUU YA MFUMUKO WA BEI...