Saturday, 1 June 2013

Ziara ya Obama nchini yazua malumbano

ZIARA ya Rais Barrack Obama wa Marekani imewagawa Watanzania huku wengi wao wakionyesha hofu kubwa ya viongozi wa mataifa makubwa kuwa wanakuja kwa nia ya kupora rasilimali za nchi. Wakati Watanzania wakiwa na hofu, Wakenya wamelalamika kupitia mitandao ya jamii kitendo cha Rais Obama kuwatenga wakati chimbuko la baba yake ni kutoka Kenya.
Wakizungumza na MTANZANIA kwa nyakati tofauti jana baadhi ya wananchi walisema wanashangazwa na ziara ya Rais Obama ikiwa ni miezi michache baada ya ziara ya Rais Xi Jimping wa China ambaye alitia saini mikataba 17 ya maendeleo.

Naibu Katibu Mkuu Bara wa Chama cha Wananchi (CUF), Julius Mtatiro alisema kitendo cha nchi kupokea wageni wakubwa wa mataifa makubwa ni heshima kwa nchi lakini inategemea kiongozi huo amebeba ajenda gani.

Naye Katibu Mkuu wa Baraza la Vijana wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (BAVICHA), Deogratus Munishi alisema Tanzania ni uwanja wa mapambano kwa mataifa makubwa kutokana na rasilimali zake.

Munishi alisema uchumi wa mataifa makubwa unategemea soko na rasilimali za mataifa madogo na akisisitiza kwamba madini ya uranium ndiyo chanzo cha viongozi wakubwa kukimbilia Tanzania.

Katika ziara yake ya kwanza katika Afrika, Rais Obama aliitembelea Ghana.

No comments:

Post a Comment