m

"If you want to conquer fear, don't sit at home and think about it. Go out and get busy. "

-- Dale Carnegie, motivational expert

Friday, 28 September 2012

MAAZIMIO YA KIKAO CHA CASETA UYOLE VETERANS(CUV)

Bwana asifiwe. 
Wapendwa, kwanza nawashukuru tena kwa namna mlivyoshiriki kwa ajili ya ufanikisha ibada na kikao cha leo Uyole Sekondari.
Ninayo furaha kuwataarifu Ex CASFETA wa Uyole Sekondari maarufu kama CASFETA UYOLE VETERANS(CUV) kuwa kama tulivyopanga tumekutana leo na kushiriki ibada kuanzia saa 12:30-14:20 na pia tukamekaa kikao na kidato cha nne na viongozi wa tawi .
Kikao cha CUV kimeudhuriwa na wanachama wauatao;
1. Upendo Malle
2. Martha
3. Peter Kapagi
4. Elly Mangula
5. Abner Zephania
6. Ikupa Mwakaje
7. Sunny Michael
Waliotoa udhuru ni;
1. Edmund Mbwaga
2. Xaveria Jonas
Waliopo vyuoni na kutoa udhuru
3. Emmanuel Nasson
4. Catherene Vicent
5. Tulipo Asangalwisye
6. Shadrack Mwakyusa.
MAAZIMIO
tumekubaliana kuwa;
CUV kiwe chombo muhimu kutukutanisha wanaCASFETA wote tuliwahi kusoma shule ya sekondari Uyole na ambacho kitatusaidia kutuunganisha ili kuhudumiana katika mambo mbalimbali ya kiroho na kijamii na matukio muhimu katika maisha kama
-Masuala ya harusi 
- ushauri katika masuala ya kiroho na kutiana nguvu kwa habari ya safari ya mbinguni.
-Kusadiana katika masuala ya kielimu kwa kuwa ni chombo kwa ajili ya yeyote aliyemaliza Uyole pasipo kujali kiwango cha elimu, kazi n.k
- kushauriana katika masuala ya kiuchumi yaani kazi, biashara na hata ujasiriamali
-Ni vema kila mwanaCUV akawa mjasiriamali endapo atakuwa ameajiriwa kazi katika sekta yoyote ili awe na uchumi safi  kwa ajili ya familia yake na kanisa.
- Kila mwanaCASFETA aliyemaliza Uyole lazma athibitishe anakuwa nguzo muhimu katika kanisa lake yaani atumike vizuri.
-CUV itakuwa sehemu muhimu kabisa ya kufanikisha mahafali ya kila mwaka ya CASFETA Uyole sekondari ili yawe mahaali bora kabisa na yenye nguvu.
 
Mambo ya kutekeleza
-Bwana atufanikishe kuwa watekelezaji wa maazimio ya chama
-Tutafute mawasiliano ya wanaCASFETA wenye sifa za kuwa CUV ili tuweze kuwtumia taarifa muhimu na kwa ajili ya mkutano mwingine tutakaopanga hapo baadaye.
mawasiliano yawe namba za simu, email n.k na yatumwe kwa 
Abner Zephania- 0765 316393
au tumia blog hii au email kakakapagi@gmail.com
Mwisho ni kuendelea kulea tawi letu la Uyole kila tupatapo nafasi na Bwana atatubariki.
 
Bwana akubariki kwa kazi njema ya huduma na umoja

Thursday, 27 September 2012

CHAMA CHA KIJAMII (CCK)

HOTUBA YA UTAMBULISHO WA CHAMA KIPYA CHA SIASA NCHINI CHA CCK

Utangulizi na Shukrani Ndugu wanachama, Waandishi wa habari Na Watanzania wote Leo hii ile ndoto ambayo ilikataliwa kutimia miaka miwili hivi iliyopita hatimaye imetimia leo. Ndoto ya kuweza kuwapatia Watanzania chaguo tofauti la kisiasa nchini lenye kubeba matarajio yao sasa limetimia. Kutimia kwa ndoto hii leo hii ni mwanzo tu wa safari ndefu ya kisiasa kwa wengi wetu.

Ni safari mpya lakini iliyojaa matumaini. Hivyo, ninayofuraha kubwa kuwaambia wanachama wetu waliotuunga mkono kila kona ya nchi hadi kufikia hatua hii kuwa hatutawaangusha kwani tumedhamiria kuchukulia imani mliyoweka juu yetu kwa uzito mkubwa na unaostahili. Kufika hapa tulipofika leo ni juhudi za watu wengi sana ambao hata nikiamua kuwataja kwa majina sitowezakuwatendea wote haki.

Hata hivyo, nitangulishe shukrani za dhati kwa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini kwa ushirikiano ambao wametupatia hadi kufikia hapa. Wametusahihisha tulipokosea, wametuelekeza tulipotaka ushauri na wakati ulipofika wa wao kufanya usaili wamefanya usaili wa wanachama wetu nchi nzima kwa weledi wa hali ya juu na kujiridhisha kuwa CCK siyo chama cha utani, siyo chama cha msimu, bali ni chama ambacho kimekusudia kujikita na kuzama kabisa katika jamii ya Watanzania na kuwa kweli chama cha jamii hiyo.

Nawashukuru wanachama na viongozi wenzangu ambao wametumia muda mwingi kwa kujitolea kufanya kazi mbalimbali za chama huku wakijua nyuma yake kuna kubezwa, kejeli, kuonekana vibaraka n.k

Hawa wametambua nafasi ya pekee ambayo CCK itakuja kufanya na hivyo waliamua kwa moyo wote kujitolea muda, vipaji na raslimali mbalimbali ili kuweza kufanikisha zoezi zima la kuwez akupata usajili wa kudumu. Ninawashukuru sana. Zaidi hata hivyo nawashukuru wanachama, mashabiki na wapenzi wetu ambao wamekuwa wakitutia moyo na kusimama pamoja nasi japo msukumo wa kutaka kukata tama ulipokuwa mkubwa hasa baada yale ambayo yalitokea katika mwaka wa 2010 ambao wananchi wengi wanajua.

Kutokana na matokeo ya wakati ule tulijifunza kitu kimoja kikubwa kwamba chama ni lazima kitoke kwa wanachama wenyewe. Hivyo, hiki ni chama cha wanachama, chama cha Watanzania.

1. Utambulisho wa CCK na Viongozi wake Napenda kutumia nafasi hii basi kuwatambulisha baadhi ya viongozi wa muda wa CCK ambao nimeambatana nao hapa ili kuweza kuuonesha umma kuwa chama chetu kimejipanga kuweza kujijenga kama chama cha siasa. Nitaanzia upande wangu wa kulia na kuwatambulisha kwenu viongozi hawa:

2.
Kwanini kimeanzishwa na kwanini kiitwe jina hilo Ndugu waandishi na wanachama, Swali kubwa ambalo bila ya shaka linahitaji jibu la moja kwa moja ni kwanini chama kingine kimeanzishwa Tanzania mahali ambapo tayari kuna vyama vingi vya kisiasa?

Swali hili ni swali ambalo litaulizwa labda zaidi na wanachama wa vyama vingine vya upinzani ambao wanaamini kabisa kuwa tayari kuna vyama vya kutosha vya upinzani na hivyo kuja kwa chama kingine cha upinzani itakuwa ni tishio kwa vyama hivyo vingine. Naomba nitoe sababu kubwa tatu tu za kwanini CCK kimeanzishwa na kwanini kinaitwa chama cha kijamii na siyo jina lolote jingine ambalo lingeweza kuonekana la kifahari fahari hivi. i. Hakuna chama kingine katika upinzani chenye msimamo kama wa kwetu.

Kama kungekuwepo na chama kingine chochote ambacho kinawakilisha hata nusu tu ya msimamo wa CCK tusingekuwa na sababu ya kuanzisha chama kingine lakini baada ya kupitia siasa za vyama vyote vya upinzani na kuona vyama hivyo vinavyofanya siasa zao tumegundua kuwa hakuna chama chenye msimamo na mtazamo kama wa kwetu kwenye masuala mbalimbali. Hili nitalielezea kidogo kwenye itikadi ya chama. ii. Wapo Watanzania wengi ambao hawajaridhika na vyama vilivyopo sasa.

Tangu upinzani urudi nchini mwanzoni mwa miaka ya tisini wamekuwepo Watanzania ambao hawajaridhishwa na mapendekezo ya kisiasa ambayo yametolewa na vyama vya upinzani vilivyopo hadi hivi sasa. Hawa ndio wale ambao waliamua kususia uchaguzi au wamebakia ni wapiga kura wa kuangalia majina ya watu na siyo chama chenyewe.

Kwenye taifa la watu karibu milioni 45 ipo nafasi ya kutosha tu kwa chama cha kwetu ambacho kimekuja ili kuwapa wananchi hawa chaguo walilokuwa wakilisubiria kwa muda mrefu. iii. CCK inaitikia changamoto za kizazi kipya; kizazi cha milenia mpya. Vyama karibu vyote vilivyopo sasa vinaitikia wito wa kizazi cha zamani; kizazi kinachopita.

Lakini CCK inaitikia changamoto za kizazi kipya siyo kwa kusahau ya zamani au kubeza kizazi kilichopita bali tunataka kuuleta ujumbe wa kizazi kilichopita kilichounda taifa letu kwenye kizazi kipya. CCK inataka kupokea kijiti cha kupokezana kwa vizazi kutoka kwa wale waliotutangulia. Ni chama kilichoundwa na kuanzishwa na vijana lakini kikiwa kimejikita katika hekima na heshima ya wazee wetu. Tunaamini wazee wetu watatuunga mkono na vijana watakuwa nasi vile vile!

Kwanini kinaitwa chama cha Kijamii?
Ndugu zangu, msingi wa mafanikio ya nchi yoyote ni msisitizo uliopo katika kuinua maisha ya jamii. Tunaamini kabisa kuwa sera zilizopo sasa zilizoundwa na CCM na serikali yake na hasa katika miaka kama ishirini iliyopita zimekuwa kinyume na jamii ya Watanzania. Tulipopata uhuru wazee wetu walitaka kuunda taifa “la jamii ya watu walio huru na sawa”. Miaka hamsini sasa baada ya uhuru jamii ya aina hiyo inazidi kutoweka nchini, na njozi hiyo ikiendelea kuwakimbia wengi. Watu walio “huru na sawa” wamebakia kuwa wachache zaidi tena ni wale wenye nguvu za fedha, siasa na nafasi!

Msisitizo wa kuipigania jamii yetu katika ujumla wake wote haupo tena. Hivyo CCK ni chama cha Kijamii kwa sababu msisitizo wa fikra zake, mwelekeo wa sera zake na maono ya uongozi wake ni kuijenga jamii ya kisasa ya Kitanzania. Jamii ambamo watu wake wote watajisikia ni sehemu ya taifa hili na ambapo wakubwa kwa wadogo, wanawake kwa wanaume, weusi na weupe, wa bara na visiwani wanafurahia matunda ya kuwa ndani ya taifa hilo.

Msisitizo wetu ni jamii yetu na sera zetu zitalenga katika kuonesha kuwa ni katika wingi wa tofauti zetu katika jamii yetu ndio utajiri wa taifa letu umefichika! Hiki ni chama cha jamii ya Watanzania! Siyo chama cha tunu fulani fulani tu za maisha! Ni chama cha Kijamii! Itikadi yake Itikadi ya CCK ni uhafidhina wa kijamii na kiuchumi.

Yaani, socio-economic conservatism. Itikadi hii msingi wake ni historia yetu kama taifa na kama jamii ya watu. Tunaamini kuwa tishio kubwa kabisa katika jamii yetu ni kuvunjwa vunjwa kwa familia ya Kiafrika na vile vile matumizi makubwa ya serikali kwenye mambo mengi ambayo kwa kweli serikali isingestahili kuwa inayafanya.

Hivyo, CCK ni chama ambacho kinataka kutetea na kuyahifadhi mambo ya msingi yanayoifanya jamii yetu kuwa ya Kiafrika katika ulimwengu wa kisasa na hasa kutetea na kulinda familia. Tunaamini kabisa kuwa sera zozote na mipango yoyote ya nchi ambayo haiweki mkazo katika kuipa nafuu na kuboresha maisha ya familia sera hizo ni za kutupwa mbali.

Kwa muda mrefu sasa nchi yetu imejiingiza kwenye sera zenye kutukuza kile kinachoitwa “soko” matokeo yake wakati wenye “soko” wakiendelea kufanya vizuri mamilioni ya familia za Watanzania wanaishi maisha ya wasiwasi wa kudumu. Hivyo, tunataka kupendekeza sera ambazo zitalenga kuinua maisha ya wananchi wetu na hivyo kuinua maisha ya familia.

Lakini haya yote yanahitaji uchumi wa kisasa. Uchumi ambao unajiendesha wenyewe kwa kiasi kikubwa na ambao unalindwa vizuri. Sera za sasa za CCM zimeshindwa kutengeneza uchumi wa kisasa na badala yake zimetengeneza uchumi ambao ni watu wachache wananufaika. Hatuwezi kujenga uchumi huo kama tutaendelea kuangalia nje ya Tanzania kwa kutafuta misaada na kukopa badala ya kuweka mkazo katika uzalishaji na ulaji wa ndani.

Hivyo, kinyume na vyama vingine vilivyopo tunatarajia kuwa chama ambacho kinahifadhi mambo ya msingi ya uchumi na kijamii huku kikihakisha tunajenga taifa la kisasa.

Katika kutengeneza itikadi hii mpya chama chetu kitachota pasipo haya wala kuomba radhi katika hazina ya hekima ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na kujifunza huku tukiboresha nadharia zake nyingi ambazo tunaamini ni msingi wa kujenga taifa la watu walio sawa na wenye kuheshimu utu wa watu wote.

HIvyo, tutapinga ubaguzi wa aina yoyote dhidi ya Mtanzania mwingine, tutapigania maadili bora ya viongozi na kuhakikisha kuwa misingi iliyiounda taifa letu ikiwemo kupigania umoja wa Afrika, usawa na haki vinasimamiwa tena. Hatutavumilia kauli za kibaguzi zitakapotolewa na kiongozi au taasisi yeyote; kama Mwalimu alivyosema “Tanzania ni ya wote, na Watanzania ni wote”

3. Malengo/maudhui yake Kwa ufupi malengo ya chama chetu ni kuboresha maisha ya jamii yetu kwa kutumia uwezo wote ambao tumejaliwa na Mwenyezi Mungu. Uwezo wa akili, maliasili, nguvu kazi na hazina mbalimbali tulizojaliwa. Katika kufikia malengo hayo tutashiriki katika siasa za nchi yetu na kusimamisha wagombea wanaotokana na wananchi wenyewe na ambao wataongozwa na misingi hii ya chama hiki kipya.

4.
Hitimisho na jinsi chama kilivyopokewa na wananchi Baada ya matukio ya mwaka 2010 ambapo tulitambua kuwa baadhi ya watu waliotaka kuanzisha chama pamoja nasi walikuwa na lengo la kutaka madaraka tu na siyo kutumikia wananchi tuliamua toka wakati ule kutoshirikisha watu wanaoitwa “vigogo” isipokuwa wale tu ambao hawana mpango wa kutumia chama chetu kupata madaraka ya haraka.

Hivyo, CCK iliamua toka mapema kabisa kuwahusisha wananchi moja kwa moja na kwa ushawishi wa hoja na kuwaonesha kuwa yawezekana chaguo bora liko nje ya vile ambavyo watu wamevipokea au kuaminishwa kuwa ndio chaguo pekee.

Hivyo, tumetiwa moyo jinsi tulivyopokewa mikoani na vijijini ambapo watu walikaa chini kutusikiliza na kutupa nafasi ya kuwashawishi. Hatukutumia magazeti au vyombo vikubwa vya habari na badala yake tumeenda vijiji na miji ambapo tumekutana na wananchi ambao baada ya kutusikiliza wengi walikuwa wanatuambia maneno ya matumaini kuwa “hiki ndicho chama walichokuwa wanakisubiria”. Tunawashukuru wananchi hawa hasa wakulima na vijana ambao wamechoshwa na sera mbovu zilizoshindwa kuboresha maisha yao.

5. Mfumo wa siasa hapa nchini Mojawapo ya matatizo makubwa ambayo yanatusumbua sasa hivi nchini na ambayo athari zake zinatoka kizazi kimoja kwenda kingine ni mfumo wetu wa kisiasa nchini. CCK inaamini kuwa mfumo huu wa kisiasa umepitwa na wakati na hauendani kabisa na matamanio ya kujenga taifa la kidemokrasia. Baadhi ya vitu ambavyo tunaamini vimepitwa na wakati na ambavyo vinahitaji kuondolewa mapema zaidi ni suala la ruzuku kwa vyama vya siasa.

Mfumo wa ruzuku uliingizwa kwenye siasa zetu na CCM kwa ajili ya kutafuta njia rahisi ya kupora raslimali zetu na kujinufaisha kwa migongo ya Watanzania. Hakuna sababu wala ulazima wa chama cha siasa kupewa fedha za umma kwa sababu tu ina watu waliochaguliwa kushika nafasi mbalimbali – huu ni wizi wa wazi! Sisi kama CCK tunataka na tutapigania hatimaye kuondolewa kwa mfumo huu wa ruzuku kwa vyama vya siasa kwani vinazawadia uzembe na ubadhirifu.

Iweje chama ambacho kimeshindwa kusimamia serikali yake na ufisadi umeshamiri chini yake bado kinapewa kila mwezi mabilioni ya fedha ambayo hayajafungwa na utendaji kazi wa chama hicho?

Yaani, haijalishi CCM inatawalaje lakini bado inalipwa kila mwezi na Watanzania! Hivyo, kinyume na vyama ambavyo vinaweza kudaiwa kuwa vimeundwa kwa ajili ya ruzuku CCK imeundwa huku ikiwa inatambua kuwa mfumo wa ruzuku ni wa hatari kwenye siasa zetu na kwa kweli ndio umechangia sana kuchelewesha kung’olewa kwa CCM madarakani!

Hivyo, katika mjadala wa Katiba Mpya sisi kama chama tutapigania na kuhakikisha kuwa ruzuku kwa vyama vya siasa zinafutwa ili kila chama kitegemee wanachama wake na akili zake kujiendesha. Kwani TANU ilipewa ruzuku na serikali ya Mkoloni ili ifanye siasa? Si ilitegemea wanachama wake? Kwanini kama wakati huo iliwezekana leo ishindikane?

6.
Ushirikiano na vyama vingine vya upinzani Tunapenda ieleweke mapema kabisa kuwa hatuna uadui na chama chochote cha upinzani na hatuna sababu ya kushindana na chama kingine cha upinzani ambacho malengo yake yanakaribiana nay a kwetu. Ugomvi wetu na mgogoro wetu ni Chama cha Mapinduzi na uongozi wake kwa taifa.

Hivyo, tunatangaza uadui wa kudumu na CCM na tutashirikiana na chama chochote kile ambacho kina lengo la kuona CCM inaondolewa madarakani. Hata hivyo, ushirikiano huo utategemea kukubaliana kwa sera mbalimbali siyo kukubaliana kwa kuondoa CCM tu madarakani.

Endapo hata hivyo, hatutaweza kufanya kazi na vyama vingine vya siasa kwa msingi wa kukubaliana kisera basi sisi wenyewe tutaendelea na juhudi zetu za kuona kuwa serikali ya CCM inadhoofishwa na hatimaye chama hicho kuondolewa madarakani kwa kutumia nguvu za kidemokrasia. Hivyo basi, tunanyosha mkono wa ushirikiano kwa vyama vingine vya upinzani nchini kuwa tuko tayari kushirikiana nao kwa namna ile ambayo vyama vyetu vitakubaliana.

7.
CCK kama chama kipya Chama chetu kina vijana wengi na vile vile nyuma yake wapo wazee ambao hekima yao tunaitegemea. Kina upya wa aina yake lakini vile vile kimejengwa kutoka katika misingi ya taifa. Hivyo, ni chama ambacho ni kipya lakini kinataka kujenga kutoka misingi ile ambayo CCM imeivunja vunja.

Kwa kweli ni chama mbadala hasa wa CCM na kinataka kuwarudishia wananchi wa Tanzania fahari yao. Tunataka kurudisha ule moyo wa uzalendo, kuipenda Tanzania na kuona fahari kuwa sisi ni Watanzania.

Hiki ni chama ambacho wananchi wamekuwa wakikisubiria. Hakina majina makubwa, hakina uwezo mkubwa wa kifedha na hakina raslimali nyingi za kutamba nazo lakini tulichonacho ni ujumbe wa wazi wa mabadiliko ya kweli yenye kutaka kulifanya taifa letu la kisasa kwa kusimamia sheria, uhuru wa habari na maoni, utu na usawa. Hivyo tunawakaribisha Watanzania wote ambao wamekuwa wakisubiria chama kama cha kwetu kujiunga nasi.

8. Hitimisho Kwa vile leo ni siku ya kwanza kutambulisha chama sitopenda kuzungumza mengi zaidi kwani nina uhakika siku zijazo tutaweza kuzungumza mengi zaidi. Sasa hivi kama chama tunajukumu la kujiandaa kuunda uongozi wetu wa kudumu na kujipanga zaidi kama chama na kuhakikisha tunakijenga chama mikoani.

Vile vile sitozungumza mengi zaidi kwa sababu tuna chaguzi mbalimbali ambazo zinakuja na tunataka kuangalia ni jinsi gani tunaweza kushiriki au kuunga mkono mgombea wa chama ambacho tunaamini kinawakilisha matarajio ya jamii husika.

Tunawashukuru kwa kuja kutusikiliza na kutupa nafasi ya kuwapelekea ujumbe kwa Watanzania kuwa “Mabadiliko ni sasa, na mabadiliko ni sisi”! Hatutasubiri tena watu wengine watuletee mabadiliko kwani mabadiliko ni yale ambayo sisi wenyewe tunajiletea. Asanteni. Constantine B. Akitanda Mwenyekiti CCK -Taifa

Copied from jamiiforums.com

Monday, 24 September 2012

FURAHA YA KANISA

Furaha ya Kanisa

Furaha ni hali isiyoshikika inayomtokea mtu pale anapopata jambo nzuri, habari njema au anapokuwa na amani moyoni, naweza kusema furaha si amani bali amani huweza kuoneshwa kwa furaha. Furaha inaweza kuwa ya muda mfupi(temporary) au kipindi kirefu (permanent).
Isaya 35:10 … na furaha ya milele itakuwa juu ya vichwa vyao..
Ukweli ni kwamba kuna kundi kubwa la watu ambalo halina furaha katika jamii ya kikristo, kuna wapendwa bado hawana furaha kanisani.
Hivyo ni lazima kufanyike jitihada ya pamoja kati ya mwamini/mshirika na kiongozi ili kuleta furaha kanisani au katika jumuiya ya kikristo.
Kwa mfano mwaka 2011 radio DW ilitangaza kwamba kanisa la RC nchini ujerumani linapoteza umaarufu kwa 70%, hapa suala si dhehebu bali ni ukristo. Unafikiri kwa nini ? Sababu kubwa ya kupoteza umaarufu ni kwamba waumini hawana furaha tena kanisani na hivyo wanaamua kutafuta furaha mahali pengine. Kama waumini wanaona kanisa(si RC bali kanisa lolote la kikristo) limeingia udhalimu kazi yake kukusanya sadaka na mbegu tu, kama kanisa limeingiza ndoa za jinsia moja na unajisi kwa watoto, kanisa linaona injili ya utajirisho na miujiza ndio imani  sahihi, litakuwa limewafanya waumini kuliona kama mahali pa wahalifu na wanyang’anyi wanaamua kulikimbia maana haliwapi furaha wanayoitaka.
Mathayo 21:13 akawaambia imeandikwa , Nyumba ya yangu haitaitwa nyumba ya sala; bali nivyi mmeifanya kuwa pango la wanyang’anyi.
Bwana Yesu mwenyewe anaona uharibifu ndani ya kanisa na hapendi kuona hali hiyo, hapendi kuona uhalifu wa ndani ya kanisa kama ifanyikavyo leo. Mfano mwishoni mwa mwaka 2011 nikakutana na mwanamke ambaye Bwana ake alidhulumiwa mamimilioni ya pesa na mtumishi mmoja huko Arusha, kwa kweli ukimuona yule mwanamke amechoka kabisa na maisha na nilipoongea naye akaoneka ni mkristo mwenye kulifahamu neno barabara na ndipo nikavutiwa kuzungumza naye na kunieleza jinsi walivyofanyiwa unyang’nyi na mtumishi na hata kupelekea bwana ake kufukuzwa kazi benki. Ipo mifano mingi ya nyang’anyi ufanyikao kanisani hata kupoteza furaha kwa waumini. Hata hivyo nikutie moyo kwamba bado kuna kanisa la kweli na furaha ya kweli tena iliyo thabiti.
Je furaha ya mkristo ni katika kutajirika, kuoa, kuoa na kuolewa au mafanikio yoyote?
La hasha Matendo 8:5-8 inajibu …6na makutano kwa nia moja wakasikiliza maneno yale yaliyosemwa na Filipo walipoyasikia na kuziona ishara…..8ikawa furaha kubwa katika mji ule.
Ni dhahiri kuwa furaha ya mkristo inaanzia kusikiliza maneno na hatimae kuziona ishara za maneno hayo. Furahaa ya mkristo ni matokeo ya kulisikiza na kulisoma neno safi la kristo na utendaji wa neno hilo na si propaganda nyingine.
Tena Yohana 16:24 inasema …ombeni nanyi mtapata, furaha yenu iwe timilifu.
Kumbe kupata kwa Bwana kunaikamilisha furaha na si kwamba ndiyo furaha yenyewe.
Kwa mfano injili ya utajirisho haina nguvu Ulaya na Arabuni maana wana utajiri mkubwa lakini bado wapungukiwa furaha ya kweli bado wana hofu na mambo mbalimbali. Kama ni mafanikio ya Nyanja zote wameyapata katika elimu, uchumi, sayansi na hata siasa lakini furaha bado ni tatizo la msingi kwao. Wao wanahitaji Yesu halisi ahubiriwe maana wengine ni wasomi bado wana hofu juu ya hatima ya maisha yao. Ikiwa kuna jehanam au la na nini hatima yao baada ya kifo.   
Hebu tupitie mambo matano yanayoleta furaha kwa mkristo
1.      Kumkaribia Mungu
Ni jambo la pekee kwa mkristo maana wakristo wengi wapo mbali na Mungu na imekuwa chanzo cha kutoiona furaha ya ukristo
Zaburi 73:28.. Mfalme Daudi anasema nami kumkaribia Mungu ni kwema kwangu…
Jambo jema kabisa kwa mkristo ni kumkaribia Mungu kwa maneno, matendo na kila jambo.
2.      Kwenda madhabahuni.
Huku ni kupiga hatua kuzungumza na Mungu kwa sala na maombi, kusifu, kuabudu na hata shukrani.
Zaburi 43:3-4 …4 Hivyo nitakwenda madhabahuni kwa Mungu, kwa Mungu aliye furaha yangu na shangwe yangu….
Kumbe ni Mungu(Yesu Kristo) ndiye furaha ya mkristo na MUngu huyu napatikana madhabahuni, na hapa madhabahu ni sehemu yoyote ifaayo kumsifu, kumuabudu na kumuomba Mungualiye hai.
3.      Kumwona Yesu
Baada ya kumkaribia na kwenda madhabahuni jambo linalofuata ni kumwona Yesu.
Yohana 20:20 inasema …basi wanafunzi wakafurahi walipomwona bwana.
Hapa ni zaidi ya kuona kwa macho ya nyama bali kushiriki na katika matendo mbalimbali, huduma na maombi na zaidi kuomba na kujibiwa. Wakristo wengi wamepata furaha baada ya kuona matokeo ya maombi na imani katika maisha yao. Kujibiwa maombi si imani yenyewe tu bali kunachochea imani na furaha ya mkristo.
4.      Kumkaribisha Bwana.
Kumkaribisha bwana ni kule kumfanya awe sehemu ya maisha yako, awe wa kwanza kwa kila jambo, kila mahali na wakati wote kutembea na bwana Yesu.
Luka 19:5-6 habari ya zakayo ..6 akafanya haraka, akashuka, akamkaribisha kwa furaha.
Ni hakika kuna wakristo wengi hawajamkaribisha bwana Yesu katika maisha yao, nyumba, kazi na biashara zao na hivyo siku zote zimekuwa za taabu na mashaka. Fanya haraka kama Zakayo ambaye aliposikia Bwana Yesu anataka kuingia nyumbani kwake na kushinda humo akamkaribisha kwa furaha.
5.      Kujifunza kwa Bwana Yesu
Mkristo ni lazima akubali kujifunza kwa Bwana wakati wote na hatua kwa hatua ili aone furaha kamili ya ukristo.
Yeremia 15:16 inanena maneno yako yalionekana, nami nikayala: na maneno yako yalikuwa ni furaha kwangu maana nimeitwa kwa jina lako, Ee Bwana wa majeshi.
Mnenaji hapa si kwamba tu aliona maneno bali aliyala, akayatendea kazi na hata kujifunza kwa maneno hayo na ndipo akapata furaha na shangwe na hata kutambua kuwa ameitwa kwa jina lake(Bwana) sawa kabisa na wa wakristo wa leo ambao kwa sababu wamegoma kujifunza neno basi hata hawatambui kwamba wameitwa kwa jina la Bwana (Kristo).
Ninaweza kumaliza maneno machache kwamba kuna kanisa la Kweli, ukristo wa kweli na ambao umejaa furaha kwelikweli. Karibu katika furaha ya milele ya wokovu.
Filipi 4:4 inaisistiza furahini siku zote.
Katika safari
Kapagi

CASFETA UYOLE VETERANS (CUV)

Bwana asifiwe

Wapendwa, kwanza nawashukuru kwa namna mlivyoshiriki kwa ajili ya ufanikisha mahafali 8 ya CASFETA Uyole Sekondari.
Ninayo furaha kuwataarifu Ex CASFETA wa Uyole Sekondari maarufu kama CASFETA UYOLE VETERANS(CUV) kuwa tumekubaliana kukutana siku ya ijumaa ya tarehe 28 sept, 2012 kwa ratiba ifuatayo;
Saa 12:20-13:30- Tutashiriki ibada ya tawi la Uyole (Nyumbani kwetu)
Saa 13:30-13:45- Tutazungumza na uongozi wa tawi CASFETA Uyole Sek.
Saa 13:45-14:30- Tutakuwa na kikao chetu binafsi wanaCUV ili kujadili mustakabali wetu na ajenda mbalimbali zitakazoletwa na wanachama( akiwemo wewe unayesoma sasa taarifa hii)
Tafadhali mpendwa USIPUUZE HATA KIDOGO yapo mambo mazuri na zaidi umoja kwa kazi njema ya Huduma.
Efeso 4:5
Upatapo habari hii mtaarifu na mwingine.

N.B MwanaCUV ni mwanaCASFETA yeyote aliyemalza Uyole Sekondari mwaka wowote na kwa jinsia zote wanaoendelea na uanafunzi na hata wasio shuleni.

Ubarikiwe.

Kumfuata Yesu

KUMFUATA YESU KUNAH1TAJI MAAMUZI NA KUFAHAMU KUWA : 
(LUKA 14:27-33)
WANATAKIWA WATU WALIO TAYARI KUJITESA/KUTESWA NA KUFANYA KAZI NYINGI TENA NDOGO NDOGO NA KWA MDA MREFU USIOJULIKANA NA KWA MALIPO YASIYOJULIKANA NA KWA MSHAHARA USIOJULIKANA AMBAO UTALIPWA KWA MDA USIOJULIKANA.
NA ALIYE TAYARI LAZIMA AWE NA SIFA ZIFUATAZO:-
1. AWE TAYARI KUFANYA KAZI ZAKE MWENYEWE ILI ASIWALEMEE WENGINE ISIPOKUWA KAMA WATAMPA KWA KUPENDA (SIO KWA UJANJA UJANJA WA KUWATISHIA LAANA). 1THES. 4:11-12, 2 THESA. 3:10-12, 2 KOR.8:1-5,9:7-8,
2. AWE TAYARI KUPOTEZA HESHIMA YAKE UTU WAKE NA HATA MALI/KAZI YAKE KWA SIKU ZA MWANZO AU HATA MPAKA MWISHO WA MAISHA YAKE.(MATH.19:27-29 FIL.3:7,8)
3. AWE TAYARI KUKONDA KWA SIKU ZA MWANZO NA HATA MPAKA MWISHO WA MAISHA YAKE (JAPO SI WOTE WANAOKONDA) KWA KUJITESA NA KUJIWAJIBISHA MWENYEWE KWA KUFUNGA "MARA KWA MARA" (ILA KWA KUZINGATIA NA KUFUATA KANUNI ZA KUFUNGA/KUFUNGUA ILI ASIDHURIKE KWA SABABU ZA UJINGA). KUKESHA KWA MAOMBI, AU KWA KUSOMA BIBLIA NA KUTAFAKARI UWEZO WA MUNGU N,K. (1 KOR.9:27 2 KOR. 11:27.) (NINAPOSEMA MARA KWA MARA NAMAANISHA ZAIDI YA SIKU MBILI KILA WIKI AU SIKU NANE KILA MWEZI HATA KAMA Nl ZA MASAA 12 YAANI ASUBUHI HADI JIONI.)
4. AWE TAYARI KUOMBA ZAIDI YA SAA MOJA KILA SIKU AU MASAA SABA KILA WIKI BILA KUJALI KAZI ANAYOIFANYA AU WATU WANAOMZUNGUKA.(1 THES.5:17)
5. AWE TAYARI KUTENGWA KUTESWA NA JAMAA AU NDUGU ZAKE KUFUNGWA GEREZANl AU KUUAWA NA WATU WA TAIFA LAKE AU JINGINE KWA SABABU YA IMANI YAKE HIYO.(YOH.16:1-4, MDO.21:13, 2KOR. 11:23-26, UFUN.6:9-11) NA KWA KIPINDl CHOTE HICHO ASIMTAMKIE WALA KUMTAKIA MTU YEYETE MABAYA. (MDO.7:59-60, EBR. 4:15,RUMI. 12:14,20)
6. AWE TAYARI WATU WAMWAGE DAMU YAKE LAKINI ASIFANYE DHAMBI. YAANI AJILINDE NA DHAMBI YA AINA YOYOTE AWAPO KATIKA HALI YOYOTE IWE YA TAABU, MISIBA AU SHEREHE, IWE YA NJAA AU RAHA, KUDHARAULIWA AU KUPENDWA N,K. (EBR.12:4, 2 KOR,6:3-10, RUMI.8:35-39)
7. AWE Nl MTU ANAYEJITUMA SANA KWA MAMBO YAONEKANAYO KUWA MADOGO MADOGO, BILA KUJALISHA ELIMU YAKE AU CHEO CHAKE AU UMRI WAKE AU JINSIA YAKE. BALI AJIFANYE KUWA MDOGO KULIKO WOTE KWA KUFANYA MAMBO YOTE MEMA KUWAZIDI WENGINE. NINAPOSEMA MADOGO MADOGO Nl KAMA;KUWAHI KUWEPO KATIKA KILA (KAZI) KIPINDl KINACHOMHUSU, KUFANYA USAFI KANISANI AU VYOONI, KUWATEMBELEA WATU WENGINE N,K. (MATH.20:27, LUK.19:17)
8 ASIPENDE VYEO WALA KUONEKANA WA MAANA KULIKO WENGINE WALA KUTAKA KUITWA MAJINA YADHANIWAYO KUWA NDO YA WAKUBWA YAANI KUITWA MTUME AU MCHUNGAJI, AU NABII, AU MWINJILISTI AU MWALIMU, AU ASKOFU AU MKURUGENZI AU MENEJA N,K. (YAK.1:9f MARK.9:33-37 MATH.20:25-27, MATH.23:9-12)

Monday, 17 September 2012

CASFETA UYOLE VETERANS(CUV)

MAHAFALI YA 8 CASFETA 2012

Bwana asifiwe

Wapendwa.. kwanza nawasalimu baada ya kutoonana kwa muda mrefu kabisa. Natumaini mnaendelea vema katika mambo yote kwa uweza wa Bwana wetu Yesu Kristo.

Mwaka jana wakati wa mahafali ya 7 ya CASFETA sekondari ya Uyole tulikubaliana kuwa tutakuwa tunayatumia mahafali ya kila mwaka ya CASFETA Uyole kama sehemu muhimu yakukutana baada ya mwaka mmoja wa masomo na shughuli mbalimbali.

Mwaka huu mahafali yamewadia yatakuwa Jumamosi tar 22 septemba. Tafadhali pamoja na kukukumbusha kutoyakosa pia watoto wanaomba tuwachangie chochote tulichonacho ili kufanikisha mahafali hayo muhimu.
Siku hiyo tunakaribisha ajenda motomoto kwa ajili ya kuboresha umoja wetu wa wana Uyole(CUV)

Ikiwa utataka kuchangia tafadhali wasiliana na Abner Zephania kwa 0765 316393.

Mara upatapo habari hii tafadhali mtaarifu na mpendwa mwingine kwa haraka.

Efeso 4:3
Jitahidi kuuhifadhi umoja wa Roho katika kifungo cha amani”
 
Wenu katika utumishi
Peter Kapagi
 

Umoja kwa kazi njema ya huduma

Wednesday, 5 September 2012

Nguvu ya Neno

SOMO:   NGUVU YA NENO
MUWASILISHAJI:     Peter Kapagi
Tukisoma waebrania 4:12 isemayo
Utagundua mambo yafuatayo juu ya neno la kristo;
1.    Lina nguvu, nguvu huwezesha jambo litendeka au kazi yote ifanyike. Neno lipo kuwezesha mambo ya mwammini yafanyike hata kama haikuwezekana mbele ya neno lazima yawezekane na yatendeke tu.
2.    Neno li hai- maana yake lipo katia utendaji wakati wote masaa yote bila kupumzika.
3.    Neno lina ukali, lina magumu yote unayoweza kukumbwa nayo.
4.   Lina choma, linaweza kutenganisha vidhaifu na vyenye nguvu na mkristo haimpasi kuwa na mambo dhaifu na yenye nguvu kwani imempasa kuwa na vyenye nguvu tu.
5.    Linatambua mawazo ya moyo, yaani linaweza linaweza kukuonya na kukuongoza kila linapotambua mawazo ya moyo wako.
Neno linaweza kuyatenda hayo kwa sababu neno ni Kristo mwenyewe kama Yohana 1:1-4 isemavyo
KAZI KUU ZA NENO
Maombi pasipo neno ni bure kwa sababu maombi ni utekelezaji wa neno na ni lazima kwanza ujifunze neno au uitwe kwa neno au uisikie sauti ya bwana Yesu ikibisha ndani yako kwa neno ndipo uombe.
Injili na huduma yoyote yenye kuhitaji mafanikio katika mambo yote inahitaji neno lenye nguvu maana hapo ndipo zile kazi/ sifa tano tajwa hapo juu zinaweza kufanya kazi na kuthibitisha utukufu/ uwezo wa Bwana Yesu.
Neno linalaani na neno linabariki neno linajenga na kuumba na neno linabomoa