Tuesday, 12 November 2013

SIRI SIRINI, SOMA HAPA



RIPOTI YA SIRI JUU YA ZITTO KABWE

KWA

CHADEMA

UCHUNGUZI WA MWENENDO WA KISIASA WA ZITTO Z. KABWE NDANI NA NJE YA CHADEMA.

UTANGULIZI:Tangu mwaka 2008 mwenendo wa kisiasa wa Zitto Zuber Kabwe ulianza kutiliwa shaka na wanachama wa CHADEMA ndani na nje ya chama, Hili lilipelekea kuibuka maneno ya chini kwa chini kuwa anakisaliti chama.
Hilo liliilazimu timu ya kijasusi ya chama kuanza kufuatilia nyendo zake kwa ukaribu zaidi usiku na mchana ili kujiridhisha pasipo kuacha chembe ya mashaka. Ifahamike kuwa chama kina idara ya ulinzi na usalama wa chama na viongozi wake yenye uwezo wa kufuatilia nyendo za majasusi wa nje na viongozi na wanachama wake popote walipo kwa masaa 24. Baada ya

kujiridhisha kuwa mwenendo wake ni wa mashaka, bila kusita timu ya ujasusi ilianza kazi rasmi ya ujasusi dhidi ya nyendo zote za Zitto Zuberi Kabwe

No comments:

Post a Comment